Muda mchache uliopita Mwenyekiti wa Chadema Mbowe alikuwa mahakamani Kisutu.
UPDATE:
TAARIFA KWA UMMA JUU YA AFYA YA MWENYEKITI WA TAIFA MHE.FREEMAN MBOWE .
Tumepokea taarifa za hivi punde kuwa Mwenyekiti wa Chama Taifa Mhe.Freeman Mbowe amefikishwa katika Mahakama ya Kisutu na amesomewa Mashitaka ya Ugaidi.
Hii ni pamoja na ukweli kuwa Familia na Mawakili wake walijulishwa kuwa wanampeleka hospitali na hivyo alifikishwa Mahakamani kimyakimya bila kuwa na uwakilishi wa wanasheria wala familia yake.
Taarifa zaidi zitakuja hapo baadaye ili kujua aina halisi ya mashitaka ambayo amefunguliwa (charge sheet) baada ya kuiona hati ya mashitaka .
Imetolewa Leo tarehe 26 Julai,2021
John Mrema
Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje