Kisarawe: DC Petro Magoti ameutaka Msikiti unaotoa elimu ya dini kwa watoto 96, kuwarudisha walipowatoa sababu ya Mazingira Mabovu ya malazi

Tatizo bajeti
 
Kwanini madrasa iwe ya bweni wanafundishwa nini?
Si bora wapelekwe hata VETA
Mkuu ziko madrasa za bweni zipo za day.

Kama ambavyo zipo shule za bweni za zipo shule za day.

Kuuliz kwa nini madrasa iwe ya bweni ni sawa na kuuliza kws nini shule ziwe za bweni , na jawabu la hapo litaingia kotekote.
 
Nimekuelewa sana Mkuu
 
The best,
Wanachama wa mwanzo wa TANU wametoka Rufiji.

Angalia video.


View: https://youtu.be/xJ0XD6zis30?si=Dpiure6A3Q1cMX2A
 
Huyu jamaa kuna anachokitafuta

Kuingia tu anawakataza wazaramo wasitumie pikipiki kubeba mkaa!

Sasa hv kaingilia masuala ya dini ya kiislam.

Yetu macho tu...mbona Jokate aliishi vizuri na wana kisarawe?
Huyo mtu kwanza inaonekana ana roho mbaya ya asili,pili ana chuki ya kidini halafu ana dharau na kujiona anajua kila kitu,kwa roho mbaya yake aliyonayo ndiyo maana mwendazake alimpenda sana lakini huko alipokwenda na upuuzi wake atatulizwa tu maana atapewa mzigo mwingine aangaike nao kwa sasa ana kibiyongo ataongezewa na busha ndiyo atajua hajui.
 
Shekhe wangu Mzee Mohamed Said, kwa hili la Bagamoyo,ungeliacha tu lipite. Si jema kwa afya za watoto.
Kosa la mmoja halimhalalishi muovu
Big Bigstone,
Hao ni watoto wa masikini.
Hapo wako peponi.

Kuna shule mbovu hazijavamiwa.

Angalia nyuma nimeweka picha ya shule moja.

Waislam tumeishi na haya tunajua kinachotafutwa.
 
The best,
Mimi ni mwanafunzi wa historia na naandika kile ninachotafiti kwa uhalisia wake.

Sina sababu ya kuficha kitu.
Angalia jina la kitabu changu:

 
The best...
Sina tatizo na wewe kutokubaliana na mimi.

Kuna wengi wanokubaliana na mimi kiasi cha kunialika kwenye mikutano na vyuoni kwao kunisikiliza kuhusu historia ya uhuru wa Tanganyika.

Kwao ni ''field of enquiry'' ambayo haikupata kutafitiwa na wasomi wanahistoria wa Tanzania.
 
Big Bigstone,
Hao ni watoto wa masikini.
Hapo wako peponi.

Kuna shule mbovu hazijavamiwa.

Angalia nyuma nimeweka picha ya shule moja.

Waislam tumeishi na haya tunajua kinachotafutwa.
Acha Unafiki unafiki na Fitina Mzee, weka hapa kinachotafutwa...acha kujiliza
 
Mzee huwa anahamisha magoli hadi sio poa. Ni kama wale jamaa wa mihadhara ukiwauliza hiki wanapeleka mada kwingine.
 
Aliyekwambia kuna usiri ni nani? Nani alienda kuuliza kinachoendelea hakujibiwa? Wazazi hawana uwezo wa kupeleka watoto shule binafsi za sekondari mlitaka wafanye nini? Mtoto asijue dini yake kisa mzazi hana uwezo? Acheni chuki za kipumbavu nyie
Ujue sometimes huwa sielewu baadhi yenu ni nini hasa mnataka. Hakuna mwenye chuki na dini ya mwenzake hapa Bongo ni tofauti ndogo tu huwa zinajitokeza mara chache na bado tunashirikiana. Kwenye koo zetu tuna ndugu ambao ni Waislamu na Wakristu. Mimi kuwachukia Waislamu ni sawa na kuwachukia ndugu zangu, rafiki zangu.

Turudi nlipoanzia. Sometimes sijui baadhi yenu huwa mnataka nini. Hapo unashabikia watoto kuachishwa shule wasome dini, baadae tutakukuta kwenye uzi mwingine unalalamika kuna udini serikali inajaza Wakristo nafasi za ajira.

MBONA KAZI.
 
Binafsi naungana na Mkuu wa wilaya. kituo kama hicho kinatakiwa kiwe kimetimiza matakwa yote ya sheria.

Waislam tunatakiwa tuwe Makhalifa na mfano bora kwa jamii, Waislam kama hao wanaoendesha hicho kituo ndiyo wanautukanisha Uislam.
Sasa kama umekubali wewe sijui wengine wanapinga nini. Na sijui kwanini tunapojaribu kushauri au kukosoa mambo fulani tunaambiwa tuna chuki za kidini.
 
Huyo DC toka apelekwe huko ameonesha chuki za waziwazi kwa wenyeji wa huko na ni kama anajiona yeye ndiye anawaweza na atawakomesha,wacha tuone mwisho wake utakuwaje.
Poa poa tumekusikia. Turudi kwenye mada husika, unazungumziaje hilo tukio?
 
Madrassa zinaharibu usalama wa Taifa ila sunday schools aaaah?! Vyuo vya watoto wadogo wanaoenda kufundishwa upadre na utawa aaah haviharibu watoto?
Wanasema makundi mengi ya Ugaidi yameanzishwa na Marekani. Sasa jiulize kwanini ni rahisi kumalaghai kijana wa kiislamu ajivike bomu ajilipue kuliko wa imani nyingine.

Kuna muda sio vibaya kukaa chini kutafakari malezi tunayowapa vijana wetu.
 
Mzee watoto ni mali ya Jamhuri. Kwamba uwatendee tu unavyojisikia kwa kisingizio cha dini serikali ikae tu inakuangalia?
 
Wanasema makundi mengi ya Ugaidi yameanzishwa na Marekani. Sasa jiulize kwanini ni rahisi kumalaghai kijana wa kiislamu ajivike bomu ajilipue kuliko wa imani nyingine.

Kuna muda sio vibaya kukaa chini kutafakari malezi tunayowapa vijana wetu.
Sijui lolote kuhusu ugaidi wala sijawahi kuona wala kusikia ugaidi ukifundishwa misikitini. Tanzania hii wapi mtakaa kikundi cha watu 5 kujifunza ugaidi au kuongelea ugaidi bila ya serikali kujua? TIS s ina mtandao mkubwa sana kuliko kawaida. Ugaidi ungekuwa unasomeshwa misikitini na kwenye madrasa basi bila ya shaka serikali ingeshaifungia misikiti yote nchini.

Anachokileta petro magoti ni chuki dhidi ya dini ya kiislam na waumini wake
 
Kwanini madrasa iwe ya bweni wanafundishwa nini?
Si bora wapelekwe hata VETA
Mbona vyuo vya biblia huwa ni vya bweni? Mbona vyuo vya watawa na mapadre huwa ni vya bweni?

Elimu ya kumjua Mungu haihitaji world distractions. Quran ili uihifadhi inahitaji mazingira ya utulivu huku ukijitenga na vishawishi vya kidunia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…