Kisarawe: DC Magoti apiga marufuku shughuli za ngoma kuhusisha wanafunzi

Kisarawe: DC Magoti apiga marufuku shughuli za ngoma kuhusisha wanafunzi

Ni kama sijaelewa,anachokataza ni hizo shughuli za ngoma kwa ujumla au anakataza wanafunzi kuruhusiwa kushiriki katika hizo shughuli?
Kama anakataza kwa ujumla kwamba ni marufuku watu kufanya shughuli za ngoma hilo hawezi na hatofanikiwa.
Wazaramo tutamfundisha jinsi mgeni ukifika sehemu ni namna gani unatakiwa kuishi na wenyeji wako, Unajua baadhi ya hawa ndugu zetu kutoka bara huko wakipata madaraka basi hujiona wao ndiyo kila kitu wanaweza kufanya chochote,hiyo siyo sawa.
 
Huyu ndiye DC Mpya wa Kisarawe aliyeaminiwa na Mamlaka ya Uteuzi, Angalieni vipaumbele vyake.

View attachment 3025814View attachment 3025815

Yaani unateua mtu hata miiko ya uongozi hajui! Hivi hii nchi imeishiwa watu wa kuteuliwa?
Anamuiga mzee wa Rombo akiwa mkuu wa mkoa wa Tabora, bwana harusi sukuma ndani, bi harusi sukuma ndani, mpiga ngoma suka ndani, mchagua mchele sukuma ndani, baba na mama wa bi harusi sukuma ndani..........
 
Anazuia mila za Pwani au sio?

Pwani huko Elimu hauna umuhimu kiviile kuliko mila zao pamoja na Uisilamia
kunema mwali hakuna uhusiano wowote na binti kutosoma, na hakuna uhusiano wowote na uislamu, ni tamaduni ya mila za makabila, ni sehemu ya elimu asilia ya jadi (jando na unyago) ya kumfundisha binti kuwa kavunja ungo anatakiwa ajielewe kama binti, wapo walio pitia mila hiyo na wakaendelea na masomo yao. halafu mkiambiwa ngoma nyie mnafikiria vigodoro vya kishenzi vya uswahilini dar es salaam, huko kisarawe kuna ngoma za asili sio hizi za mijini
 
Sasa watani zangu watakata wapi mauno maana tulikua tunaenda kukatiwa mauno na watani wangu kipenzi mpaka tunajichokea .Mh waache bwana mzararmo yuko radhi auze shamba amchezi mwanae ww unaleta katazo watakupiga shipa huko kisarawe uteseke nalo🤣🤣🤣🤣
 
Huyu ndiye DC Mpya wa Kisarawe aliyeaminiwa na Mamlaka ya Uteuzi, Angalieni vipaumbele vyake.

View attachment 3025814View attachment 3025815

Yaani unateua mtu hata miiko ya uongozi hajui! Hivi hii nchi imeishiwa watu wa kuteuliwa?
huyo namfananisha na mhusika mmoja kwenye novels za James Hadley Chase akiitwa Vitto Ferrari. Huyo kazi yake ni kutoa roho tu, ukimpa kazi ya kumuua mtu anakuuliza kuwa unataka ionekane vipi, yaani iwe ni mauji, mtu amejiua mwenyewe au ajali, vyovyote unavyotaka ndiyo itakuwa.
 
Back
Top Bottom