Huyu ndio amekuja kuharibu kabisa, maana huwa ana itikadi za kutokupenda amani ya nchi yetu, kwa ujumla Chadema tumebugi sana.
Hii amani iliyopo ilikuwepo tangu mkoloni alipokuja Tanzania m
Jambo la kwanza alilofanya mkoloni ni kuwaondoa watu aina ya Mkwawa. Na kuwanyongelea mbili wapigania uhuru wote.
Watawala wote wanana awe mloloni mzungu au mweusi.
Hivi unafikiri wakati Mwingereza anatawala walukua wanavuruga amani ?
Ili mtawala apate raha ya kutawala ni lazima pawe na amani.
Amani inayodumu ni ile inayotokana na Haki.
Kukosekana kwa haki kunawaumiza Watu wasio na kitu. Wenye mali na madaraka siku zote hawana shida sana na haki hasa wale walioko laribu na watawala.
Lakini kukosekana kwa amani anayepata shida zaidi ni mwenye mali nyingi.
Leo hii Somalia hakuna Serikali lakini watu wanaendelea na maisha yao . Waliokimbia nchi ni matajiri na watawala .Maskini kwao kila siku ni kama wapo kwenye vita.
Mtu anajangaika na maisha miaka 60 anashindwa kununua hata pikipiki halafu Waziri anakaa kwenye uwaziri kwa mwaka mmoja kwa Kodi ya wananchi halafu anamiliki maghorofa mashamba ,malori,magari ya kutembelea, watoto wanasoma Nje na bima ya afya ya kimataifa na kila aina ya maisha mazuri na familia yake.
Bila Shaka anayehitaji amani ni Mtawala na familia zao zenye maisha mazuri sana na starehe za kila aina.
Lakini maskini anahitaji Haki ili asionewe na kufungwa kwa kuitwa halifu wakati sio. Asionewe kwa kunyimwa uhuru na haki ya kulalamika na kupinga dhulma.
Amani zipo za aina mbili :
Amani inayopatikana kutokana na ncha ya Upanga na Amani inayotokana na Haki.
Amani ya CCM ni amani inayotokana na ncha ya upanga. Hii ni ya kupiga watu risasi na kuwatisha ili wasifurukute hata kama wanadhulumiwa. Amani hii ni kama zile za nchi za Kidikteta. Hii Amani inawanufaisha watawala zaidi na watoto wao huku watoto wa watawaliwa wakiwa wanaishi kwa hofu na unyonge mkubwa na vilio vikubwa . Amani hii ni amani ya watawala kujiuna wao ndio wenye haki ya kuamua na kufanya chochote. Amani hii inafikia kikomo mana kundi kubwa linakuwa halunufaiki na amani hii hasa kiuchumi na kisiasa Mana ni rahisi watu wakavunjiwa nyumba au wakanyanganywa ardhi bila fidia na wakijaribu kudai fidia wanapigwa mabomu na risasi na kukaa kimya. Wafanyakazi wanalipwa mshahara kiduchu ukilinganisha na watwala halafu wakidai kuwa na sisi ni binadamu kama nyie ,wanapigwa risasi na kukaa kimya pawe amani na utulivu. Wananchi wakijaribu kuwaambia basi kama mmeshindwa kutupa Haki zetu pisheni waje wengine wenye uwezo wa kutusililiza , wanapigwa risasi na mabomu.
Mwisho wale maskini wanachoka na kuona hawana cha kupoteza wanaamua kufanya vurugu ili kila mtu aumie na familia yake ipate adha ili litimie lile neno la wahenga ,"Amani haiji ila kwa ncha ya upanga.
Amani inayotokana na Haki inadumu mana ni amani ya Kimungu. Mungu anajiita ni Mungu wa Haki.
Miaka mitano Siprian Musiba ameruhusiwa kuhamasisha chuki, mauaji,uzushi , matusi, ukabila, uhasama na kila aina ya rafu za kisiasa kwa sababu tu ameona fursa ya kulinda biashara yake kupitia amani ya risasi.
Serikali za zenye kusimamia Katiba na Haki za Kila mtu kamwe hawapigani wenyewe kwa wenyewe mana kila mtu anafurahia amani na kupata haki yake.
Mamuunga mkono Shekhe Ponda. Waathirika zaidi wakubwa wa dhulma tangu ukoloni ni Waislam isipokuwa wale tu wenye maslahi ninafsi ndani ya amani ya risasi.
Kukosekana kwa Haki hakuwezi kumuumiza Huseni mwinyi wala Ridhiwani mana wao wana Kila kitu na wanaweza kuhonga na kununua haki yao.
Wote tuhamasishe amani lakini haki ni lazima itendeke. Kwenye uchaguzi.
CCM oneni aibu. Miaka mitano mnapiga kampeni, mmejenga madaraja,mmejilimbikizia mahela na mali chungu nzima, mmesaidiwa na watu wasiojulikana kwa miaka mitano kuwapiga wapinzani ,kuwateka ,kuwaua na kuwajeruhi lakini bado tena mnataka kuiba kura na kupindua matokeo.
Hapo amani kwa kweli itakua sio amani bali ni ubinafsi ambao jata wajukuu wenu watawashangaa watanzania kuwa ilikua ni amani ama ni woga.