Kuna shida gani madrasa kulea mtoto?! Tuanze hapo .. kuna shida yoyote mimi kumtoa mwanangu akasome dini ?!;Nenda Tanga kuna madrasa za aina hii nyingi tu zimetoa walimu wa dini wakubwa Afrika mashariki na kati .. baadhi yao ni viongozi ndani ya bakwata kwa sasa kama Mufti.. na kwanini aanze kufanya ziara za kushtukiza misikitini?!
Tanga palikua na vyuo rasmi vya kiislam kwa miaka mingi. Havikua na shida.
Shida ilianza pale walipoibuka wanaharakati wanaochanganya dini na siasa na kuwafundisha watoto wadogo bila kujali maisha yao ya baadae katika dunia yenye ushindani mkubwa wa sayansi . Hata kwenye mihadhara mashehe wenye elimu kubwa ya Darasani/Dunia wanaheshimika zaidi kwa uwezo wao wa kufafanua mambo ya dini Kizazi hiki hata huko Uarabuni hapo huko kidini zaidi ya uchumi ndio maana Saudi Arabia hawajitengi na Taifa dhalimu la Marekani kwa sababu ya kuangalia laslahi yao.
Hakuna mtu atamchagua shekhe mkuu asiye na elimu ya kidunia. Huku ni kuwadanganya hao watoto na kuja kuwatumia kujitoa Mhanga.
Hii hata kwa Wakristo ipo umaskini na kukosa Elimu sahihi ya dini ni mtaji mkubwa sana wa watu matapeli wenye tamaa ya mali. Watu wanauza pipi na maji na chumvi makani makanisani .
Tofauti ya Wakrsto na Waislam ni kwamba Waislam wanafanya kwa siri na hawaweki hadharani ili atu wajue nini malengo yale.
Wakrsto wanaweka wazi kwenye tv hata kama ni mazingaumbwe . Mtu ataenda kwa hiyari yake mwenyewe bila kushawishiwa kwa pesa kisirisiri zaidi yeye atauza mali zake na kuwapelekea.
Hatuoni hizo kozi au shule zikitangazwa kuwa zitagunguliwa lini na masomo yake ni yapi na wanafuata mtaala upi na nana anasimamia hiyo mitaala kama ni BAKWATA au ni Wizara ya Elimu au ni nani?
Kwa nini inakua ni siri . Watoto wanatokewa Kenya kuja kusoma Porini kama Maisha Plus . Kuna jambo nyuma yake na halina tija kwa Taifa zaidi ya kakikundi ka watu kujinufaisha kisasa na kiuch
Bagamoyo,
Rejea kwenye hiyo video uitazame na usikilize ukiwa makini.
Hakuna mwanafunzi yeyote kutoka nje ya Tanzania.
Rejea usikilize tena hao wanafunzi wengi wameishia darasa la saba na wameletwa hapo na wazee wao waje wasome dini.
Tatizo labda liko hapa.
Nimetumia neno ''labda'' kwa makusudi ili ikiwa lipo tatizo lingine lisemwe.
Ikiwa wewe ni Muislam hutopata tabu unapambiwa watoto wengi wa Kiislam huishia darasa la saba.
Kitwana Kondo alipata kulizungumza hili Bungeni.
Nakuwekea hotuba yake uisome.
(
Hotuba ya Mh. Kitwana Kondo (MB) aliyoitoa Bungeni Dodoma, 1999)
Waislam waliofanyiwa mtihani wa kuingia kidato cha kwanza majority yaani wengi walikuwa Waislam na Wengine walikuwa ndiyo wachache.
Waliochaguliwa kuanza kidato cha kwanza wengi walitoka katika wale Wengine na Waislam wakawa wachache.
Waislam kwa kuthamini elimu ndiyo wanawapeleka watoto wao katika shule hizi za ''kimasikini,'' kusoma.
Hatuna ubavu wa kushindana na shule za Wengine ambazo zinapewa ruzuku mabilioni ya kutoka serikalini kupitia Memorandum of Understanding (MUM) katika ya Serikali na Makanisa.
Yapo mengi katika matatizo yanayowakabili Waislam moja wapo ilikuwa NECTA kuhujumu shule za Waislam.
Naamini unayajua maandamano ya Waislam mwaka wa 2012.
Tutoke hapo.
Kama tatizo la kuvamia msikiti usiku wa manane DC na Kamati ya Amani mbona kuna shule za mbovu kupita kiasi hazijavamiwa na wanafunzi kurudishwa makwao?
Angalia ushahidi huo hapo chini:
View attachment 3039350
Upo ushahidi mwingi lakini tuanze na huu.
Nipe jibu kwa nini shule hii haijavamiwa usiku wa manane na DC na Kamati ya Usalama?
Hakuna Mtanzania anayebaguliwa na serikali kwa sababu ya dini n hakuna dini 8nyopendelewa na serikali .
Hizo ni propaganda zinazoratibiwa na Mahaidi na fedha nyingi sana zinatolewa kwa sababu ya hizo propaganda .
Magaidi siku zote huwa na watu ndani ya mifumo ya utawala.
Hii nchi imetawaliwa na watu wa dini Mbili kubwa yaani Waislam na Wakatoliki tu., na madaraka ya Rais ni makubwa sana. Memorandum of Understanding haikuwa kwa ajili ya Wkristo peke yao ,huo ni upotoshaji unaotumiwa na mawakala wa ugaidi kufakanisha jamii kwa malengo ya kuleta chuki kwenye jamii. Hakuna Kanisa linalojengwa na seriakali wala Msikiti lakini ni Wazi kuwa kwa upande wa uislam serikali hua inwatafutia mpaka wafdhili kwa ajili ya kujenga misikiti. Na hakuna shida kwa sababu ni maamuzi na maombi yao.
Hakuna Hospitali au shule ya Kanisa au Bakwata inayojengwa na serikali kwa sababu serikali yenyewe haina fedha za kujenga shule zake.
Sasa hiyo MoU ya kuwapendelea wakristo peke yao na kuwatenga Waislam inatoka Wapi?
Fedha Mtriloni yanayoruhusiwa kuingia kusaidia uislam toka uarabuni zingetumiwa kuleta miradi ya maendeleo kwenye taasisi za dini za kiislam leo hii hakuna mtoto wa kitanzania angesoma shule ya Kata mana shule zingejenhwa kila kona ya nchi na mahospitali .
Kuna watu wanajinufaisha sana na masuala ya Ugaidi kupitia dini ya kiislam na wapo mpaka ndani ya serikali ndio maana fedha zinazoingizwa na Waarabu hazifanyi shughuli za maendeleo ya taasisi za dini na mbaya zaidi zinatumika kuhujumiana na kukusanya watoto wa maskini kwenye mazingira magumu na picha zinatumwa kuombamisaada.
Haiingii akilini kuwa waislam hawana uwezo wa kujenga shule bora na mahospitali wakati katika Mabilionea kumi Tanzania hakuna Mkristo hata mmoja wote ni Waislam.
MoU ilikua ni makubaliano kati ya Serikali na Taasisi za dini zinazotoa huduma kwenye jamii kuwa pale penye mradi wa dini sehemu fulani basi serikali isiweke huduma kama hiyo kushindana na taqsisi hiyo iliyoanzisha na waumini wenyewe kwa michango yao au sadaka zao bali serikali iweke utaalamu wake au fedha za kuboresha huduma hiyo. Hii ni kwa dini yoyote hata kama ni Upagani alimradi kuna huduma inatolewa inayopaswa kutolewa na serikali.
Mfano Hospitali ya Kanisa kama KCMC ni hospitali ya rufaa kanda ya Kaskazini kulingana na ukubwa wake. Inahumia watu wa dini zote na inaajiri watu wa dini zote na wanapona au kufa watu wa dini zote bila ubaguzi. Na kama kuna ubaguzi ni mtu binafsi lakini sio sera wala mpango wa kanisa wala serikali. Halikadhalika hospitali ya Ndanda,Nyangao ,Bugando n.k. Maeneo hayo wakakubaliana kuwa serikali isijenge tena Hospitali kwa sababu hizo za kanisa zitakufa kutokana na ukweli kuwa hawana ruzuku ya kutoa huduma bure kama serikali. Wakati huo huduma za afya zilikua ni bure kwenye hospitali za Serikali. Hivyo ili zile za binafsi na taasisi za umma zitolewe bure kwa watu maskini ni vyema serikali ikatoa fedha au kupeleka madaktari wake pale ili wananchi maskini wapate huduma ya afya bure. Huo ukawa msingi wa MoU.
Hata Waislam wakijenga Hospitali eneo fulani bado serikali ingepeleka Dawa na wataalam na ruzuku ili ihudumie wananchi wake. Kwa sasa Bima ya afya imekwenda mbali zaidi mpaka hospitali ya mtu binafsi na Famasi bila kujali ni wa dini gani?
Wakristo wanachanga sana kujenga na kuanzisha Miradi yao wenyewe jambo ambalo waislam hawakatazwi kufanya hivyo.
Ushahidi upo wazi Chuo cha Kiislam cha Morogoro wanafunzi wake wanapata milopo sawa na wa SAUT na UDSM . Hayo ndiyo matunda ya MoU. Lakini ukiwaskiliza mawakala wa Ugaidi wakiwa wanasimilia na kupotosha MoU utafikiri ni lijitu likubwa linalogawa pesa na chakula kwa Wakristo. Sijui aliweka Lowasa akiwa waziri mkuu sijui nini !! Kuwajengea tu watu roho mbaya na chuki bila sababu. Hivi Waziri mkuu anaweza kufanya MoU ambayo haiwezi kuvunjwa na Rais. ?
Yaani Rais alikua Muisam wakati huo JK aone waziri mkuu anafanya lakubaliano ya kugandamiza dini yake halafu na yeye ayakubali halafu baadae atume watu watu waseme kuwa wakrsto wanapendelewa. Hivi unajua kuwa hakuna fedha zinazoweza kutoka na kwenda kokote kama Rais hajakubali?
Lowasa alitumwa tu nenda kawasikilize lakini maamuzi yoyote ya mkataba wa kudumu yanakuwa ni ya Rais.
Kule Moshi kuna Waumini wa dini ya Kikristo juzi wamechanga fedha wakakarabati barabara ya maeneo yao . Seeikali ilitoa wataalam toka Tarura sasa hapo wamependelewa au wameipendelea serikali yao badala ya kuandamana na kuishinikiza ifanye majukumu yake.
Iko hivi : Ubepari ni Unyama ; Kuna watu toka ndani na nje ya nchi ,walioko madarakani na nje ya madaraka wao wanatafuta mafanikio yao kwa namna yoyote hata kama jamii itaangamia. Hawa ndio wanaofadhili vita na ugaidi duniani . Wapo Wakristo kwa upande wa magharibi na wapo Waislam kwa upande wa nchi za Kiarabu. Hawa hawajali mila ,tamaduni na desturi za Mafrika zaidi ya malengo yao na mila zoa. Kwa mfano mimi binafsi sinufaiki na chochote kama Mkrsto kwenye taasisi na miradi ya dini ya Kikristo zaidi ya michango isiyokoma katika miradi hiyo.
Sasa akitokea gaidi mmoja akaanza kuafarakanisha watu na kuwadanganya kuwa wakrato kama dini wananufaika na miradi hiyo ni muongo mkubwa sana. Hiyo miradi ina mpaka ufisadi ndani yake na mikopo mikubwa toka kwenye mabenki. Hakuna Mkrsto anyepunguziwa gharama za matibabu ya figo kwa sababu tu ni mkristo . Hakuna. ! Ukiugua uwe ni mkrsto uwe ni muislam utalipia gharama za matibabu bure.
Juzi kuna Taaisisi Moja ya kiislam ilitoa ngombe zaidi ya elfu tatu kwa ajili ya kuchinja kwenye idi. Ng'ombe elfu 3 ni karibu bil.2. Sasa hapo kupanga ni kuchagua. Kama watu wanapanga zaidi ya peponi kama vile wanaiandaa wao basi waache. Kuna watu wanatoaga maburungutu ya pesa wakati wa sikukuu ya Iddi . Ni maamuzi yao na imani yao kuhusu kesho yao sasa kuwapangia kuwa wajenge hospitali haiwezekani mana anayesimamia taasisi hiyo ana malengo yake.
Kuna wakrsto wanatoa laki tano ili wakamuone Nabii . Na Wanafurika kama nyuki lakini ukiwaambia wajenge shule ya kanisa hawaoni kuwa kuna kubarikiwa na kuleta maendeleo ya jamii nzima leo na kesho. Nabii anachukua pesa anakwenda kununua Hammer na Helkopta binafsi . Kesho anaongiza Waumini kulalamikia MoU inawapendela Wakatoliki .
Ubinafsi ni kitu kibaya sana.
Leo hii ungenipa Urais hospitali na shule zote za dini na serikali zingekua sawa ili kila mtu achague mwenyewe pa kwenda.
Wanasiasa wanachota fedha za umma bila kujali dini zao halafu wanazitumia kuweka machawa wa kueneza propaganda za kuwahawa watu kuwa umaskini wetu umetokana na dini fulani kupendelewa. Badala ya kuwawajibisha Wanasiasa na Watawala kwa kushindwa kuleta maendeleo tunasema kuwa serikali inapendelea dini fulani. Cha ajabu huyo anayeeneza hayo ni Chawa wa serikali hiyo inayopendelea dini moja na eneo analotoka tangu uhuru hakuna diwani wala mbunge wa chama cha upinzani na yeye mwenyewe ni chama kilichotawala tangu uhuru na MoU imewekwa na serikali yake na rais wa Dini yake.
Hqpo ndipo chuki zinapojegwa bila sababu.