Kisarawe: DC Petro Magoti ameutaka Msikiti unaotoa elimu ya dini kwa watoto 96, kuwarudisha walipowatoa sababu ya Mazingira Mabovu ya malazi

Mini...
Wanafunzi wamehojiwa na DC na wamesema wamefeli darasa la saba.
Sikusikia kuwa kuna waliofaulu.

Nifafanulie isiwe mimi sikusikia vizuri.
 
Samia badala ya kukimbizana na Vijana wa CHADEMA awe makini na Mafundisho ya Siasa kali na Ugaidi maana Tanzania yangu iko Vulnerable sana na haya mambo.
 
Katoa muda mpaka Jumamosi. Wasiokuwa na nauli atawapatia.
 
Mzee, ungetafuta kwanza ufafanuzi wa wa mafundisho wanayopewa humo msikitini kabla hujaamisha mjadala kwenda NECTA. Litakapotokea la kutokea utasema uislam hautufundishi hivyo. Sasa hivi kun jukumu la kujua mafundshilo hayo yanalenga nini na wanagungldishwa nini? Isije kuwa wanafundishwa vitu tofauti kwa mhongo wa elimu ya dini. Najua wewe ni msomi, Sasa wasomi hufanya utafiti kabla ya kuzungumza. Tafuta kwanza mafundisho yao Yana msingi gani.
 
Huyo mwinyi wako wengine wanaona hakuwa kiongozi mzuri na ndiye aliyeua uchumi wa Tanzania. Anyways, hilo siyo hoja hapa. Hoja ni kujua wanafundishwa nini basi. Halafu mengine ndiyo yafuate.
 
Yanaweza yasiwe mafundisho ya ugaidi lakini vijana 96 wa kiume kulala pamoja Msikitini mwaka mzima badala ya kulala bwenini huku wakilipiwa ada na wazazi wao si sawa.
 
Watanzania wengi hatuko huru kwenye vichwa vyetu na mara nyingi sana fikra zetu zimefungwa either kwa ushabiki au kwa kuwa na uelewa mdogo.

Mohamed Said hapo juu amegusia jambo fulani nyeti sana ambalo watanzania wote kuna mahala tunapaswa kuwa serious nalo saana.

Shule za Serikali za msingi kawaida kwa kiasi kikubwa ndio zinazoandikiasha wanafunzi wengi sana wa kiislam na wengi sana ndio huhitimu shule hizi elimu ya msingi, kutokana na umasikini kwenye jamii kubwa ya waislamu, vijana hawa wengi huishia darasa la saba na kukosa uelekeo na hujikuta hawana namna zaidi ya kutafuta uelekeo kwenye mafundisho ya dini ambayo kwao hayana gharama zozote.

Tunapotaka kupambana na issue ya za kigaidi kwa kuamini wahusika ni vijana wa kiislam basi hatuna budi pia kuchimba mzizi wa tatizo, kama hawa vijana huachwa wakizagaa baada ya kuhitimu shule za msingi na wengi wao ndio hao waislamu hatuoni kama itakuwa rahisi kutegeka na kuingia kwenye makundi haya?
 
Kufeli shule ya msingi siku hizi ni kutaka kwako mwenyewe. Nina waiswasi kama ninkweli hao wote wamefeli.
 
Kufeli shule ya msingi siku hizi ni kutaka kwako mwenyewe. Nina waiswasi kama ninkweli hao wote wamefeli.

Tatizo hili sio la juzi wala jana,tunaongelea issue ya miaka mingi hata hiyo tunayosema elimu ilikuwa Bora.

Wote tunakubaliana ubora usiofaa wa elimu ya msingi lakini tusisahau shule hizo wanaosoma ni wengi kutoka jamii za kimasikini, kwakiasi kikubwa jamii zakiislamu kuanzia Pwani, tabora, Kigoma, Lindi, Mtwara nk ndio masikini.

Kwanini jamii hizi ni masikini, hii ni topic nyingine japo mengi husemwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…