Kisarawe: DC Magoti apiga marufuku shughuli za ngoma kuhusisha wanafunzi

Kisarawe: DC Magoti apiga marufuku shughuli za ngoma kuhusisha wanafunzi

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2016
Posts
15,835
Reaction score
23,776
1.jpeg


Wazaramo na wandengereko sasa wamefikiwa, mambo ya kula vitoto vya miaka 12 sasa basi !
Ila bwana DC Magoti kuna swali huku, ni utamaduni wa Wazaramo na wandengereko msichana akifika miaka 12[kuvunja ungo] anachezwa ngoma na anafundishwa na kungwi namna ya kufanya mapenzi, je na hili nalo la kuwacheza watoto liachwe?


Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Petro Magoti amepiga marufuku Watu kuandaa shughuli za ngoma kama vile mdundiko, unyago na sherehe za muziki na kuruhusu Wanafunzi kujumuika na kuserebuka kwenye shughuli hizo ambapo amemuagiza Mkuu wa Polisi Wilaya hiyo kwamba vitendo hivyo vikibainika akamate kuanzia Mpiga ngoma, Wazazi wa Mtoto, aliyepewa tenda ya muziki hadi gari lililobeba muziki huo.

“Mtu wa Maendeleo ya Jamii upo wapi?, malezi hapa ni zero, una Watoto? Mwanao yupo darasa la ngapi?, chekechea?, sasa fikiria Mwanao yupo darasa la tatu akapigwa mimba utajisikiaje?, si vibaya? ndio rahisi anavyojisikia vibaya hivyo kusikia Watoto wana mimba, kwahiyo andaa utaratibu wa semina na mikutano ya darasa la maadili kuanzia July mwaka huu kila Shule tuwe na mambo ya maadili, Mtu yoyote anayetaka kuweka nguvu kuhusu unyanyasaji wa kijinsia twende nae, ukiona Mtu ananyemelea kabinti kashule njoo niambie huyu alikuwa na Mtoto nimemuona anamshika chuchu tutamshughulikia vibaya mno!

 
Huyu ndiye DC Mpya wa Kisarawe aliyeaminiwa na Mamlaka ya Uteuzi, Angalieni vipaumbele vyake.

View attachment 3025814View attachment 3025815

Yaani unateua mtu hata miiko ya uongozi hajui! Hivi hii nchi imeishiwa watu wa kuteuliwa?
Nimesikia akiongea redioni leo nikasema nani huyu mbona anaonekana hana weledi kabisa, nikashangaa mno kusikia eti ni dc wa Kisarawe, kweli ccm imeishiwa watu kabisa.
 
Back
Top Bottom