Kishindo kingine cha Rais Samia katika SGR; TRC yaingia mkataba na kampuni ya China ununuzi wa behewa 1,430

Kishindo kingine cha Rais Samia katika SGR; TRC yaingia mkataba na kampuni ya China ununuzi wa behewa 1,430

Aya mabehewa wananua tuu sijui wataweka wapi. Hii ni story ya 3 kutoka kandarasi tatu nasikia ya mabehewa
Ni order yanatakiwa yawe tayari ndani ya mwaka mmja.Muwe mnasikiliza sio kukurupuka kwa chuki zenu.

Kadogosa kasema hadi yawe fabricated watakuwa tayari wamemaliza kujenga sgr hadi bandarini na sgr itakuwa tayari imemalizika hadi makutopola kwa hiyo biashara itaweza kuanza kufanyika kwenye sgr mpya.
 
Hiyo ilani, mabehewa ya kisasa yanakuja, tunaenda kuteka soko la Rwanda,Uganda na Burundi pamoja na congo DRC, mzigo inafika mpaka sebuleni kwa mteja kutoka bandarini, yale mambo ya gari za IT kuangushwa na madereva wakati wa safari yanafikia mwisho, kitu ikitoka Japan au ujerumani, kama ilivyo, inafika
Watanzania hamjifunzi? Una uhakika na ubora wa hayo mabehewae? Kwanini usijipe muda kabla ya kusifu na kupongeza?
 
Watanzania hamjifunzi? Una uhakika na ubora wa hayo mabehewae? Kwanini usijipe muda kabla ya kusifu na kupongeza?
Ubora wa hali ya juu, Chadema walinunua magari ya M4C kwa mabilioni, lakini gari zote mtumba na hazitembei, nyie ndio mpewe nchi?
 
Idadi hii ya mabehewa haijawahi kuagizwa na Rais yeyote tangu nchi hii iumbwe, na pengine katika ukanda wa SADC, yameagizwa kwa wakati mmoja na mama huyu jabali la kizanzibari. Anacheza kama Pele
 
Ni order yanatakiwa yawe tayari ndani ya mwaka mmja.Muwe mnasikiliza sio kukurupuka kwa chuki zenu.

Kadogosa kasema hadi yawe fabricated watakuwa tayari wamemaliza kujenga sgr hadi bandarini na sgr itakuwa tayari imemalizika hadi makutopola kwa hiyo biashara itaweza kuanza kufanyika kwenye sgr mpya.

Nimecheka sana
 
Mwambieni main contractor wa SGR awalipe subcontractors pesa zao wanapata tabu sana.... wanakaa hadi miezi 3 bila malipo.
 
Kuna umuhimu wa kuhakikisha tunakua na umeme wa uhakika.

Otherwise haitanoga.
 
Nimecheka sana
Ngoja nikusaidie kucheka 👇

2738144_JamiiForums764709745.jpg

200 (13).gif

2892336_AM1hnY.jpg
 
Sasa hicho kishindo cha Rais Samia kiko wapi hapo? Si suala la kawaida tu hilo! Mnakopa ili kununulia hayo mabehewa, na baadaye Watanzania tutatakiwa kulipa huo mkopo na riba juu kupitia kodi na hizi tozo mlizo tuanzishia?

Kwa nini wataalam tunao wategemea, mnapenda kutanguliza siasa na kujipendekeza kwenye mambo ya msingi? Kiukweli mnaboa sana.
Wanakopa Marekani na mataifa makubwa mengine unashangaa Tanzania kukopa?!.
 
Wanakopa Marekani na mataifa makubwa mengine unashangaa Tanzania kukopa?!.
Mimi sijashangaa kukopa. Ninaongelea hicho 'kishindo cha Rais Samia' je, ni katika nini? Maana kama ni huko kukopa, wala siyo jambo la kushangaza.

By the way, hiyo mikopo yenyewe tutakuja kulipa sisi! Sasa kishindo kiko wapi? Kama siyo muendelezo tu wa kujipendekeza na kumpa mtu sifa asizo stahili?
 
Back
Top Bottom