Kisarawe: DC Magoti apiga marufuku shughuli za ngoma kuhusisha wanafunzi

Kisarawe: DC Magoti apiga marufuku shughuli za ngoma kuhusisha wanafunzi

Shida ni huko serikali kuu sio mkuu wilaya, utamaduni wa hovyo kufundisha watoto mambo ya kikubwa umepitwa na wakati.

Hizo ngoma zao za unyago wasubiri mabinti wakifika miaka 18 ndio wafanye hayo mambo, sio kwa watoto wadogo.

Badala ya kumpongeza mtu anaetetea haki za watoto ndio tunataka kuona kakosea.
 
Pwani na ngoma ni kichwa na macho, sasa awachokonoe ndio atajua.

KIla sehemu ambayo haiko sawa katika mwili huwa na athari ya moja kwa moja kwenye ubongo na akili
 
Wanasemaga hata mpumbavu akikaa kimya huonekana na hekima. Watu wengi tuliwaheshimu sana wakati wapo kimya. Muhongo, Kabudi, Chalamila et al
 
Ni kama sijaelewa,anachokataza ni hizo shughuli za ngoma kwa ujumla au anakataza wanafunzi kuruhusiwa kushiriki katika hizo shughuli?
Kama anakataza kwa ujumla kwamba ni marufuku watu kufanya shughuli za ngoma hilo hawezi na hatofanikiwa.
Wazaramo tutamfundisha jinsi mgeni ukifika sehemu ni namna gani unatakiwa kuishi na wenyeji wako, Unajua baadhi ya hawa ndugu zetu kutoka bara huko wakipata madaraka basi hujiona wao ndiyo kila kitu wanaweza kufanya chochote,hiyo siyo sawa.
Anakataza wanafunzi kuchezewa hizo ngoma
 
Back
Top Bottom