Kisutu: Ajali ya Mwendokasi makutano ya Jamhuri na Morogoro Road

Sijui kwanini wengi hawajaliona hili na video ya camera inaonesha wazi.

Iwapo dereva wa gari ndogo ya Rwanda air angesimama halafu mwendokasi ipite, kila mtu angekuwa salama kwenye hilo tukio.

Kuna muenda kwa miguu hapo sioni watu wakimuongelea, baba wa watu, sijui kama amepona.
Yule kaka aliyekuwa amekaa kwenye kiti alikimbia.
Hapo ndio utakapojua kila mtu na siku yake hapa duniani,kwa harakaharaka unaweza kumcheka yule aliekimbilia ukutani ukasema huyu ningekuwa mimi ningerudi nyuma au ningekimbilia upande wa kulia,wakati huyu naye kama isingekuwa kuuangalia magari yanayokuja saa nyingine saa hizi ingekuwa habari nyingine,hebu jaribu tu kuwaza kama angekuwa kainama anasoma gazeti ingekuwaje...
 
Sema kwenye ajali kila mtu anaangalia maisha yake; yule mwamba alipogundua alitakiwa akimbie huku.anapiga makele ya ajali na hivyo kumshitua yule aliyekuwa analifuata basi.
Hebu jaribu kuhesabu sekunde ilizochukua hiyo ajali kutokea. Ni sekunde chache sana na huyo jamaa hakuwa na namna ya ku escape maana ni kama alishawekwa mtu kati na bus na ukuta.

Ni ngumu sana kufanya split second decision kwenye situation kama hiyo huwa ni bahati tu itokee ila kuhusu maamuzi huwezi kufanya chochote.
 
Halafu inaonekana hakuliona hilo basi, maana yule jamaa aliyekaa alipoliona na kuanza kukimbia, yeye akawa analifuata huohuo upande wake. Huenda alikuwa na mawazo ya mbali sana na hivyo kutohisi chochote.
Hapana, kaliona na kasikia.
Tatizo alikuwa karibu ziadi.

Na reaction yake ya kwanza, ni kukwepa pembeni.
Bahati mbaya pembeni hakukuwa na upenyo.

Huyo mwingine alikuwa mbali ndio maana kapata nafasi ya kukimbia.
 
Sema kwenye ajali kila mtu anaangalia maisha yake; yule mwamba alipogundua alitakiwa akimbie huku.anapiga makele ya ajali na hivyo kumshitua yule aliyekuwa analifuata basi.
Ndugu yangu,kwa hiyo speed ya bus,angekimbiaje?
Ni rahisi sana kusema hivi,ila Mkuu ni haiwezekani.
Speaking from experience yaani huwezi.
 
Halafu inaonekana hakuliona hilo basi, maana yule jamaa aliyekaa alipoliona na kuanza kukimbia, yeye akawa analifuata huohuo upande wake. Huenda alikuwa na mawazo ya mbali sana na hivyo kutohisi chochote.
Hata angeliona bado asingefanya chochote.
Kitendo cha papo kwa papo kukwepa ni ngumu.
 
Hii haina ubishi ndugu dereva alikuwa Kitungi...Pole kwa wahanga.
Tumia macho na akili. Mwendokasi ana right of way kwenye hiyo barabara. Mwenye RAV4 ndio naingia bila kuchukua tahadhari.
Sio mpaka ukasomee u trafik ndio ujue mwenye kosa. The video is self explanatory.
Take your time and look again.
 
Madereva wa bongo wakipita kwenye junction, wanapita kama wanaingia bafuni/chooni tu
Hawasimami,hawaangalii kushoto ama kuliaa ....mtu anakatiza mazima

Ova
 
Hapo ndio utakapojua kila mtu na siku yake hapa duniani,kwa harakaharaka unaweza kumcheka yule aliekimbilia ukutani ukasema huyu ningekuwa mimi ningerudi nyuma au ningekimbilia upande wa kulia,wakati huyu naye kama isingekuwa kuuangalia magari yanayokuja saa nyingine saa hizi ingekuwa habari nyingine,hebu jaribu tu kuwaza kama angekuwa kainama anasoma gazeti ingekuwaje...

Nimebaki nafikiria tuu watu wake wa karibu....
Kuna kitu alikuwa anawaza huku anatembea...
Kuna mipango alikuwa anaipanga aifanye leo jioni au kesho....
Kuna siri aliifahamu ilikuwa aiseme mwisho wa mwezi labda.....
Pengine ametoka kazi za usiku anarudi nyumbani na hiyo ndo njia yake....
Pengine anaelekea shughuli zake za kila siku ametoka kwake alfajiri....
Pengine kuna mtu waligombana jana usiku....

Kwa hali yoyote aiyonayo sasa ya uhai au mfu bado watu wake wa karibu wako kwenye majonzi ama ya msiba au kuuguza....

Ukisikia ajali haina kinga ndo kwa huyu baba aliyekuwa anatembea kwa miguu.
 
Hatari sana

Ova
 
Sema kwenye ajali kila mtu anaangalia maisha yake; yule mwamba alipogundua alitakiwa akimbie huku.anapiga makele ya ajali na hivyo kumshitua yule aliyekuwa analifuata basi.
Hata angemshtua bado isingesaidia chochote.
Kumbuka ni kitendo cha ghafla,hata wa kwenye kiti hakukitarajia

Hata angekimbia kurudi nyuma bado gari lingemfikia tu.
 
Tumia macho na akili. Mwendokasi ana right of way kwenye hiyo barabara. Mwenye RAV4 ndio naingia bila kuchukua tahadhari.
Sio mpaka ukasomee u trafik ndio ujue mwenye kosa. The video is self explanatory.
Take your time and look again.
Hata ukiwa na haki ya njia wajibu wako wa kwanza ni kuepusha ajali.
 
Nimekuwa nikifuatilia madereva wanaosababisha ajali, hasa za usafiri wa uma, nimegundua kuwa wote ni wanaume. Wanawake wapo makini sana wawapo kazini, huwezi kukuta mwanamke anakunywa pombe na kuendesha. Ningependekeza madereva wa usafiri wa uma wawe wanawake
Ni kweli kabisa
Halafu ndio watu ambao tunaogopa sana kuwaachia magari
 
Mwenye taarifa za huyo mpita njia yu hai au amekufa atujuze maana nawa ambia watu hapa kua taarifa ya polisi imeonyesha hakuna Kifo.....

Mm nikiangalia tukio naona kama jamaa Ali escape Kwa kurukia ndani ya jengo la mwendokasi ndani
Kwenye makutano ya Morogoro Rd na Jamhuri St pana kituo cha mwendokasi?
 
Back
Top Bottom