Hii nimeitoa kwenye archive yangu, nikuletee nyingine..!???
Kwenda kwa:kamati kuu ya
mahusiano chitchat
copy:
Baba V,
copy:
Judgement ,
Mamndenyi
BADILI TABIA ,
yah:kutokua na imani na
mwenyekiti wa mahusiano
chitchat
Baba V .
Rejea kichwa cha habari hapo juu
chahusika,nikiwa pamoja na
mwenzi wangu
madame
B,tunasikitika kutokana na tabia
ama kauli za kidikteta anazozileta
mwenyekiti kwa kuona yupo juu
ya sheria.mojawapo ya baadhi ya
sababu zinazotupa wasiwasi ni
kama zifuatazo,
1.toka tumetangaza tuna
mahusiano,amekuwa mstari wa
mbele kutaka kuvuruga ama
kuuvunja uhusiano wetu na
Madame B ,kwa kuzusha tuhuma
mbalimbali,
2.amekuwa ana nia ya kuvunja
mahusiano na sio kusuluhisha
kwa kuwa anakuja katika
usuluhishi akiwa na jibu na
uamuzi tayari
3.toka ameanza kutufuatilia
tumeshindwa kuelewa ni yeye
ndiye anayeleta malalamiko akidai
ameletewa na mtu anayejiita
Ruttashobolwa,ilhali hatujawahi
kuona huyo mtu akitamka
hadharani
4:mwenzi wangu
Madame B
alishatamka kuwa hamtaki na
wala hampendi mtu anayejiita
Ruttashobolwa lakini mwenyekiti
amejifanya kama hakuona hiyo
statement
5.sababu inayotupa mashaka ni
kuwa barua niliyoituma katika
kamati ya screening ameidharau
na amewadharau wanakamati
hiyo kwa kuwa hakusubiri wakae
kikao na kuamua kujichukulia
hatua mikononi kwa kujiona yupo
juu ya sheria
ninaomba kuupitia kamati hii
mwenyekiti aweke vithibitisho
vifuatavyo,malalamiko ya ndugu
Ruttashobolwa,na taarifa rasmi
aliyoletewa na kamati ya
screening kama anavyojaribu
kuuhadaa umma wa wanachitchat
watuone sisi ni wabaya.
Pia kwa muonekano dhahiri
inaonyesha kuwa mwenyekiti
Baba V anamtaka mwandani
wangu
Madame B ndio maana
ananishinikiza niutangazie umma
kwamba nimemuacha ili
nikishatangaza yeye apate sababu
ya kimaandishi ya kutumia ili
yeye ampate janja yake
tumeishtukia.
Na swali analotakiwa kujibu
baba
V ni ndoa ipi ambayo mwanaume
hajui mke wake analala
wapi,anavaa nini,anakula nini kwa
muda mrefu?kwa sababu anajua
fika ktk umri alionao bado anakaa
kwa wazazi na alimuona
madame
B anakaa katika nyumba yeye
mwenyewe ameona atumie huo
mwanya ili akaishi na mwandani
wangu.
Ndugu wanakamati,mpenzi wangu
Madame B sikumfuata katika
nyumba ya mtu anayejiita
Ruttashobolwa la,bali nilimkuta
katika nyumba moja yeye
mwenyewe na ndipo nilipomwaga
sera zangu naye akazikubali,.
Kutokana na hayo machache
naomba kamati iitishe kikao cha
dharula kuangalia mwenendo
mzima wa mwenyekiti kwa kuwa
kila dalili inaonyesha kuna
mchezo mchafu unafanyika na
ambao wanaujua ni
Baba V na
Ruttashobolwa.HAKI IPO WAPI
KAMA NA MWENYEKITI ANAANZA
KUZENGEA WACHUMBA WETU,JE
KWA WASIO NA UWEZO
WATASALIMIKA?
Asanteni
Chimbuvu &
Madame B