Kisa kipi kilikufanya ujute sana?

Sengerema secondary
 
Pole sana Mkuu,kuoa ni kama kamali. Ila mimi sitoicheza hiyo kamali.
Ndoa ni jambo la kheri,

Mke ni mama wa watoto wako,

Mke hukupa msimamo na heshima kwenye jamii

Mke ni mtu muhimu mwenye kujua shida zako kwa ukaribu zaidi kuliko hata wazazi waliokuzaa

Mke mratibu wa mipango mingi na mwenye kukukumbusha mambo mengi

Oa kijana kila mtu na mapito yake vitu vingine visikuchanganye

Mimi sijutii kuoa Bali najutia kumuoa huyu
 
Pole sana ndugu,Mjita alikuponza.
 
Majuto mengine yanatokana na tamaa. Sielewi hata ile akili tuliitoa wapi, Ila mm na mwanangu Shedrack tulipanga tuibe nguruwe wa shule tukauze. Kipindi hicho tupo O level, kwenye shule ya kanisa (seminary)...
Ooh aise pole San mkuu
 
Mkuu wapi ulielezea weka link[emoji3][emoji3][emoji3]

Check na hiyo mkuu [emoji3][emoji3][emoji3]
 
Nipo darasa la tatu hasubuhi mama kaniandaa kwa ajili ya kwenda shule vizuri tu na chai nimekunywa na nauli kanipa na pesa ya kutumia pia..

Sasa sijui alizubaa vipi? Si nikachukua/nikaiba pesa shs 400 tena mezani iliwekwa sijui ya nini? Poa nikasindikizwa mpaka kituoni nikapanda basi nikaenda shule baadae niliporudi.. ikagundulika kama ni mimi niliechukua pesa banah wewe.. mama alinitandika sana..

Nilipigwa sana yaani hakuna mfano wa kichapo kilee ukiringanisha na umri ule mdogo na moto nikaunguzwa kidogo mkononi.. ila ilinisaidia baada ya pale sijawahi kuiba tena yaani niliachana na habari ya kuchukua kitu cha mtu popote palee hata mtu akidondosha pesa/kitu na nimeona ntamuokotea na kumpa pesa yake.. ilinisaidia sana..

Cha ajabu nilipofika form 1 .. ilikuwa siku ya malipo mama na dada walikuwa wametoka kazini siku ya kupokea mshahara.. kufika home wakaweka mabegi yao mda huo mimi sipo nipo zangu kiwanjani nacheza mpira.. kumbe banah wameficha pesa zao za mshahara kwa sababu hawataki Baba apate pesa sijajua kama walikuwa na utaratibu wa kumpa pesa au laaah

Nimerudi zangu sina lile wala hili nimeoga zangu na kwenda tena nje kupiga story.. baadae nikaitwa kwa ajili ya chakula nikala..

Baba alivyorudi nilikuwa nimeshalala nikaamshwa na kuanza kuulizwa kuhusu pesa zingatia mda wote mama na dada hawakuniuliza kuhusu pesa kama ingekuwa kweli wameibiwa wangeniuliza kabla ya baba kurudi “ nikajua hapa wanataka kunisingizia tu..

Kikaanza kichapo daah nilipigwa sana bila sababu alaf ilikuwa usiku saa nne inaenda saa tano cha haibu zaidi baba akaanza kunitembeza kwa marafiki zangu kuwauliza kuhusu kuniona na pesa au laah.. marafiki zangu wanasema huyo kwanza sio mwizi wala hachukui cha mtu na leo hakuwa na pesa wala nini! Yaani nilipigwa sana kama mtu ambaye amechukua pesa lazma angesema tu cha ajabu nilikuwa napigwa na mwiko mpaka ukavunjika nikawa napigwa na bakora yaani ingekuwa sio wazazi wangu walllah sijui ingekuaje!!

Mambo yakaishaga maisha mengine yakaendelea sasa nimekua nimemaliza shule na nikaanza kazi sasa lile tukio linajirudia rudia kichwani nikafikilia ngoja nimuulize mama ilikuaje zile pesa mliibiwa kwenye daladala au ilikuaje!!

Mama nikimuulizaga ananiambia tu mwanangu naomba unisamehe sana na anakuaga na huzuni sana kila nikimuulizaga hayo mambo.. yaani analengwagwa mpaka na machozi najisikiaga vibaya sana na nimeachaga kumuuliza tena na kwa moyo wangu wote nimemsamehe sana ila natamani siku aniambie ukweli wa lile jambo lilikuaje!! Nahisi siku moja atanambia tu nimewasamehe ila likinijia kichwani huwa linanisumbua sana kichwa.. daaah baba alinipigaga sanaa kama sio mwanae vilee

Wababa msitoe hadhabu kwa watoto wenu kabla ya kuchunguza kosa..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…