Kisichoeleweka kwa wadau kuhusu mbunge wa Morogoro Mjini, Abdulaziz Abood

Kisichoeleweka kwa wadau kuhusu mbunge wa Morogoro Mjini, Abdulaziz Abood

wafiwa huenda kuomba usafiri.
Dereva huelekezwa siku na eneo la tukio.

Huu ni utamaduni ulikuwepo hata kabla ya Hood kufilisika katika basi zake zilizokuwa haziwezi kwend a safari ndefu kusaidia misiba.

Ni uungwana tu, basi ni bure kwa huduma hii. Wafiwa hawalipii dereva wala kuchangia mafuta, ni jambo la utu sana siyo la kubeza.

Matajiri wa mabasi nchi hii ni wengi hawatoi basi zao bure. Hata zile zilizochoka.

Everyday is Saturday............................... 😎
Hivi hood hazipo siku hizi
 
Binafsi Naona Ni Ujuha Tu Wananchi kuwa cloned na mbunge wao kuwasaidia mazishi kwa kutoa magari ya mazishi.

Sio mwana morogoro mie sipajui tofauti na kuja kubarizi mara kwa mara milimani kule nakupita kwa baiskeli kuelekea lake zone na kanda ya kati lakini Je kwanini Abood asiwapatie ambulance na kuboresha zahanati zenu hizo badala ya nyie kukomaa na mauti.

Unajua sie the #commonmwananchi mbumbu sana na wanasiasa wanatitumia kupitia sympathies za matukio ya masikitiko kama misiba nk nk kama njia ya kuendelea kutunyonya but they don't make a progressive leading to a permanent solutions to our well being.
Waluguru hao wanaona kupewa basi wakazike ndio jambo la maana sana.dunia ina mengi usikute kutoa huko basi kuna tija Kwake kwenye spiritual world
 
Jana Magufuli amemponda sana Mbunge Aziz Abood kwa kuua viwanda lakini kuna kauli haijaeleweka na wadau wa Morogoro wamekuwa kimya kuhusu baadhi ya kauli. Ninalazimika kuandika kuhusu kauli hizo na sababu ya CCM kumsimamisha kama mbunge huku wakijua ameua viwanda

Abood amesimamishwa kwa mara nyingine kama mbunge kwa kuwa tangu zamani amekuwa akitoa magari yake bure kusaidia shughuli za msiba za raia yeyote ndani ya manispaa, Hivyo wadau wanasema Abood anazika watu kwa maana hiyo. Hili jambo pia amesifiwa na Magufuli wakati anazindua Soko la Kingaru Morogoro Mjini.

Morogoro imechukuliwa na Mbunge Abood baada ya Dr. Mzeru kushindwa kufanya kitu, tangu wakati huo viwanda tayari vilikuwa vimeshakufa. Lakini kifupi ni kuwa raia wanamkubali mtu wao kwa sababu hiyo ya kuwazika hivyo hata kwa CCM inakuwa ngumu kumleta mwingine, wakati watu wanamjua Abood

Halafu kama mnavyojua jinsi raia walivyo rahisi kudanganyika, Kuzikwa kuwa wazi zaidi kwao kuliko viwanda ambavyo vingeweza kuwa saidia. Mwaka 2018 Abood aliita watu kuandikisha kama anataka kufufua kiwanda cha MOPROCO raia wakaenda kutuma maomba na kuacha CV ila hadi leo kimya. Anyway sio ishu

So, kuna watu walielewa kuwa kuwazika ni kuwa kuna wafanyakazi walikuwa wanakufa viwandani halafu wanazikwa kwa siri, hapana! Angefanya mambo hayo maana yake ingekuwa ni suala la ajabu serikali ijue halafu ikae kimya, point ni kuwa anawazika raia wote ambao wengine angeweza kuwaajiri kwa kufufua viwanda.

Pia, kwa hili suala limemshushia sana Abood na viongozi wa CCM, Manispaa ya Morogoro so inawezekana akakaa pembeni 2025 ili mwingine achukue, kwa kuwa sidhani kama ataweza kufufua viwanda viwili ndani ya miaka mitano iliyobaki wakati yeye amejiwekeza zaidi kwenye Redio na Usafirishaji.

Kwa vijana wanaotaka kuingia kujaribu bahati yao Morogoro, tutafutane kupeana mikakati kuanzia sasa ili kufikia lengo la kuchukua jimbo na kufanya maajabu, maana Morogoro ina shida nyingi sana. Mikakati inabidi ianze sasa.

Mathematical Equation
Yule mkimbizi wa burundi ana wivu wa kike
 
Mkoa wa Morogoro kuna watu wamuufanya shamba la bibi. Rais akiwa Kilosa pia alichukizwa kuhusu mashamba. Morogoro inahitajika uongozi imara kuliko mikoa mwingine kuanzia mkuu wa mkoa,wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa Halmashauri, wakuu wa idara zote ndani ya Halmashauri.

Pia mkoa wa Morogoro unaonyesha hauna vipaumbele vya mkoa wako, kama vipio ni nadharia tu. Morogoro kuna kila kitu ila wananchi wake ni maskini sababu hazijulikani.
Wananchi wake ni wachapakazi ?
 
Kwani bila kutoa mabasi kwenda kuzika,
Wafu wasingezikwa?
Uchaguzi uliopita wananchi hawakumcagua Abood,Devota Minia ndiye alichaguliwa na wananchi wa Jimbo la Morogoro mjini
Cha ajabu majambaz ya kura kama kawaida yakampa mtu wa Fisiemu
 
Huwa najaribu kufikiria misaada mwingine nakosa hata majibu, hv kutoa mwili hapo bigwa kwenda kuzika hapo kola inamaana mtaa mzma nmekosa hata kuchanga mia tano miatano mkakodi gari. Mnaacha kudai Mambo ambayo yakitekelezwa kunauwezekano wa kuzitatua shida ndogo ndogo kama kupata gari la kusafirisha maiti kwenda kuzika. Mtu huna maji, viwanda vimeuwawa lakini cha maana tumeona misaada ya mazishi ndio ishu. Ila wajumbe na nyie mnawaangusha waluguru.
 
Jana Magufuli amemponda sana Mbunge Aziz Abood kwa kuua viwanda lakini kuna kauli haijaeleweka na wadau wa Morogoro wamekuwa kimya kuhusu baadhi ya kauli. Ninalazimika kuandika kuhusu kauli hizo na sababu ya CCM kumsimamisha kama mbunge huku wakijua ameua viwanda

Abood amesimamishwa kwa mara nyingine kama mbunge kwa kuwa tangu zamani amekuwa akitoa magari yake bure kusaidia shughuli za msiba za raia yeyote ndani ya manispaa, Hivyo wadau wanasema Abood anazika watu kwa maana hiyo. Hili jambo pia amesifiwa na Magufuli wakati anazindua Soko la Kingaru Morogoro Mjini.

Morogoro imechukuliwa na Mbunge Abood baada ya Dr. Mzeru kushindwa kufanya kitu, tangu wakati huo viwanda tayari vilikuwa vimeshakufa. Lakini kifupi ni kuwa raia wanamkubali mtu wao kwa sababu hiyo ya kuwazika hivyo hata kwa CCM inakuwa ngumu kumleta mwingine, wakati watu wanamjua Abood

Halafu kama mnavyojua jinsi raia walivyo rahisi kudanganyika, Kuzikwa kuwa wazi zaidi kwao kuliko viwanda ambavyo vingeweza kuwa saidia. Mwaka 2018 Abood aliita watu kuandikisha kama anataka kufufua kiwanda cha MOPROCO raia wakaenda kutuma maomba na kuacha CV ila hadi leo kimya. Anyway sio ishu

So, kuna watu walielewa kuwa kuwazika ni kuwa kuna wafanyakazi walikuwa wanakufa viwandani halafu wanazikwa kwa siri, hapana! Angefanya mambo hayo maana yake ingekuwa ni suala la ajabu serikali ijue halafu ikae kimya, point ni kuwa anawazika raia wote ambao wengine angeweza kuwaajiri kwa kufufua viwanda.

Pia, kwa hili suala limemshushia sana Abood na viongozi wa CCM, Manispaa ya Morogoro so inawezekana akakaa pembeni 2025 ili mwingine achukue, kwa kuwa sidhani kama ataweza kufufua viwanda viwili ndani ya miaka mitano iliyobaki wakati yeye amejiwekeza zaidi kwenye Redio na Usafirishaji.

Kwa vijana wanaotaka kuingia kujaribu bahati yao Morogoro, tutafutane kupeana mikakati kuanzia sasa ili kufikia lengo la kuchukua jimbo na kufanya maajabu, maana Morogoro ina shida nyingi sana. Mikakati inabidi ianze sasa.

Mathematical Equation
Jiwe amewaambia 2025 jimbo mpeni Rostam Aziz. Si mmezoea kuwapa maponjolo.
 
Hivi hood hazipo siku hizi
Exactly Hood hazipo kampuni ilishafilisika.
Ila Hood alizika misiba miaka mingi kabla Abood kuanza.
Halikuwa jambo la kashfa.
Kwa waliofiwa na wahitaji, hii kitu wanaielewa.
Mabasi yapo available kwa wote profesa na kibarua.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Back
Top Bottom