Kisa Kizito cha Mzee aliyemnyooshea Bakora Mwalimu Nyerere

Wivu tu kwa vile aliwazidi wazee wao mambo nengi sana kuelimu, maarifa na hekima
Huihui,
Bahati mbaya hukupata kuwajua wazee wetu wala hukupata kusikia mchango wao katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Historia hii umeisikia kwangu na bahati mbaya imekuumiza nafsi yako.

Sababu ya wewe kuumia ni kuwa imekudhihirikia wema wao na uzalendo wa hali ya juu waliokuwanao hawa wazee.

Kila hatua unawakuta kuanzia 1924 Dr. Kwegyir Aggrey alivyomshauri Kleist Sykes kuunda African Association hadi 1929 alipoiunda na 1933 alipounda Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika.

Kuandika historia ya maisha yake kabla ya kifo chake na mswada huu kufikishwa University of East Africa Department of History na kila kitu kuwekwa wazi.

Hadi 1950 Schneider Abdillah Plantan anashinikiza kuondolewa madarakani kaka yake Thomas Plantan aliyekuwa President wa TAA na Secretary Clement Mohamed Mtamila na kuwaingiza madarakani vijana wadogo Dr. Vedasto Kyaruzi na Abdulwahid Sykes.

1952 Nyerere anapelekwa nyumbani kwa Abdul Sykes na Joseph Kasella Bantu na 1953 Hamza Mwapachu anamshauri Abdul Sykes wampe Nyerere uongozi wa TAA na 1954 waunde TANU.

Mimi kuandika historia hii si kwa kuwa nina wivu au namchukia Nyerere.

Nimeandika kuweka sawa historia ya uhuru wa Tanganyika.

Historia ya Sheikh Suleiman Takadir ilifutwa.

Nimeiweka hapa ili tuijue na tujifunze kwayo.

Hii si chuki.
 
Ukitajiwa jina la Nyerere unapata tumbo la kuhara. Pole sana, ndiye shujaa wa Tanzania, Rais wa kwanza Tanzania na Baba wa Taifa.

Hizo ngonjera zako zitaishia misikitini kwenu tu
 
Maandiko yako yote ni Islamcentric , au unaitazama historia kwa miwani ya dini yako.
Unachohadithia ni tofauti na uhalisia.
Sasa utuambie kama Nyerere aliyetoka huko misituni, kama aliwashikia majambia "wazee wako" ili awaghilibu na kuwatawala.
Ninyi ndio mnafaa kukaa misikitini tu na kuhubiri dini kuliko kupotosha historia.

Hatupingi watu wa Pwani walishiriki kikamilifu kudai uhuru, lakini hawakuwa peke yao kama unavyo vutia ngozi ya uislamu kwako.
 
Ukitajiwa jina la Nyerere unapata tumbo la kuhara. Pole sana, ndiye shujaa wa Tanzania, Rais wa kwanza Tanzania na Baba wa Taifa.

Hizo ngonjera zako zitaishia misikitini kwenu tu
Huihui,
Mimi sikupata hata kwa mbali kufikiria kuwa kitabu cha Abdul Sykes mosi kitawaathiri baadhi ya watu kwa kiwango kama hiki chako cha kutoa matusi kwa ghadhabu.

Pili sikufikiria hata kidogo kuwa kitabu cha Abdul Sykes kitabadili historia si ya Mwalimu Nyerere peke yake bali kitabadili pia historia nzima ya uhuru wa Tanganyika.

Mimi uwanja wangu si msikitini.
Tazama hizo picha hapo chini:


BBC Glasgow Scotland 1991

VoA Washington 2011

BBC Dira ya Dunia​
 
Jidu...
Kama mimi nisingeandika historia hii basi ni hakika historia hii yote ingepotea.

Katika historia ya uhuru wa Tanganyika usingesoma majina haya ya waasisi wa African Association 1929: Kleist Sykes, Mzee bin Sudi, Ibrahim Hamisi, Ali Said Mpima, Suleiman Majisu, Zibe Kidasi, Cecil Matola, Raikes Kusi na Rawson Watts.

Ulipata kuyasikia majina haya?
Je ulipata kujua jina la mratibu wa safari ya Nyerere UNO 1956, Iddi Faiz Mafungo?

Ulipata kujua majina ya wajumbe wa TAA Political Subcommittee 1950: Mufti Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Said Chaurembo, Hamza Mwapachu, Abdulwahid Sykes, Steven Mhando (Steven Abdallah Mhando) na John Rupia.

Wewe hupendi kusoma historia uliyokamilika?


Kushoto Iddi Faiz Mafungo, Sheikh Mohamed Ramiyya, Julius Nyerere, Saadan Abdu Kandoro na Haruna Iddi Taratibu, Dodoma Train Station 1955/56​
 
Nakuambia tena, kadanganye watu wa msikitini. Hivyo vijarida vyako as long as havijaingia kwenye mtaala wa Wizara ya Elimu Tanzania havibadili kitu. Ongezeni tu kwenye hadidu rejea za kaswida
 
Hazina pekee ya historia ya Tanganyika iliyobaki.

Huyu mzee pamoja na ubinadamu wake, ni hazina kubwa
 
Nakuambia tena, kadanganye watu wa msikitini. Hivyo vijarida vyako as long as havijaingia kwenye mtaala wa Wizara ya Elimu Tanzania havibadili kitu. Ongezeni tu kwenye hadidu rejea za kaswida
Huihui...
Mimi sijapatapo kuandika kijarida:
Angalia vitabu hivyo hapo chini:




 
Huyu mzee Mohammes Said mbona haelezi juu ya biashara yz utumwa iloyowaathiri sana " wazee wake*.
 
Masopo...
Ungependa tuanze na biashara ipi ya utumwa?
Cross Atlantic Slave Trade au Belgian Congo?
Zote tu?
Na usijikite Belgian Congo, anzia hapa kwetu Tanganyika.
Na ueleze wale waiochukuliwa utumwa kwenda Uarabuni kilichowatokea na sasa wako wapi vitukuu vyao
 
Usilolijuwa ni usiku wa kiza.

Jambo lipi kubwa nililoliandika la kufanya nilisahau? Nyerere kununuwa sigara kwetu au kuwasahau wazee wangu?

Mimi nakumbuka hata nilivyokua nanyonya kifuani kwa mamangu.
Sina akili za kipoyoyo kama wewe.
Kumbe julius alikuwa anagonga fegi
 
Zote tu?
Na usijikite Belgian Congo, anzia hapa kwetu Tanganyika.
Na ueleze wale waiochukuliwa utumwa kwenda Uarabuni kilichowatokea na sasa wako wapi vitukuu vyao
Maso...
Anza kusoma Atlantic Slave Trade utueleze ulichojifunza.
 
Maso...
Anza kusoma Atlantic Slave Trade utueleze ulichojifunza.
Usibadili magoli to your convenience. Najua unakwepa swali kwa vile jibu unalijua.
Naongelea watumwa waiochukuliwa Uyaoni , Nyasaland, Urambo,East Congo.
Waliishia wapi?
Na uzao wao huko uko wapi?
 
Usibadili magoli to your convenience. Najua unakwepa swali kwa vile jibu unalijua.
Naongelea watumwa waiochukuliwa Uyaoni , Nyasaland, Urambo,East Congo.
Waliishia wapi?
Na uzao wao huko uko wapi?
Maso...
Ikiwa unaijua historia ya utumwa na walikoishia watumwa sasa mimi unaniuliza kwa sababu gani ilhali wewe ni mjuzi?
 
Maso...
Ikiwa unaijua historia ya utumwa na walikoishia watumwa sasa mimi unaniuliza kwa sababu gani ilhali wewe ni mjuzi?
Good, umekubali utumwa ulikuwepo East Coast ya Africa.
Sasa wewe mjuzi wa historia, tupe vituo vikuu vya kusafirishia watumwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…