Uchaguzi 2020 Kishindo: Sheikh Ponda atoa neno kwenye mkutano wa Lissu Dodoma, Uwanja walipuka kwa shangwe


Ponda amefanya jambo la maana sana, tena anatakiwa azunguke na Lisu kila mahali akihamasisha waislamu wampe kura Lisu. Tumeona wazi vingozi kadhaa wa dini wakitumika na serikali hii kufunika uchafu wake. Chaguzi zote toka Magufuli kaingia madarakani zimekuwa zinanajisiwa, kisha viongozi wa dini wakihoji wanatishiwa. Acha sasa viongozi wa dini wapande majukwaani kumpigia Lisu debe. Liwalo na liwe, tunataka amani ya haki na sio amani ya kutishwa na vya dola.
 

Hapo hamna kiingereza, bali naona furushi la maneno ya kiingereza yasiyo na maana yoyote.
 
Shekhe Ponda ni Shekhe jasiri sana, CCM walipanga auwawe pale Morogoro kwa mshangao wa wengi Shekhe akazikwepa risasi kininja

Huyu Shekhe ni kaliba ya Lissu kama Lissu kaamua kumchukua Shekhe huyu ili amalizie nae kampeni basi ni jambo zuri sana
Na uchaguzi ukipita watafungwa gereza moja.
 
Nimesoma ukurasa wa Shura ya maimamu kule twitter na kuona shehe Ponda kama Katibu mkuu wa shura ya maimamu akiwataka waislamu wamchague Tundu Lissu eti amebeba ajenda zao.

Ndio nawauliza Bakwata huyu shehe Ponda ameingia kwenye majukwaa ya kampeni kama nani?

Nawatakia Dominica yenye baraka.

Maendeleo hayana vyama!
 
Huyu ndio sheikh sio lisheikh ubwabwa la Dar es salaam , anasimama upande wa haki . Kulwa na Doto na Askofu Emmaus Mwamakula Mungu awabariki sana kwa kukataa hela , Mali ,vitu na vishawishi vyote vya Jiwe .
 
Kwa muda wote wa kampeni nimefuatilia Sana kampeni za CCM kuanzia Magufuli. Samia hadi Majaliwa wote Hawa hawasemi chochote kuhusu mashekh wetu waliopo jela kwa miaka bila kufikishwa mahakamani
Wanajifanya hawajui Hilo..... Sasa mimi na Familia zetu na waislamu wooooooooote wapenda haki kura kwa Lissu
Takbirr
Allah Akbar
 
Waislamu walio wengi ni BAKWATA. PONDA ni siasa kali ya wale mashehe magaidi walioko rumande huwa anawaporomoshea mitusi BAKWATA.

Ukishakuwa na PONDA tu ujue waislamu walio wengi ambao ni BAKWATA kura zao hupati.

Hakuna mtu asiyependwa na waislamu wa BAKWATA kama huyo shehe Ponda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…