Kisarawe: DC Magoti apiga marufuku shughuli za ngoma kuhusisha wanafunzi

Kisarawe: DC Magoti apiga marufuku shughuli za ngoma kuhusisha wanafunzi

Ni ujinga na muda wao wa kukomeshwa mila za hovyo bado haukufika, sasa umefika na DC kazuia.

Zile ngoma ni za hovyo sana, mpiga ngoma akizima anachagua mwanamke yeyote yule anayemtaka hata km mke wa mtu akamle kichakani, akimaliza ndio ngoma inaendelea na hapo ni kundi zima linaingia vichakani kila mtu na wake.!! Hakuna kinga hapo ni kujibebea magonjwa.

Ndiomana wanaimba “Chakala chakala mikoroshini mamaa!! Waambulia gono la Mia mbili mamaa!!”
Acheni kashfa zenu kwa stori mnazopeana vijiweni,inawezekanaje mtu amtake mwanamke yeyote tu hata akiwa mke wa mtu na lazima eti huyo mwanamke akubali? Ukiona jambo kama hilo huyo mwanamke atakuwa amekubali mwenyewe labda kwa sababu ya umalaya wake tu na hakuna kitu kinaitwa sijui chakala chakala mikoroshini sema sehemu yoyote ya starehe na kwenye matamasha labda kutokana na ulevi mihemko ya ngono hujitokeza sana na watu hujikuta wanafanya matendo ya ovyo hata huko kwenye masherehe yenu nyie wenzetu mnaojiona mna mila nzuri mambo hayo hujitokeza na sisi tunayajua.
 
kunema mwali hakuna uhusiano wowote na binti kutosoma, na hakuna uhusiano wowote na uislamu, ni tamaduni ya mila za makabila, ni sehemu ya elimu asilia ya jadi (jando na unyago) ya kumfundisha binti kuwa kavunja ungo anatakiwa ajielewe kama binti, wapo walio pitia mila hiyo na wakaendelea na masomo yao. halafu mkiambiwa ngoma nyie mnafikiria vigodoro vya kishenzi vya uswahilini dar es salaam, huko kisarawe kuna ngoma za asili sio hizi za mijini
Acha ujinga
 
Acheni kashfa zenu kwa stori mnazopeana vijiweni,inawezekanaje mtu amtake mwanamke yeyote tu hata akiwa mke wa mtu na lazima eti huyo mwanamke akubali? Ukiona jambo kama hilo huyo mwanamke atakuwa amekubali mwenyewe labda kwa sababu ya umalaya wake tu na hakuna kitu kinaitwa sijui chakala chakala mikoroshini sema sehemu yoyote ya starehe na kwenye matamasha labda kutokana na ulevi mihemko ya ngono hujitokeza sana na watu hujikuta wanafanya matendo ya ovyo hata huko kwenye masherehe yenu nyie wenzetu mnaojiona mna mila nzuri mambo hayo hujitokeza na sisi tunayajua.

Ushawahi kushiriki ukaona?
 
Tamaduni zinafundishwa hadi mashuleni yeye anakataza vipi? Kwa maana hiyo mitaala ibadilishwe pia?
Hawa wajinga ndio wanamuangusha Rais, mbaya zaidi halioni hilo.
Yaani mambo mengine ni basi tu.
Yaani tukose pa kupumulia siyo?
Maisha na ugumu wake mliotusababishia, halafu hadi kwenye starehe zetu mnakuja kutuwekea kauzibe?
 
Wengi mnamshambulia kwa mihemko. Labda tumkosoe hilo la kutoboa matairi kwani kufanya hivyo ni jinai.
 
Huyu ndiye DC Mpya wa Kisarawe aliyeaminiwa na Mamlaka ya Uteuzi, Angalieni vipaumbele vyake.

View attachment 3025814View attachment 3025815

Yaani unateua mtu hata miiko ya uongozi hajui! Hivi hii nchi imeishiwa watu wa kuteuliwa?
Nimecheka sana,eti badala ya kutafakari waanzishe miradi ya kiuchumi ili kupunguza umaskini unapoteza muda kuanza kukimbizana na wapiga ngoma,wapiga ngoma hiyo ndio starehe yao ya kujiliwaza na umaskini walionao.
Yaani wakati matajiri wanakwenda kuburudika Serena hotel na Mlimani City hao maskini wa kisarawe starehe yao ndio hiyo ngoma.
Sitetei watoto kwenda ngomani au kupewa mimba ila kuna namna ya kufanya ili watoto wawe bize shuleni na kuisahau ngoma automatically na sio kwa kukimbizana na wapiga ngoma
 
Ni kama sijaelewa,anachokataza ni hizo shughuli za ngoma kwa ujumla au anakataza wanafunzi kuruhusiwa kushiriki katika hizo shughuli?
Kama anakataza kwa ujumla kwamba ni marufuku watu kufanya shughuli za ngoma hilo hawezi na hatofanikiwa.
Wazaramo tutamfundisha jinsi mgeni ukifika sehemu ni namna gani unatakiwa kuishi na wenyeji wako, Unajua baadhi ya hawa ndugu zetu kutoka bara huko wakipata madaraka basi hujiona wao ndiyo kila kitu wanaweza kufanya chochote,hiyo siyo sawa.
Mtani pigeni busha la kilo tatu huyo 🤣🤣🤣haiwezekani bwana awakataze watani wangu kujinafasi na mila zao.
 
Ni kama sijaelewa,anachokataza ni hizo shughuli za ngoma kwa ujumla au anakataza wanafunzi kuruhusiwa kushiriki katika hizo shughuli?
Kama anakataza kwa ujumla kwamba ni marufuku watu kufanya shughuli za ngoma hilo hawezi na hatofanikiwa.
Wazaramo tutamfundisha jinsi mgeni ukifika sehemu ni namna gani unatakiwa kuishi na wenyeji wako, Unajua baadhi ya hawa ndugu zetu kutoka bara huko wakipata madaraka basi hujiona wao ndiyo kila kitu wanaweza kufanya chochote,hiyo siyo sawa.
Le

Huyu jamaa hana weledi wowote wa uongozi! Kapewa nafasi tu ya upendeleo kutokana na ulemavu wake
 
View attachment 3025621

Wazaramo na wandengereko sasa wamefikiwa, mambo ya kula vitoto vya miaka 12 sasa basi !
Ila bwana DC Magoti kuna swali huku, ni utamaduni wa Wazaramo na wandengereko msichana akifika miaka 12[kuvunja ungo] anachezwa ngoma na anafundishwa na kungwi namna ya kufanya mapenzi, je na hili nalo la kuwacheza watoto liachwe?

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Petro Magoti amepiga marufuku Watu kuandaa shughuli za ngoma kama vile mdundiko, unyago na sherehe za muziki na kuruhusu Wanafunzi kujumuika na kuserebuka kwenye shughuli hizo ambapo amemuagiza Mkuu wa Polisi Wilaya hiyo kwamba vitendo hivyo vikibainika akamate kuanzia Mpiga ngoma, Wazazi wa Mtoto, aliyepewa tenda ya muziki hadi gari lililobeba muziki huo.

“Mtu wa Maendeleo ya Jamii upo wapi?, malezi hapa ni zero, una Watoto? Mwanao yupo darasa la ngapi?, chekechea?, sasa fikiria Mwanao yupo darasa la tatu akapigwa mimba utajisikiaje?, si vibaya? ndio rahisi anavyojisikia vibaya hivyo kusikia Watoto wana mimba, kwahiyo andaa utaratibu wa semina na mikutano ya darasa la maadili kuanzia July mwaka huu kila Shule tuwe na mambo ya maadili, Mtu yoyote anayetaka kuweka nguvu kuhusu unyanyasaji wa kijinsia twende nae, ukiona Mtu ananyemelea kabinti kashule njoo niambie huyu alikuwa na Mtoto nimemuona anamshika chuchu tutamshughulikia vibaya mno!

Kwa jinsi walivyo nalo watalihusisha na dini
 
Back
Top Bottom