KISUTU, DAR: Maxence Melo akutwa bila hatia shtaka la Kikoa. Apewa 'Conditional Discharge' kwenye shtaka la kutotoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi

KISUTU, DAR: Maxence Melo akutwa bila hatia shtaka la Kikoa. Apewa 'Conditional Discharge' kwenye shtaka la kutotoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi

Tunaotumia majina yetu halisi na tusio na wasi hatuna wasi.

Nyie mnaokosoa kosoa serikali na kuikwamisha isitekekeze mipango yake kwa umbea umbea ndio mtaufyata
MTU yeyote asieweza kutenganisha mema na mabaya huyo anaitwa MTU MFU anaeishi, hakuna binadamu asiyekuwa na mapungufu, hao unaodhani huwa hawakosei sio kweli hata wao wanajua huwa wanakosea ila huwa hawapendi kukosolewa, silaha yao huwa ni kiburi na watu wafu wanaoishi kama wewe mnaounga mkono hata yasiyofaa kuungwa mkono, msioweza kukemea yanayopaswa kukemewa. Hata hivyo hongera kwa tabia yako nzuri.
 
Mkuu, umeielewa hukumu lakini?
Kwa kifupi hukumu ya kosa namba mbili ni kosa la jinai kwa JF kukataa kutoa taarifa za member yoyote wa JF kwenda polisi. Kama kuna mtu ameelewa tofauti na mimi naomba ufafanuzi please!
 
Kwahiyo mahakama imesisitiza taarifa za hao member zitole. Kwa muktadha huo je JF itawachinjia baharini kwa kutoa hizo taarifa au haitatoa na itakata rufaa?

Ngoja nianze kufanya marekebisho ya acc yangu kwa kubadili email na kutumia vpn tu.
 
Hapa ndipo wasiwasi unaponiingia
Mwaka mmoja ni mwingi, hii imekuwa kuwasahaulisha kidogo yale yanayopigiwa kelele, waimba mapambio wapo kazini, kutumia mwanya waliotengenezewa kuhujumu. Uhuru huu naweza sena pekee ulio bakia Tumuombe Mungu awape upofu, hata wasikumbuke nia yao ovu.
 
Kwahiyo mahakama imesisitiza taarifa za hao member zitole. Kwa muktadha huo je Jf itawachinjia baharini kwa kutoa hizo taarifa au haitatoa na itakata rufaa?

Ngoja nianze kufanya marekebisho ya acc yangu kwa kubadili email na kutumia VPN tu
Hata mimi hicho ndicho nilichoelewa mkuu!
 
JamiiForums hawawezi kuizima kwa Style hiyo washinde
 
Tunaotumia majina yetu halisi na tusio na wasi hatuna wasi.

Nyie mnaokosoa kosoa serikali na kuikwamisha isitekekeze mipango yake kwa umbea umbea ndio mtaufyata
KUIKOSOA serikali ni KUREKEBISHA serikali ili itekeleze mipango yake vizuri..

Tumeona juzi tu serikali imeamua KUREKEBISHA na KUVIBORESHA vitambulisho vya machinga baada ya kukosolewa

Mawazo ya wengi ni mtaji Kwa Taifa..

Tafakari

free Mazrui and all Political Prisoners
 
Tusidanganyane kwa kweli kufutwa kwa chombo hiki si rahisi kwani hata Serikali inapata vyanzo vingi vya habari hapa. Wote wanachungulia hapa na ID zetu zile pendwa

Hata Pascal Mayalla ni shahidi.
 
Back
Top Bottom