Kisarawe: DC Petro Magoti ameutaka Msikiti unaotoa elimu ya dini kwa watoto 96, kuwarudisha walipowatoa sababu ya Mazingira Mabovu ya malazi

Kisarawe: DC Petro Magoti ameutaka Msikiti unaotoa elimu ya dini kwa watoto 96, kuwarudisha walipowatoa sababu ya Mazingira Mabovu ya malazi

Bagamoyo,
Rejea kwenye hiyo video uitazame na usikilize ukiwa makini.
Hakuna mwanafunzi yeyote kutoka nje ya Tanzania.

Rejea usikilize tena hao wanafunzi wengi wameishia darasa la saba na wameletwa hapo na wazee wao waje wasome dini.

Tatizo labda liko hapa.
Nimetumia neno ''labda'' kwa makusudi ili ikiwa lipo tatizo lingine lisemwe.

Ikiwa wewe ni Muislam hutopata tabu unapambiwa watoto wengi wa Kiislam huishia darasa la saba.

Kitwana Kondo alipata kulizungumza hili Bungeni.
Nakuwekea hotuba yake uisome.

(Hotuba ya Mh. Kitwana Kondo (MB) aliyoitoa Bungeni Dodoma, 1999)

Waislam waliofanyiwa mtihani wa kuingia kidato cha kwanza majority yaani wengi walikuwa Waislam na Wengine walikuwa ndiyo wachache.

Waliochaguliwa kuanza kidato cha kwanza wengi walitoka katika wale Wengine na Waislam wakawa wachache.

Waislam kwa kuthamini elimu ndiyo wanawapeleka watoto wao katika shule hizi za ''kimasikini,'' kusoma.

Hatuna ubavu wa kushindana na shule za Wengine ambazo zinapewa ruzuku mabilioni ya kutoka serikalini kupitia Memorandum of Understanding (MUM) katika ya Serikali na Makanisa.

Yapo mengi katika matatizo yanayowakabili Waislam moja wapo ilikuwa NECTA kuhujumu shule za Waislam.

Naamini unayajua maandamano ya Waislam mwaka wa 2012.
Tutoke hapo.

Kama tatizo la kuvamia msikiti usiku wa manane DC na Kamati ya Amani mbona kuna shule za mbovu kupita kiasi hazijavamiwa na wanafunzi kurudishwa makwao?

Angalia ushahidi huo hapo chini:

View attachment 3039350

Upo ushahidi mwingi lakini tuanze na huu.

Nipe jibu kwa nini shule hii haijavamiwa usiku wa manane na DC na Kamati ya Usalama?
Tatizo bajeti
 
Kwanini madrasa iwe ya bweni wanafundishwa nini?
Si bora wapelekwe hata VETA
Mkuu ziko madrasa za bweni zipo za day.

Kama ambavyo zipo shule za bweni za zipo shule za day.

Kuuliz kwa nini madrasa iwe ya bweni ni sawa na kuuliza kws nini shule ziwe za bweni , na jawabu la hapo litaingia kotekote.
 
Hapana hiyo sio sawa mkuu,hao watoto ni wadogo sana bado wanahitaji malezi ya karibu ya wazazi kwsni hata mzazi kumlea mwanawe ni ehemu ya dini.

Hivyo wasidhani kama dini ni kumsomesha mtoto madrasa qurani pekee,bali hsta kukaa naye ukamlea ni sehemu ya Dini..

Nilichokuwa nataka kufikisha ni kwamba watu wasione kwamba madrasaa za bweni za kulala misikitini kwaba ni jambo la ajabu,bali ni utaratibu wa kawaida sana,ila kuwakusanya watoto wadogo katika mazingira hatarishi au mazingira yasiyo rafiki hiyo sio sawa.
Nimekuelewa sana Mkuu
 
Hizi hadithi kawasimulie wajukuu wako ambao umewanyima elimu dunia. Historia iko wazi sana na haihitaji kufundishwa kupitia tamaduni za watu wengine.

Kwa haya maneno yako bado hauko huru kwa sababu tamaduni za kiarabu haziwezi kukupa uhuru. Yaani bila aibu unasema uhuru wa Tanganyika uliletwa na utamaduni wa kiarabu?
Samahani sana, najua wewe ni mtu mzima ila usitumie uzee wako kutafutia watu laana kwa aya unayoyasema kwa sababu kwa mtu mwenye anayejielewa atakuona hamnazo.

Ningekuona wa maana kama ungesema uhuru wa Tanganyika uliletwa na Wandengereko na Wazaramo.
The best,
Wanachama wa mwanzo wa TANU wametoka Rufiji.

Angalia video.


View: https://youtu.be/xJ0XD6zis30?si=Dpiure6A3Q1cMX2A
 
Huyu jamaa kuna anachokitafuta

Kuingia tu anawakataza wazaramo wasitumie pikipiki kubeba mkaa!

Sasa hv kaingilia masuala ya dini ya kiislam.

Yetu macho tu...mbona Jokate aliishi vizuri na wana kisarawe?
Huyo mtu kwanza inaonekana ana roho mbaya ya asili,pili ana chuki ya kidini halafu ana dharau na kujiona anajua kila kitu,kwa roho mbaya yake aliyonayo ndiyo maana mwendazake alimpenda sana lakini huko alipokwenda na upuuzi wake atatulizwa tu maana atapewa mzigo mwingine aangaike nao kwa sasa ana kibiyongo ataongezewa na busha ndiyo atajua hajui.
 
Shekhe wangu Mzee Mohamed Said, kwa hili la Bagamoyo,ungeliacha tu lipite. Si jema kwa afya za watoto.
Kosa la mmoja halimhalalishi muovu
Big Bigstone,
Hao ni watoto wa masikini.
Hapo wako peponi.

Kuna shule mbovu hazijavamiwa.

Angalia nyuma nimeweka picha ya shule moja.

Waislam tumeishi na haya tunajua kinachotafutwa.
 
Makabila yao yanajulikana, ninachopinga nikuwatambulisha kwa dini. Watambue kwa utanganyika wao na kama kuna ulazima basi watambue kwa maeneo waliyotoka na makabila yao na siyo kwa dini.

Unaunajisi uhuru wa Tanganyika kwa kuufungamanisha na tamaduni za waarabu ambao walitumia huo utamaduni kuwapumbaza wazee wetu na kuwachukua na kwenda kuwauza utumwani.

Mtanganyika au Mtanzania huru atasema uhuru uliletwa na watanganyika ila siyo ukristo wala uislamu. Ukiona mtu anasema uhuru tulionao uliletwa na dini fulani, kwa maoni yangu huyo mtu hayuko huru.
The best,
Mimi ni mwanafunzi wa historia na naandika kile ninachotafiti kwa uhalisia wake.

Sina sababu ya kuficha kitu.
Angalia jina la kitabu changu:

1720808814889.jpeg
 
Mzee wangu ambacho sikubaliani nancho ni kusema kwamba uhuru wa Tanganyika ulipiganiwa na dini wakati dini yenyewe ni sehemu ya ukoloni na uvamizi. Hapo ni sawa na kusema uhuru ulipiganiwa na wakoloni ambao walileta hizo tamaduni tunazozitukuza kwa sasa.

Kwa maana hadi sasa hatuko huru kama tunasema uhuru wetu ulipiganiwa na dini. Mzee wangu kama nvitabu vyako vya historia ndo vina habari kama unazozisema hapa basi tunashida kubwa sana kama jamii.

Waacheni watoto wapate elimu dunia na elimu ya dini ambayo inawapasa. Hizo nchi ambako zimetokea hizo dini raia wao wanaongoza kwenda kwenye mataifa yaliyoendelea ili kupata elimu dunia. Inakuwaje sisi ambao tunategemea misaada kutoka kwa walioharibu tamaduni zetu tukazanie kuifundisha jamii yetu tamaduni za watu bila kuwapa maarifa mengine ya dunia.

Hao watoto wakishahitimu hayo mafunzo wanaenda wapi? Yatawasaidia vipi katika kukidhi mahitaji yao ya kidunia na jamii inayowazunguka? Ni nchi ipi imeendelea kwa kufundisha watoto elimu ya dini tu bila elimu dunia?
The best...
Sina tatizo na wewe kutokubaliana na mimi.

Kuna wengi wanokubaliana na mimi kiasi cha kunialika kwenye mikutano na vyuoni kwao kunisikiliza kuhusu historia ya uhuru wa Tanganyika.

Kwao ni ''field of enquiry'' ambayo haikupata kutafitiwa na wasomi wanahistoria wa Tanzania.
 
Big Bigstone,
Hao ni watoto wa masikini.
Hapo wako peponi.

Kuna shule mbovu hazijavamiwa.

Angalia nyuma nimeweka picha ya shule moja.

Waislam tumeishi na haya tunajua kinachotafutwa.
Acha Unafiki unafiki na Fitina Mzee, weka hapa kinachotafutwa...acha kujiliza
 
Mzee, ungetafuta kwanza ufafanuzi wa wa mafundisho wanayopewa humo msikitini kabla hujaamisha mjadala kwenda NECTA. Litakapotokea la kutokea utasema uislam hautufundishi hivyo. Sasa hivi kun jukumu la kujua mafundshilo hayo yanalenga nini na wanagungldishwa nini? Isije kuwa wanafundishwa vitu tofauti kwa mhongo wa elimu ya dini. Najua wewe ni msomi, Sasa wasomi hufanya utafiti kabla ya kuzungumza. Tafuta kwanza mafundisho yao Yana msingi gani.
Mzee huwa anahamisha magoli hadi sio poa. Ni kama wale jamaa wa mihadhara ukiwauliza hiki wanapeleka mada kwingine.
 
Aliyekwambia kuna usiri ni nani? Nani alienda kuuliza kinachoendelea hakujibiwa? Wazazi hawana uwezo wa kupeleka watoto shule binafsi za sekondari mlitaka wafanye nini? Mtoto asijue dini yake kisa mzazi hana uwezo? Acheni chuki za kipumbavu nyie
Ujue sometimes huwa sielewu baadhi yenu ni nini hasa mnataka. Hakuna mwenye chuki na dini ya mwenzake hapa Bongo ni tofauti ndogo tu huwa zinajitokeza mara chache na bado tunashirikiana. Kwenye koo zetu tuna ndugu ambao ni Waislamu na Wakristu. Mimi kuwachukia Waislamu ni sawa na kuwachukia ndugu zangu, rafiki zangu.

Turudi nlipoanzia. Sometimes sijui baadhi yenu huwa mnataka nini. Hapo unashabikia watoto kuachishwa shule wasome dini, baadae tutakukuta kwenye uzi mwingine unalalamika kuna udini serikali inajaza Wakristo nafasi za ajira.

MBONA KAZI.
 
Binafsi naungana na Mkuu wa wilaya. kituo kama hicho kinatakiwa kiwe kimetimiza matakwa yote ya sheria.

Waislam tunatakiwa tuwe Makhalifa na mfano bora kwa jamii, Waislam kama hao wanaoendesha hicho kituo ndiyo wanautukanisha Uislam.
Sasa kama umekubali wewe sijui wengine wanapinga nini. Na sijui kwanini tunapojaribu kushauri au kukosoa mambo fulani tunaambiwa tuna chuki za kidini.
 
Huyo DC toka apelekwe huko ameonesha chuki za waziwazi kwa wenyeji wa huko na ni kama anajiona yeye ndiye anawaweza na atawakomesha,wacha tuone mwisho wake utakuwaje.
Poa poa tumekusikia. Turudi kwenye mada husika, unazungumziaje hilo tukio?
 
Madrassa zinaharibu usalama wa Taifa ila sunday schools aaaah?! Vyuo vya watoto wadogo wanaoenda kufundishwa upadre na utawa aaah haviharibu watoto?
Wanasema makundi mengi ya Ugaidi yameanzishwa na Marekani. Sasa jiulize kwanini ni rahisi kumalaghai kijana wa kiislamu ajivike bomu ajilipue kuliko wa imani nyingine.

Kuna muda sio vibaya kukaa chini kutafakari malezi tunayowapa vijana wetu.
 
Tena aache kabisa kuingilia waislamu, hili suala linamhusu kiongozi wa dini na sio yeye, kama anatafuta kiki kupitia dini ya Mwenyezi Mungu uislamu basi hataweza, mama samia tunakuomba sisi kama waislamu tuondolee huyo magoti huko kisarawe na uweke Muislamu mwenye imani, huruma na atakua msaada mkubwa kwa waislamu.
Mzee watoto ni mali ya Jamhuri. Kwamba uwatendee tu unavyojisikia kwa kisingizio cha dini serikali ikae tu inakuangalia?
 
Wanasema makundi mengi ya Ugaidi yameanzishwa na Marekani. Sasa jiulize kwanini ni rahisi kumalaghai kijana wa kiislamu ajivike bomu ajilipue kuliko wa imani nyingine.

Kuna muda sio vibaya kukaa chini kutafakari malezi tunayowapa vijana wetu.
Sijui lolote kuhusu ugaidi wala sijawahi kuona wala kusikia ugaidi ukifundishwa misikitini. Tanzania hii wapi mtakaa kikundi cha watu 5 kujifunza ugaidi au kuongelea ugaidi bila ya serikali kujua? TIS s ina mtandao mkubwa sana kuliko kawaida. Ugaidi ungekuwa unasomeshwa misikitini na kwenye madrasa basi bila ya shaka serikali ingeshaifungia misikiti yote nchini.

Anachokileta petro magoti ni chuki dhidi ya dini ya kiislam na waumini wake
 
Kwanini madrasa iwe ya bweni wanafundishwa nini?
Si bora wapelekwe hata VETA
Mbona vyuo vya biblia huwa ni vya bweni? Mbona vyuo vya watawa na mapadre huwa ni vya bweni?

Elimu ya kumjua Mungu haihitaji world distractions. Quran ili uihifadhi inahitaji mazingira ya utulivu huku ukijitenga na vishawishi vya kidunia.
 
Back
Top Bottom