KISUTU, DAR: Maxence Melo akutwa bila hatia shtaka la Kikoa. Apewa 'Conditional Discharge' kwenye shtaka la kutotoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi

KISUTU, DAR: Maxence Melo akutwa bila hatia shtaka la Kikoa. Apewa 'Conditional Discharge' kwenye shtaka la kutotoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi

Mungu awatie nguvu katika kutetea jukwaa huru linasaidia sana watu mbalili kwa Imani tutashinda.
 
The only way out of this case ni kumtanguliza Mungu yeye aujuae ukweli wa mambo yote. Nae atawavusha salama.
 
Kwa kuwa hii sio "official political forum" naombeni uongozi wa jamii forum uwe unafuta thread ambazo haziendani na matakwa ya yule MUTU. hii itaweza kuwaepusha na kesi kesi. yaan in short futeni jukwaa la siasa and the likes mana haiwesekani jukwaa moja likosti Forum nzma asee...
Yaani lifutwe jukwaa la siasa libaki jukwaa la mapenzi?

Una akili au matope?
 
Nikiripoti kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mambo yametuendea vizuri kwa upande wa JF.

Shktaka moja la kikoa cha Dot. Tanzania JF imekutwa haina hatia na shtaka la pili kuhusu CRDB, Maxence Melo amepewa 'Conditional Discharge' kwamba ndani ya mwaka mmoja asifanye kosa litampelekea kwenye mtafaruku kama huu.
 
Hukumu ya kesi namba 458 ya 2016 ya Jamhuri dhidi ya JamiiForums inatarajiwa kusomwa leo Novemba 17, 2020 katika Mahakama ya Kisutu

Katika shauri hili lenye mashtaka mawili, watuhumiwa wanashtakiwa kuendesha mtandao ambao haujasajiliwa kwa kikoa cha DO-TZ.
MUNGU akubariki Sana Mkurugenzi wa JamiiiForums, na ninaamini utashinda Kesi hii leo Katika Jina la Yesu!
 
JF tunaendelea kuuzwa tu. Aluenielewa afafanue tafadhali. Nna familia kubwa inantegemea
 
Mahakama ya hakimu mkaazi kisutu imemwachia huru mkurugenzi wa jamiiforum bwana Max melo kutoka kwa kesi ya 2016 yenye mashitaka mawili ambayo kimsingi yaliamua Uhuru wa habari ndani ya JF.

Kufuatia hukumu hiyo kutoa uhakika wa Uhuru wa habari na kutoa maoni ndani ya mtandao huu wa kizalendo, kuna wana JF ambao hawajapendezwa na hukumu hii?

Je, kuna wanaJF wanatamani JF ifungwe?
 
safi sana kwa maamuzi ya kimahakama yaliyochukuliwa, Jf idumu milele, uhuru wa vyombo vya habari na raia kupata habari uzidi kutamalaki.
 
Hilo kosa namba mbili wamemkuta na hatia lakini wakamuachia huru kwa kumpa hiyo "Conditional discharge"

Yani hapa mahakama inakiri amekosea lakini hawajataka kumuadhibu mpaka atakaporudia tena hilo kosa ndani ya mwaka mmoja.

Huu ni utapeli, wanachofanya hapo ni kumuweka Melo under pressure, kwamba Polisi wakirudi tena JF kutaka taarifa za watumiaji wake, Melo atoe kwa kuiogopa hiyo hukumu, lakini naamini hilo sio kosa kisheria.
 
Back
Top Bottom