Kisarawe: DC Petro Magoti ameutaka Msikiti unaotoa elimu ya dini kwa watoto 96, kuwarudisha walipowatoa sababu ya Mazingira Mabovu ya malazi

Kisarawe: DC Petro Magoti ameutaka Msikiti unaotoa elimu ya dini kwa watoto 96, kuwarudisha walipowatoa sababu ya Mazingira Mabovu ya malazi

Hivi Mzee wangu unajua baadhi ya rejea hupoteza uhalisia wake baada ya muda mrefu kupita kutokana na mabadiliko kadhaa ambayo huwa yanatokea?
Kitendo cha kutumia rejea ya 1999 ambayo kiuhalisia kwasasa kuna mabadiliko makubwa kwenye baraza la Taifa la Mitihani na kuongezeka kwa ufaulu kutokana na ongezeko la shule nyingi za Sekondari kunapoteza credibility ya andiko lako.
Kinacholalamikiwa si uchakavu wa majengo wala vijana kukosa fursa ya kwenda Sekondari, bali Mkuu wa Wilaya ana detailed information kuwa kuna vijana wamefaulu na hawajaenda sekondari ila wamesafirishwa na wazazi wao kupelekwa hapo kupata hiyo elimu ya dini.
Huoni kuna kitu cha kufikirisha hapo juu ya kinachoendelea maana ukiachilia mbali shuleni kuwa na somo la dini na huko walipotoka kuna misikiti na madrasa, kwanini wakatishwe masomo walipotoka na kuletwa hapo ilihali hiyo elimu ya dini walikuwa wana uwezo wa kuipata hata huko walipotoka?
Mini...
Wanafunzi wamehojiwa na DC na wamesema wamefeli darasa la saba.
Sikusikia kuwa kuna waliofaulu.

Nifafanulie isiwe mimi sikusikia vizuri.
 
Samia badala ya kukimbizana na Vijana wa CHADEMA awe makini na Mafundisho ya Siasa kali na Ugaidi maana Tanzania yangu iko Vulnerable sana na haya mambo.
 
Huyu nae badala ya kujiuliza nani kawaleta hapo na je wazazi wanajua hilo?
Na kama wanajua wameangalia maisha wanayoishi watoto na je wanafundishwa nini hapo?

Lazima kuangalia chanzo na kama wamevunja sheria wachukuliwe hatua ila kama ni child slavery lijulikane pia wanalimishwa na nani?

Kabla ya kufika maamuzi ya kuwaondoa hapo ingebidi awajuishe wazazi pia kuwa waje wawachukuwe watoto wao

Tatizo letu hatujui kutatua matatizo
Serikali igharamie watoto kwa kuhakikisha wanachukuliwa salama

Je kama wakipelekwa kwingine na kufichwa tena
Au Magoti anataka kuona hakuna watoto hapo kwa masaa 24 bila kujua watapelekwa wapi

Tumieni akili basi
Katoa muda mpaka Jumamosi. Wasiokuwa na nauli atawapatia.
 
Bagamoyo,
Rejea kwenye hiyo video uitazame na usikilize ukiwa makini.
Hakuna mwanafunzi yeyote kutoka nje ya Tanzania.

Rejea usikilize tena hao wanafunzi wengi wameishia darasa la saba na wameletwa hapo na wazee wao waje wasome dini.

Tatizo labda liko hapa.
Nimetumia neno ''labda'' kwa makusudi ili ikiwa lipo tatizo lingine lisemwe.

Ikiwa wewe ni Muislam hutopata tabu unapambiwa watoto wengi wa Kiislam huishia darasa la saba.

Kitwana Kondo alipata kulizungumza hili Bungeni.
Nakuwekea hotuba yake uisome.

(Hotuba ya Mh. Kitwana Kondo (MB) aliyoitoa Bungeni Dodoma, 1999)

Waislam waliofanyiwa mtihani wa kuingia kidato cha kwanza majority yaani wengi walikuwa Waislam na Wengine walikuwa ndiyo wachache.

Waliochaguliwa kuanza kidato cha kwanza wengi walitoka katika wale Wengine na Waislam wakawa wachache.

Waislam kwa kuthamini elimu ndiyo wanawapeleka watoto wao katika shule hizi za ''kimasikini,'' kusoma.

Hatuna ubavu wa kushindana na shule za Wengine ambazo zinapewa ruzuku mabilioni ya kutoka serikalini kupitia Memorandum of Understanding (MUM) katika ya Serikali na Makanisa.

Yapo mengi katika matatizo yanayowakabili Waislam moja wapo ilikuwa NECTA kuhujumu shule za Waislam.

Naamini unayajua maandamano ya Waislam mwaka wa 2012.
Tutoke hapo.

Kama tatizo la kuvamia msikiti usiku wa manane DC na Kamati ya Amani mbona kuna shule za mbovu kupita kiasi hazijavamiwa na wanafunzi kurudishwa makwao?

Angalia ushahidi huo hapo chini:

View attachment 3039350

Upo ushahidi mwingi lakini tuanze na huu.

Nipe jibu kwa nini shule hii haijavamiwa usiku wa manane na DC na Kamati ya Usalama?
Mzee, ungetafuta kwanza ufafanuzi wa wa mafundisho wanayopewa humo msikitini kabla hujaamisha mjadala kwenda NECTA. Litakapotokea la kutokea utasema uislam hautufundishi hivyo. Sasa hivi kun jukumu la kujua mafundshilo hayo yanalenga nini na wanagungldishwa nini? Isije kuwa wanafundishwa vitu tofauti kwa mhongo wa elimu ya dini. Najua wewe ni msomi, Sasa wasomi hufanya utafiti kabla ya kuzungumza. Tafuta kwanza mafundisho yao Yana msingi gani.
 
Hiyo ni sawa na boarding tu,Cha ajabu nini!?..wamekua wakifanya hivyo tangu ikulu ni madrasa,wakilala palepale ocean road,mzee mwinyi alipopelekwa Zanzibar kusoma alipelekwa kwenye shule Kama hizo!..na akaja kuwa rais asiyewatia dhiki watu aliowaongoza Wala kuwazuwia kutoa maoni
Huyo mwinyi wako wengine wanaona hakuwa kiongozi mzuri na ndiye aliyeua uchumi wa Tanzania. Anyways, hilo siyo hoja hapa. Hoja ni kujua wanafundishwa nini basi. Halafu mengine ndiyo yafuate.
 
Babuu,
Unajitia hofu isiyokuwa na sababu.
Waislam wamefanya makubwa katika nchi hii.

Soma historia yao.

Soma historia ya Mtwa Abdallah Mkwawa, Abushiri bin Salim, Hassan Omari Makunganya, Khadija Mkomanile, Abdulrauf Songea Mbano, Kleist Abdallah Sykes na mwanae Abdulwahid Abdallah Kleist, Hamza Mwapachu, Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Suleiman Takadir, Sheikh Haidar Mwinyimvua kwa kuwataja wachache.

Soma historia za watu hawa utawajua Waislam na mafunzo yao na alama walizoacha.

View attachment 3039388
Yanaweza yasiwe mafundisho ya ugaidi lakini vijana 96 wa kiume kulala pamoja Msikitini mwaka mzima badala ya kulala bwenini huku wakilipiwa ada na wazazi wao si sawa.
 
Watanzania wengi hatuko huru kwenye vichwa vyetu na mara nyingi sana fikra zetu zimefungwa either kwa ushabiki au kwa kuwa na uelewa mdogo.

Mohamed Said hapo juu amegusia jambo fulani nyeti sana ambalo watanzania wote kuna mahala tunapaswa kuwa serious nalo saana.

Shule za Serikali za msingi kawaida kwa kiasi kikubwa ndio zinazoandikiasha wanafunzi wengi sana wa kiislam na wengi sana ndio huhitimu shule hizi elimu ya msingi, kutokana na umasikini kwenye jamii kubwa ya waislamu, vijana hawa wengi huishia darasa la saba na kukosa uelekeo na hujikuta hawana namna zaidi ya kutafuta uelekeo kwenye mafundisho ya dini ambayo kwao hayana gharama zozote.

Tunapotaka kupambana na issue ya za kigaidi kwa kuamini wahusika ni vijana wa kiislam basi hatuna budi pia kuchimba mzizi wa tatizo, kama hawa vijana huachwa wakizagaa baada ya kuhitimu shule za msingi na wengi wao ndio hao waislamu hatuoni kama itakuwa rahisi kutegeka na kuingia kwenye makundi haya?
 
Watanzania wengi hatuko huru kwenye vichwa vyetu na mara nyingi sana fikra zetu zimefungwa either kwa ushabiki au kwa kuwa na uelewa mdogo.

Mohamed Said hapo juu amegusia jambo fulani nyeti sana ambalo watanzania wote kuna mahala tunapaswa kuwa serious nalo saana.

Shule za Serikali za msingi kawaida kwa kiasi kikubwa ndio zinazoandikiasha wanafunzi wengi sana wa kiislam na wengi sana ndio huhitimu shule hizi elimu ya msingi, kutokana na umasikini kwenye jamii kubwa ya waislamu, vijana hawa wengi huishia darasa la saba na kukosa uelekeo na hujikuta hawana namna zaidi ya kutafuta uelekeo kwenye mafundisho ya dini ambayo kwao hayana gharama zozote.

Tunapotaka kupambana na issue ya za kigaidi kwa kuamini wahusika ni vijana wa kiislam basi hatuna budi pia kuchimba mzizi wa tatizo, kama hawa vijana huachwa wakizagaa baada ya kuhitimu shule za msingi na wengi wao ndio hao waislamu hatuoni kama itakuwa rahisi kutegeka na kuingia kwenye makundi haya?
Kufeli shule ya msingi siku hizi ni kutaka kwako mwenyewe. Nina waiswasi kama ninkweli hao wote wamefeli.
 
Kufeli shule ya msingi siku hizi ni kutaka kwako mwenyewe. Nina waiswasi kama ninkweli hao wote wamefeli.

Tatizo hili sio la juzi wala jana,tunaongelea issue ya miaka mingi hata hiyo tunayosema elimu ilikuwa Bora.

Wote tunakubaliana ubora usiofaa wa elimu ya msingi lakini tusisahau shule hizo wanaosoma ni wengi kutoka jamii za kimasikini, kwakiasi kikubwa jamii zakiislamu kuanzia Pwani, tabora, Kigoma, Lindi, Mtwara nk ndio masikini.

Kwanini jamii hizi ni masikini, hii ni topic nyingine japo mengi husemwa.
 
Back
Top Bottom