Kisichoeleweka kwa wadau kuhusu mbunge wa Morogoro Mjini, Abdulaziz Abood

To be fair kuweka maji ni serikali mkuu kupitia mamlaka zilizopo.
Akiwa kama mbunge alipaswa alivalie kibwebwe wapiga kura wake wapate maji

Yeye anakaa mjini huko maji yako bwerere Ila wanachi kihonda wanasukuma matoroli kutafuta maji mbali huko Tena hayatoki kila siku

Yaani Moro mvua ikinyesha wanachi wanashukuru
 
Huwa anatumia utaratibu gani kulitoa?,akiona msiba anaenda kuwaomba wafiwa atoe basi au wafiwa ndio wanaenda kuomba
Ni utaratibu ambao kafanya uwe mazoea kwa watu wa Morogoro, mwanzo alikuwa na timu ya watu wanafatilia kujua taarifa za misiba na kuleta taarifa kisha anaratibu msaada wa usafiri.

Mambo yakabadilika baada ya wananchi kujengewa mazoea, sasa wao ndiyo wanapigana vikumbo kuomba kusaidiwa usafiri na hata gharama zingine kama chakula kwenye msiba.
 
Hivi huyo Jiwe wenu yeye kazi yake Ni kulalamika tu sio kuchukua hatua yeye sindio mwenyekiti wake wa chama alimchukulia hatua gani? Yeye ndio rais amemchukulia hatua gani ? Hii nchi Ina Safari ndefu Sana ya kwenda kwenye maendeleo kwa uongozi aina hii ya Jiwe na CCM ?
 
Mkoa wa Morogoro kuna watu wamuufanya shamba la bibi. Rais akiwa Kilosa pia alichukizwa kuhusu mashamba. Morogoro inahitajika uongozi imara kuliko mikoa mwingine kuanzia mkuu wa mkoa,wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa Halmashauri, wakuu wa idara zote ndani ya Halmashauri.

Pia mkoa wa Morogoro unaonyesha hauna vipaumbele vya mkoa wako, kama vipio ni nadharia tu. Morogoro kuna kila kitu ila wananchi wake ni maskini sababu hazijulikani.
Huu mkoa ni mgumu jamani...wengine hatuko serikalini lakini ukiuangalia kwa undani sidhani kama kuna mkoa uliobobea vigeugeu, unafiki, fitina, majungu, pashkuna, vizavizabina, utapeli wa ardhi, migogoro ya wakulima na wafugaji kama Morogoro!

Everyday is Saturday............................. 😎
 
Jana Magufuli amemponda sana Mbunge Aziz Abood kwa kuua viwanda lakini kuna kauli haijaeleweka na wadau wa Morogoro wamekuwa kimya kuhusu baadhi ya kauli. Ninalazimika kuandika kuhusu kauli hizo na sababu ya CCM kumsimamisha kama mbunge huku wakijua ameua viwanda

Abood amesimamishwa kwa mara nyingine kama mbunge kwa kuwa tangu zamani amekuwa akitoa magari yake bure kusaidia shughuli za msiba za raia yeyote ndani ya manispaa, Hivyo wadau wanasema Abood anazika watu kwa maana hiyo. Hili jambo pia amesifiwa na Magufuli wakati anazindua Soko la Kingaru Morogoro Mjini.

Morogoro imechukuliwa na Mbunge Abood baada ya Dr. Mzeru kushindwa kufanya kitu, tangu wakati huo viwanda tayari vilikuwa vimeshakufa. Lakini kifupi ni kuwa raia wanamkubali mtu wao kwa sababu hiyo ya kuwazika hivyo hata kwa CCM inakuwa ngumu kumleta mwingine, wakati watu wanamjua Abood

Halafu kama mnavyojua jinsi raia walivyo rahisi kudanganyika, Kuzikwa kuwa wazi zaidi kwao kuliko viwanda ambavyo vingeweza kuwa saidia. Mwaka 2018 Abood aliita watu kuandikisha kama anataka kufufua kiwanda cha MOPROCO raia wakaenda kutuma maomba na kuacha CV ila hadi leo kimya. Anyway sio ishu

So, kuna watu walielewa kuwa kuwazika ni kuwa kuna wafanyakazi walikuwa wanakufa viwandani halafu wanazikwa kwa siri, hapana! Angefanya mambo hayo maana yake ingekuwa ni suala la ajabu serikali ijue halafu ikae kimya, point ni kuwa anawazika raia wote ambao wengine angeweza kuwaajiri kwa kufufua viwanda.

Pia, kwa hili suala limemshushia sana Abood na viongozi wa CCM, Manispaa ya Morogoro so inawezekana akakaa pembeni 2025 ili mwingine achukue, kwa kuwa sidhani kama ataweza kufufua viwanda viwili ndani ya miaka mitano iliyobaki wakati yeye amejiwekeza zaidi kwenye Redio na Usafirishaji.

Kwa vijana wanaotaka kuingia kujaribu bahati yao Morogoro, tutafutane kupeana mikakati kuanzia sasa ili kufikia lengo la kuchukua jimbo na kufanya maajabu, maana Morogoro ina shida nyingi sana. Mikakati inabidi ianze sasa.

Mathematical Equation
Abood ni kielelezo cha uchafu unaolelewa na mfumo kwa mgongo wa siasa za " mwenzetu" za CCM.
CCM kuanzia Mlimba mpaka Lumumba, kuanzia kwa balozi wa nyumba kumi mpaka kwa mwenyekiti Taifa, haina nia njema kwa Tanzania.
 
Mkoa wa Morogoro kuna watu wamuufanya shamba la bibi. Rais akiwa Kilosa pia alichukizwa kuhusu mashamba. Morogoro inahitajika uongozi imara kuliko mikoa mwingine kuanzia mkuu wa mkoa,wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa Halmashauri, wakuu wa idara zote ndani ya Halmashauri.

Pia mkoa wa Morogoro unaonyesha hauna vipaumbele vya mkoa wako, kama vipio ni nadharia tu. Morogoro kuna kila kitu ila wananchi wake ni maskini sababu hazijulikani.
Shida ziko kila sehemu kiutendaji, Bwawa la Mindu walianza kitambo kulizungumzia ili kuongeza upatikanaji wa maji kwa Manispaa lakini hadi sasa imekuwa ni kwenye maandishi tu hakuna vitendo
 
Na asikudanganye mtu hivi Bus moja au mawili makuu kuu yanaweza kuzika wakazi wa manispaa nzima ambao wanakufa daily?? Sijaona hata akihamasisha ujenzi wa vituo vya afya, mfano Kihonda nzima hakuna kituo cha afya, watu inabidi waende mafiga hukooo... Haya ameshindwa hata kushirikisha wananchi kuamua stend mpya ya daladala iwe wapi matokeo yake wameihamishia porini huko Mafiga. Yaani kama unaenda hospitali ya mkoa uende kushukia huko mafiga halafu upande bodaboda au bajaji kuja mjini tena. Ameshindwa kuchukua mawazo ya wananchi ili angalau stendi ihamie pale Fire (wawahamishe wauza mbao wote pale) waende huko Mafiga....
Morogoro ni tabu tu, hakuna kitu kinakera kama mashimo ya barabarani na maji.
Karibia siku ya kutoa ankara ndipo utakuta maji yanatoka angalau kwa utaratibu mzuri lakin baada ya hapo ni shida. Wakuu wa mkoa huu sijui wako kufanya nini, hawafuatilii haya matatizo on daily basis utadhani hawakai Morogoro.
 
..viwanda vyetu viliuwawa na watendaji wabovu wa serikali za ccm.

..abood hakuuwa kiwanda chochote, bali aliuziwa kiwanda kilichokufa.

..serikali ilishindwa kufufua kiwanda ndio maana ikamuuzia abood.

..hii habari ya kusema abood ameuwa watu waliokosa kazi ktk kiwanda ni kuzushiana na kuchafuana.
 
Mkoa wa Morogoro kuna watu wamuufanya shamba la bibi. Rais akiwa Kilosa pia alichukizwa kuhusu mashamba. Morogoro inahitajika uongozi imara kuliko mikoa mwingine kuanzia mkuu wa mkoa,wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa Halmashauri, wakuu wa idara zote ndani ya Halmashauri.

Pia mkoa wa Morogoro unaonyesha hauna vipaumbele vya mkoa wako, kama vipio ni nadharia tu. Morogoro kuna kila kitu ila wananchi wake ni maskini sababu hazijulikani.
Magufuli analalamika kuwa watendaji wake wanamwangusha, ninani anayewateua, anawateua kwa sifa zipi?
Mfano mzuri mkuu wa mkoa huyu,Ole sanare amekwisha shindwa kuongoza mkoa was morogoro, sijui mkuu aliangalia Nini kwake hata akampa mkoa

Mkuu wa wilaya kilosa huyo ndiyo buyu yupu

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
 
..Jpm analalamika na kuomba msaada toka kwenye chama, wakati yeye ndiyo mwenyekiti wa chama.
 
Magufuli analalamika kuwa watendaji wake wanamwangusha, ninani anayewateua, anawateua kwa sifa zipi?
Mfano mzuri mkuu wa mkoa huyu,Ole sanare amekwisha shindwa kuongoza mkoa was morogoro, sijui mkuu aliangalia Nini kwake hata akampa mkoa

Mkuu wa wilaya kilosa huyo ndiyo buyu yupu

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
RC aliangizwa chaka, huu haukupaswa kuwa mkoa wake wa kwanza kuongoza, Mwenyekiti CCM mkoa, bila uzoefu wa utendaji serikalini ni shida.
Morogoro jamani kwa uchonganishi, ulozi, utapeli, uongo, unafiki, ufitini, huyu baba wasipomuondoa ama asipojiondoa mwenyewe, aweza ugua!

Ukisikia ya vijiweni ukichuja utamuonea huruma, siasa za kina Mkude na Kingalu Mwana Banzi zinapelekesha jamani, manicures ukigeuka wanakung'ong'a. Basi tumuombee tu!

Kilosa labda tuhamishe wakazi wa kule wabadilishwe waletwe wanyamwezi na waha na wahehe ndiyo kutabadilika.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Huwa anatumia utaratibu gani kulitoa?,akiona msiba anaenda kuwaomba wafiwa atoe basi au wafiwa ndio wanaenda kuomba
Binafsi Naona Ni Ujuha Tu Wananchi kuwa cloned na mbunge wao kuwasaidia mazishi kwa kutoa magari ya mazishi.

Sio mwana morogoro mie sipajui tofauti na kuja kubarizi mara kwa mara milimani kule nakupita kwa baiskeli kuelekea lake zone na kanda ya kati lakini Je kwanini Abood asiwapatie ambulance na kuboresha zahanati zenu hizo badala ya nyie kukomaa na mauti.

Unajua sie the #commonmwananchi mbumbu sana na wanasiasa wanatitumia kupitia sympathies za matukio ya masikitiko kama misiba nk nk kama njia ya kuendelea kutunyonya but they don't make a progressive leading to a permanent solutions to our well being.
 
Huwa anatumia utaratibu gani kulitoa?,akiona msiba anaenda kuwaomba wafiwa atoe basi au wafiwa ndio wanaenda kuomba
wafiwa huenda kuomba usafiri.
Dereva huelekezwa siku na eneo la tukio.

Huu ni utamaduni ulikuwepo hata kabla ya Hood kufilisika katika basi zake zilizokuwa haziwezi kwend a safari ndefu kusaidia misiba.

Ni uungwana tu, basi ni bure kwa huduma hii. Wafiwa hawalipii dereva wala kuchangia mafuta, ni jambo la utu sana siyo la kubeza.

Matajiri wa mabasi nchi hii ni wengi hawatoi basi zao bure. Hata zile zilizochoka.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Kwa vijana wanaotaka kuingia kujaribu bahati yao Morogoro, tutafutane kupeana mikakati kuanzia sasa ili kufikia lengo la kuchukua jimbo na kufanya maajabu, maana Morogoro ina shida nyingi sana. Mikakati inabidi ianze sasa.
Kutafuta mikakati ya nini, huku tayari Abood kishawapa somo?

Nanyi nendeni "mkazike" wana Morogoro, miaka mitano inatosha kuwarubuni wananchi kwa "rushwa" hiyo mtakayoitumia kama alivyoitumia kwa mafanikio mwalimu wenu.

Ujinga wa waTanzania ni mzigo mzito sana kwao.
 
Jana Magufuli amemponda sana Mbunge Aziz Abood kwa kuua viwanda lakini kuna kauli haijaeleweka na wadau wa Morogoro wamekuwa kimya kuhusu baadhi ya kauli. Ninalazimika kuandika kuhusu kauli hizo na sababu ya CCM kumsimamisha kama mbunge huku wakijua ameua viwanda

Abood amesimamishwa kwa mara nyingine kama mbunge kwa kuwa tangu zamani amekuwa akitoa magari yake bure kusaidia shughuli za msiba za raia yeyote ndani ya manispaa, Hivyo wadau wanasema Abood anazika watu kwa maana hiyo. Hili jambo pia amesifiwa na Magufuli wakati anazindua Soko la Kingaru Morogoro Mjini.

Morogoro imechukuliwa na Mbunge Abood baada ya Dr. Mzeru kushindwa kufanya kitu, tangu wakati huo viwanda tayari vilikuwa vimeshakufa. Lakini kifupi ni kuwa raia wanamkubali mtu wao kwa sababu hiyo ya kuwazika hivyo hata kwa CCM inakuwa ngumu kumleta mwingine, wakati watu wanamjua Abood

Halafu kama mnavyojua jinsi raia walivyo rahisi kudanganyika, Kuzikwa kuwa wazi zaidi kwao kuliko viwanda ambavyo vingeweza kuwa saidia. Mwaka 2018 Abood aliita watu kuandikisha kama anataka kufufua kiwanda cha MOPROCO raia wakaenda kutuma maomba na kuacha CV ila hadi leo kimya. Anyway sio ishu

So, kuna watu walielewa kuwa kuwazika ni kuwa kuna wafanyakazi walikuwa wanakufa viwandani halafu wanazikwa kwa siri, hapana! Angefanya mambo hayo maana yake ingekuwa ni suala la ajabu serikali ijue halafu ikae kimya, point ni kuwa anawazika raia wote ambao wengine angeweza kuwaajiri kwa kufufua viwanda.

Pia, kwa hili suala limemshushia sana Abood na viongozi wa CCM, Manispaa ya Morogoro so inawezekana akakaa pembeni 2025 ili mwingine achukue, kwa kuwa sidhani kama ataweza kufufua viwanda viwili ndani ya miaka mitano iliyobaki wakati yeye amejiwekeza zaidi kwenye Redio na Usafirishaji.

Kwa vijana wanaotaka kuingia kujaribu bahati yao Morogoro, tutafutane kupeana mikakati kuanzia sasa ili kufikia lengo la kuchukua jimbo na kufanya maajabu, maana Morogoro ina shida nyingi sana. Mikakati inabidi ianze sasa.

Mathematical Equation
Kuzika waliokufa imekuwa jambo la maana kuliko kuzuia wasife !
 
Back
Top Bottom