Kisa kipi kilikufanya ujute sana?

COUNTERFEIT MONEY

Wakati bado nipo chuo kabla ya msala wa Receipt fake.. ilikua ni mwaka wa pili kama sikosei sem ya pili.

Hii story kama mhusika yuko humu JF atanijua rasmi mimi ni nani. Ila hakuna shida, cha kuogopa ni kifo pekee na bado kidgo kingenikuta!

Jamaa yangu mmoja nilikua naishi naye hostel nje kidgo ya chuo. Yeye kama ilivyo mimi hatukuwa na mkopo, na kwao hawakua vizuri kama ilivyo kwetu. Sema yeye alikua mtoto wa mjini kushinda mimi na alikua ameniacha parefu ki umri. Sema kuna vitabia flani hivi huwa vinafanya watu wanakua marafiki. Kwa namna yeye na mimi tulivyokua, ungeweza kutuita wazee wa michongo katika rejesta za kileo.

Kwa vile tulikua tunakaa room moja, vitu vingi kuhusu mimi vilikua wazi. Sina hela. Nimefulia. Sikua hata na confidence ya kusimamisha mwanamke nimtongoze. Akitaka tutoke out nitampeleka wapi? Kwa hela ipi? Kwaiyo nikawa ni mtu wa kutulia sana ndani na kuishi kikamilifu ndani ya ratiba za chuo na hostel. So unaweza ku imagine vile maisha yangu yalikua Boring!

Siku moja wakati tunapiga story za hapa na pale na jamaa akaniambia kuna mchongo wa siri anataka kunishirikisha. Nikatega sikio vizuri. Akaniambia kuna jamaa anamjua tukimpa kiasi fulani halali anaweza kututumia hadi mara nne yake ya bandia. Kwaiyo sisi kazi yetu ni kutafuta changes (Chenchi) tu ili tupate za halali.

Duh, wakati ananiambia mimi natetemeka. Nikamwambia mwanangu hii issue si inaweza ikatufanya tufungwe kabisa? Akaniambia "Ufungwe na nani?" .. "Tulia nikuoneshe", na mimi nikatulia.

Jamaa akaagiza mzigo, ukafika. Ilikua kama Mil 1 hivi ya Bandia. Nikamuona kwenye zile pande mbili za kuwekea hela kwenye Wallets; upande mmoja kaweka pesa halali kama 30K, na upande mwingine kaweka bandia kama 100K (Laki). Kaoga kamaliza, huyoooo kasepa!


Alikua ni mtu wa viwanja sana, sikumsikia wakati anarudi usiku. Kwaiyo kesho yake ahsubui namuona kakaa kwenye angle ya kitanda anahesabu hela, Duh. Ni kaki na buku be za kutosha. Mshenzi kashikisha watu zaidi ya elf 90 za bandia. Kabaki na 10 tu. Mimi tamaa ikawa imeanza kugonga mlango, nikawa sitaki kuifungulia. Unajua ukiwa umefulia sana vishawishi ni rahisi sana kukuzidi nguvu. Nikaendelea kujikaza huku jamaa yangu anazidi kuagiza mizigo na anapiga hela vibaya mno.

Mimi nampiga tu vi mizinga vya hapa na pale mwisho wa siku nikajikuta na mimi kanigawia fungu la kuchekecha. Ilikua kama laki 5. Laki 4 bandia, laki 1 halali.

Kama uko viwanja pesa za kwanza unatoa halali, halafu unatafuta mhudum mmoja mwenye tamaa unampiga vi ofa vya Beer huku ukiandaa mazingira ya yeye tu kukuhudumia. Akianza kuchangamka unamsukumia hizo noti mdogo mdogo kama hatasanuka ndio imeisha hiyo. Kazi inakua imebaki kuhesabu changes(Chenchi) nikifika hostel.

Shetani ni mjanja sana. Huwa anakulinda ukiwa unaanza magendo halafu baadae anakutelekeza ukisha kolea. Ndio kilichonikuta mimi, sikumaliza hata mwezi kwenye huo mchongo. Mungu huyu ni wa kumshukuru sana! Nisingekua naandika huu uzi hapa sasa hivi.

Kuna mahali nilikuja kusoma kuwa "Katika magendo yoyote yale, daima epuka kuwafanyia watu wenye hali za chini [kama masikini na wenye disabilities] kwa sababu ina create a very bad luck".Mfano mzuri ni watu wanaoiba vipochi vya wa Mama barabarani au sokoni, nadhani mnajua kinachowakuta wakidakwa! Na ndio kilichoniponza, kwa sababu nilikua desperate sana kupata hela haraka haraka nikaanza kuwafanyia hako ka mchezo mpaka boda boda na dereva taxi. Eh bhana eeh. Kumbe walikua wakifika sheli wanakataliwa pesa zao, wengine mpaka wanaitiwa polisi mimi sijui.

Wakawa wamejipanga siku wakimkamata huyo anayetoa pesa za bandia wanamuua. Mimi sikua nafahamu, nilikuja kugundua baadae huko. Sasa kuna boda wawili ambao nilikua napenda sana kuwatumia katika mishe zangu ambao nilikua nawapa pesa halali, hao ndio walikuja kuniokoa siku nimebananishwa nataka kumalizwa.

Siku yenyewe ilikua hivi. Mida ya jioni nimetoka zangu misele nikapita kijiwe kimoja kipya cha toyo nika scan sura za wajomba nikamuona mmoja kama boya boya hivi nikamchagua anipeleke maeneo karibu na Hostel (Huwa napenda kushukia kwa nyuma kidgo). Sasa kosa la kwanza, sikuwa na pesa ya halali hata moja kwenye wallet.

Sijui ilikuaje nikatumia zote huko nilipotoka halafu sikukagua kabla sijapanda boda. Ile nimeshuka si nikampa jamaa ten. Akaanza kuikagua akakuta ni bandia, akanikwida shati faster. Akasema wewe ndio tulikua tunakutafuta. Nikawa nabishana naye pale kwani vipi, kama ni bandia huenda hata mimi nimeshikishwa nikatoa wallet nikachomoa ten nyingine kumpatia alivyoicheck nayo ni bandia. Mama yangu!

Akapigia simu washkaji wa kijiweni na wao wakapigiana simu na wengine wakajaa pale. Mimi najifanys sielewi nimepanick najisachi kila mahali. Akaja jamaa mmoja akasema huyu mnamuhoji wa nini nikapigwa kofi moja la maana mpka nikajikuta niko chini. Nikaanza kulia kwa huruma. Wahuni wengine wanasema litafutwe tairi nichomwe. Ghafla mmoja kati ya wale jamaa naowatumiaga mara nyingi akawa na yeye amefika eneo la tukio. Hapo nimesha shikwa shikwa sana mpaka shati limechanika. Sura yangu imeanza kufanana kabisa na ya mwizi. Moyoni mwangu nimeshakubali kuwa leo ndio mwisho wangu!

Jamaa kuniona si ndio akawambia mbona huyu ni mwanafunzi wa chuo namchukuaga sana. Boda wengine wakakataa kata kata kuwa hakuna huyu ni jambazi hakuna kutetea. Wengine wakataka ninyang'anywe pochi waangalie ID. Ndio wakaona kweli mimi ni mwanafunzi. Hapo nimeshalia nimechoka, nawambia mimi sio mwizi jamani, mtaniua bure tu, nawaelewesha kuwa nilikua na shida nikaamua kuuza simu yangu ya kupangusa nahisi wale jamaa niliyowauzia ndio wamenifanyia huo mchezo hata mimi sielewi kama ni bandia.

Wakanichukua wakanipeleka kituo kidgo cha polisi hakikua sana mbali na pale. Nikaandika maelezo yangu na wao wakaandika maelezo yao. Sikumaliza hata siku tatu jamaa yangu akaja na wenzake wawili kuniwekea dhamana. Mambo yalikuja kuisha lakini baada ya hilo tukio na jamaa yangu akaachana na hayo mambo kabisa.

Bado nakumbuka vile nilikua najuta na kusali kule kituoni. Kumbe kufa ni kitu kidogo sana. Nikasema nikitoka hapa naenda nyumba za ibada kutoa sadaka ya shukrani. Washkaji walivyoisikia issue yangu, waliniambia nina bahati sana. Lazima kuna kusudi la Mungu katika maisha yangu ndio maana nimeponea kwenye tundu la sindano.
 
Kwenye Maisha tunajifunza kutokana na makosa na makosa yanaleta majuto kabla ya funzo.

Aidha ufanye kosa kwa siri au hadharani, ni lazima likugharimu kwa namna moja au nyingine na hivyo kupelekea majuto...
Umenikumbusha kisa kimoja sema hawakukamatwa, hizo documents huwa zinafanyiwa editing to na software za Adobe. Jamaaa alikuwa anataperi wazungu.

Hivyo anafanya malipo ya dollars 200 Kisha documents ya benk inafanyiwa editing inasoma $4000. Etc. Ilikuwa kwenye malipo ya gold serikalini.

Hivyo anaenda kulipa za gram 20 Kisha mzungu anaambiwa nimekusanya grams 2000, Ili amtumie pesa. Siku ya siku jamaaa katoroka na simu kuzima. Nilishangaa kuona Hadi list za NBC bank nazo zinafanyiwa editing.
 
Wakati bado nipo chuo kabla ya msala wa Receipt fake.. ilikua ni mwaka wa pili kama sikosei sem ya pili..

Hii story kama mhusika yuko humu JF atanijua rasmi mimi ni nani. Ila hakuna shida, cha kuogopa ni kifo pekee na bado kidgo kingenikuta...
Mmmmh we jamaa misala yako si ya kitoto[emoji848][emoji848]

Na kila mchongo lazima udakwe
 
Angevuta ingekuwa bonge la msala...Mungu ni mwema...
Mkuu nilicho gundua maugomvi ya wazazi jua kuna upande una makosa na sisi kama watt wao wana tusisha sana,Na wazazi nao wanatupotezea kitu si sahihi.
Baadae huko wanajirudi na kuona hatuwajali...
 
Je!Umesha bahatika kupata mwingine wa kukupenda kama yule alietutangulia?
 
Ivi sisi watoto wa kiume na uwizi qu udokozi uko kwenye damu nn?

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
Hamna uko peke yako mkuu.
Tofautisha watoto wa kiume na wanaume.
Mwanaume haibi bali anatafuta kwa nguvu zake na kula jasho lake.

Kuiba sio uanaume ni utoto au subiri dunia ya wanaume ikufunze madhara ya kuchukua kitu cha mwanaume kilichotafutwa kwa nguvu, damu, jasho na akili ndio utajua maana ya uanaume.
 
Hahahahaha 821kj, mtu unaenda kudoji ziwani unarudi mda wa mzabuni , ikifika muda wa bustani unazama tena ziwani. Balaa linakuja muda wa kufoleni ..watu wako na namba zao.
 
😂😂😂😂 Sijui nifanye Siri 🤔🤔au nimwage🤣🤣..wanaumeeee qu........e
Na wewe pia.

Uliyataka mwenyewe hakuna kitu kinakuja tuu we ulkua unadhani dunia hii n wewe tuu ndo ulikuwepo ndo ujipange sasa
 
Aise nikimkumbuka yule mwanamke naishia kujuta kwa nini nilimgegeda siku ile....ndio safari yangu ya arv ilipoanza[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ni kama nakupata hivi. Tunafanana. Una ulemavu wowote?
 
Tobaaa kumbe we ni mhenga eeeh? Nimeghairi kukutongoza. Ni bibi kabisa
 
Uliishi maisha ya ukiwa sana
 
yaani wewe ni mi mi kabisa mkuu-mimi jana tu nimetoka kuwakiana na mmoja hapo Bungoni....kila kitu nalipa kuanzia ada,nguo,sikukuu,chakula etc,..halafu anawapigia simu rafiki zangu eti sihudumii mtoto.

mbaya sana
Nina mengi ya kuandika juu ya hili kifup Wewe n mm kabisa

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…