Kisutu: Ajali ya Mwendokasi makutano ya Jamhuri na Morogoro Road

Kisutu: Ajali ya Mwendokasi makutano ya Jamhuri na Morogoro Road

Hii imenikumbusha zamani mambo ya tungi nlikuwa napenda kukaa kwenye viti vinavyowekwa pembezoni mwa Road...mk bar hyo siku nasema niende washroom nyuma huku nasikiaa yalaaaahhh gari imeacha njia
Ikawagusa watu...mwinjumq Road hyo
Nkajirudia kuwa mzee wa kaunta tu

Ova
Nadhani hili liwe somo kwa wafanyabiashara machinga kandokando ya barabara kuu na hasa Dar - Dodoma siku itatokea zitafagia wengi balaa
 
Hii njia mi naona dereva labda alikua anajaribu kukwepa kitu Kama sio mtu basi Gari, haiwezekani uniambie dereva asubuh yote hii kalewa mleta habari hapa umebuni tu.

Ungesema uenda labda bado anawenge la usingizi wa asubuhi hapo sawa atleast kidogo ungeeleweka... alafu we mwenyw ulikua unapita na mwendokasi ukapiga picha ulijuaje kama dereva kalewa!!?
Ni bahati mbaya tu kama bahati mbaya zingine.
Kibaya zaidi haya magari yanakuwa kasi, hata kukwepa bila kuyumba inakuwa tabu.

Kuna siku fire pale boda alijipachika katikati anavuka
Dereva wa mwendokasi alimkwepa ila aliyumba sana.
Hadi gari kutulia tulimshukuru Mungu.
 
Nadhani hili liwe somo kwa wafanyabiashara machinga kandokando ya barabara kuu na hasa Dar - Dodoma siku itatokea zitafagia wengi balaa
Mmh ngumu sana kuelewa

Maana barabarani wendawazim ni wengi sana kila mtu anaendesha ajuavyo
Watu wanajikaliaa tu mpaka ndani ya barabara bila kujali

Ova
 
Mpeni pole dereva wakuu kosa sio lake kuna gari ndogo ilichomeka ghafla ikabd akwepee upande huo mana upande aliokuewpo nasikia kulikua na watoto wadogo...

Wote tunajua ugumu uliopo kugongesha upande wako ila jamaa kajitoa kafara watoto wapone.... Hakua kalewa
Dah [emoji3064]
Mungu awaponye


Kwa kweli magari na boda wasiojitambua kujipachika katika barabara za mwendokasi ni janga sana.

Hizi gari nimekuwa nikipanda mara nyingi na mara kadhaa zimewahi kuyumba
Chanzo cha kuyumba ni hawa boda,magari na watembea kwa miguu kujichomeka kwenye barabara za mwendokasi.
Dereva anakuwa hana namna kulingana na speed.
 
Halafu inaonekana hakuliona hilo basi, maana yule jamaa aliyekaa alipoliona na kuanza kukimbia, yeye akawa analifuata huohuo upande wake. Huenda alikuwa na mawazo ya mbali sana na hivyo kutohisi chochote.
Israeli akitaka rohoo yako,lazima akutie ukiziwi au upofu wa muda kwanza!!

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Halafu utakuta huyu dereva bado ana leseni yake na bado yupo kwenye hiyo kampuni anafanya kazi. Upumbavu kabisa.

Huyo akamatwe, afutiwe leseni akaombe upya na afukuzwe kazi kabisa katika taasisi yoyote ya Serikali asijekuajiriwa. Na akome kabisa.
Unahukumu picha,je,unamaelezo yeyote ya kina kuhusu hiyo ajalj?au tuu team roho mbaya.
 
Imagine bata na kale kakichwa kale chake kalivo kadogo ila anakuzidi akili your head is 30times larger than a bata head ila kwa maoni yako haya am sure humzidi akili
Umetumia uhuru wako wa kutoa maoni; sikulaumu, hii ndio raha ya JF, kila mtu anaweza kuandika anachotaka!
 
Halafu inaonekana hakuliona hilo basi, maana yule jamaa aliyekaa alipoliona na kuanza kukimbia, yeye akawa analifuata huohuo upande wake. Huenda alikuwa na mawazo ya mbali sana na hivyo kutohisi chochote.
Labda masikio mabovu, pale lazima alisikia mlio wa kugongana
 
Kuliona ameliona sema akajiambia akimbie mbele akijua atapishana nalo bahati mbaya akakutana nalo kwenye ukuta. Iwapo kapona atakuwa kapata upenyo kabla gari alijamgandamiza.
Halafu inaonekana hakuliona hilo basi, maana yule jamaa aliyekaa alipoliona na kuanza kukimbia, yeye akawa analifuata huohuo upande wake. Huenda alikuwa na mawazo ya mbali sana na hivyo kutohisi chochote
 
Chanzo cha ajali ni gari ndogo imeingia barabarani ghafla, ndo chanzo

Sijui kwanini wengi hawajaliona hili na video ya camera inaonesha wazi.

Iwapo dereva wa gari ndogo ya Rwanda air angesimama halafu mwendokasi ipite, kila mtu angekuwa salama kwenye hilo tukio.

Kuna muenda kwa miguu hapo sioni watu wakimuongelea, baba wa watu, sijui kama amepona.
Yule kaka aliyekuwa amekaa kwenye kiti alikimbia.
 
Back
Top Bottom