Kisutu, Dar: Mbowe afikishwa mahakamani kwa Ugaidi. Akosa dhamana na kupelekwa rumande. Kesi kuendelea Agosti 5, 2021

Kisutu, Dar: Mbowe afikishwa mahakamani kwa Ugaidi. Akosa dhamana na kupelekwa rumande. Kesi kuendelea Agosti 5, 2021

watuhumiwa wakikaa muda mrefu polisi sheria imeshaweka remedy zake, nenda kasome sheria au ajiri mwanasheria atakufafanuliwa. there are remedies in every thing that you people complain about.
Sawa hizo remedies zipo je ni wangapi wanajua kuhusu hizi remedies na je zinatekelezwa? Maana Tanzania mabingwa kuandika vitu vizuri kwenye makaratasi lakini sio utekelezaji
 
Nafikiri Rais alikuwa tayari kuzingumza na upinzani mpaka pale mlipotangaza Mpango wa kumnyoa mbele ya waandishi wa habari.

Namaanisha huu upande wa pili wa SSH,umefunuliwa na upinzani wenyewe.
Hapa hawataki kukiri kuwa walikosea! Chadema nao ni wale wale tu kama CCM.
 
Tatizo na nyinyi Chadema mlianza shobo mapema sana kwa Samia mlikuwa nyinyi ndo mmepewa kazi ya kusifu na kuabudu ghafla mwenyekiti wenu kajitokeza alipojificha na kutaka kukutana na Rais lile tu nikajua bhasi siku zote mwanamke ukimshobokea sana anakudharau hata kama alikuwa na interest na ww 😂😂

Jpm pamoja na mabaya yake wanayosema Chadema hakuwahi kumpa kesi ya Ugaidi mwenyekiti wa wachaga na Chadema Mr Mbowe . Sasa Serikali ya Muhula wa 6 mliyokuwa mnaipamba na kuimba nyimbo za kusifu na kuabudu kwa roho mbaya zenu juu ya JPM, inamweka ndani Mwenyekiti wenu na Kesi ya Ugaidi


Mbowe yupo kundi Moja na Osama na Chadema ni Chama cha kigaidi kikiungana na Abu Sayyaf Group (ASG),Afghan Taliban,Al-Nusrah Front, Al-Shabaab,Ansar al-Sharia, Ansar Bayt al-Maqdis (ABM), Al-Qa'ida Core (AQ)
Mashehe walipatikana na hukumu hizi kesi ushahidi ndiyo muhimu
 
Huyu baba ana matusi jamani wasukuma sijui tulimuudhi nn, yaani anaenda usukumani halafu anatukana hao wasukuma waliompokea na kuhudhuria shughuli yake, haya katoka hapo kaenda gereza la shy Nako wamefika ni kutukana tu kila mtu, yaani kwa kweli mi hata sishangai kwa kesi zake za ugaidi.
Ng'wanokoz....
 
Mbona mnashangaa sana Mbowe kushatakiwa? Hakuna mtu mwenye crime history ndefu kama Mbowe ila mfumo ulikuwa unammezea tu. Miaka ya 1985- 1990s alikuwa ni drug trafficker. Kuanzia 1990 amefanya biashara kwenye nyumba ya NHC kwa kutapeli mpaka 2016 Magufuli alipovunja Bilcanas.
Hii ni kweli?

Sina chama, nataka kujua ni kweli?
 
Wanaosambaza taarifa kwamba Mbowe amefikishwa mahakamanj kwa Ugaidi nadhani wanapotosha ili kuvifanya vyombo vya dola vitoke adharani kueleza kwanini afikishwi Mahakamani. Leo kwenye vyombo vya habari tumeona dreva tax aliyepewa kesi ya MO ameachiwa, vyombo vilivyoripoti habari hii vilikuwa Kisutu, je Mbowe amepitushwa Mlango gani waandishi wasimwone? Gaid kwa namna tulivyozoea kuona walivyokuwa wanalindwa mashekkhe wa uhamsho si escort ambayo unaweza ukaificha.

Lakini pia hii nikuichafua mahakama, maana hakuna makosa yanayoonekana ya mtuhumiwa. Means mahakama inarudi kulekule ambako ilijaza watu mahabusu wasio na kosa kwa kisingizio imefungwa mikono.

Tatu nikumchafua Mhe. Rais, kwamba yeye anahusika na hiki kilichotokea. Mwenyekiti wa chama Cha siasa kuwekwa ndani kwa Ugaidi ambao Watanzania milioni 60 awauoni na ambao hakuna ufafanuzi nikumuhusisha moja kwa moja Mhe. Rais kwenye Jambo ambalo hata wananchi wasipoandamana Wala kuingia mtaani, hakuna namna ambavyo utaweza kuwaaminisha watu wa ndani na wageni kwamba ni sehemu salama.

Hii itatoa picha kwamba ipo siku dangote atakamatwa na kuitwa Gaidi Kisha Mahakamani to gerezani, wamiliki wa viwanda na biashara watakamatwa na kuitwa magaidi Kama ambavyo dola ilitumia neno uhujumu uchumi kuwafilisi watu na kuwanyang'anya Mali zao.

Sidhani Kama Rais aliapa kuifanya hii nchi isiwe sehemu sahihi pakuwekeza na kuhifadhi fedha iwe sehemu sahihi yakuchuma na kupeleka kwenye mabenki nje.

Katika Hali ya kawaida kabisa tutakuwa tunashika namba moja Duniani kwa kukiuka haki za binadamu na kuwa na Taifa ambalo hakuna sheria.

Japo sikatai kwamba kwa akili za watu wasiofikiri sawa sawaswa na kwa akili za watu ambao wameakikisha wanarithishana madaraka Kama wafalme sioni Kama haiwezekani kuwaweka watu ndani wanavyojisikia kwa sababu wamejimilikisha nchi.

Wanaopaswa kushauri haya sidhani Kama wataweza kwa sababu JK mke na mtoto wapo bungeni si kwa sababu Wana sifa Bali kwa sababu wamepewa nafasi na utawala uliopo, ataanzaje kuhoji? Mzee Mwinyi naye akihoji haya mwanaye ni muhusika mkuu. Mzee Lowasa mwanaye yupo Dodoma, Warioba mwanaye yupo kwenye mfumo so sidhani kama yupo wakuyapinga haya yasitikee Tanzania.

Ushauri tu ni kwamba, kwa Hali ya Dunia ya Sasa upo uwezekano tutashindwa hata kulipa mishahara au tukauza nchi kwa wachina kulipa mabilioni na matrilioni tunayokopa kufanya mambo ambayo Taifa lingekuwa la haki yangefanywa na wananchi wenyewe.

Mbowe naamini yupo mahabusu osterbay na hana Ugaidi ndani yake.
 
Mimi na Magufuli ni kitu kimoja, hamkuelewa msiba umeisha sasa ni kazi kazi Bisiness as usually Tanzania hoyee, Kazi iendelee.
 
maneno kama haya ndio hata mtuhumiwa DJ gaidi alikuwa nayo, sasahivi yupo segerea amepewa ndoo.
EeenHee Bhwanah,

Mbona na huyo unamchelewesha kumfikisha Segerea mkuu?

Hapana, usinigeukie, ninakukumbusha tu wewe wajibu wako unaouhimiza hapo.
 
Baada ya ccm kutuletea rais msukuma wa kwanza dikteta sasa wameamua kutuletea rais wa kwanza mwanamke dikteta

Kweli katiba mpya imewashika penyewe wameamua kufuata nyayo za hayati kuwabatiza wadanganyika ubatizo wa moto
 
Nitasema na mbiguni nitasema mda wangu ukifika ,hakuna UGAIDI KWA MBOWE,

KAMA MBOWE NI GAIDI BASI NA FAMILIA MWL NYERERE NI FAMILY YA UGAIDI ,naishia hapo, wengine mpo hapo hata hamjui taifa kimetokea wapi, tz history back ground hamjui nawambia, umejikuta tu upo police,Tiss, magereza,uamiaji, JWTZ, Mgambo, n.k someni history ya taifa Hili mtajua tumetoka wapi na mtaondoka gizani, na kuongeza kitu flani vichwani kwenu
Soon wataaibika Katiba mpyaa HAIEPUKIKI
 
Hii ni kweli?

Sina chama, nataka kujua ni kweli?
Magufuli alikua anazifanyia kazi sana taarifa anazopewa ndio maana maamuzi yake yalikua tofauti na mitazamo ya wengi.
 
nenda mahakamani kamtolee ushahidi ashinde kesi, acha kutapatapa hapa, haimsaidii chochote kwanza hata hajakusikia.
Mahakama yangu ya kwanza ni ya Mungu, utaniambia nini mfano mtu kama wewe, mahakama za kwangu sio za kidunia ila next level Mara elfu moja mahakama zenu za kidunia ambapo mwajiona mmefika

Sikia binafsi sio level YAKO japo WENDA unayo mamlaka ya kidunia, take care, nakuonya Mara mmoja, na zingatia sio ombi ila ni lazima asema bwana
 
Sawa hizo remedies zipo je ni wangapi wanajua kuhusu hizi remedies na je zinatekelezwa? Maana Tanzania mabingwa kuandika vitu vizuri kwenye makaratasi lakini sio utekelezaji
nenda kwa mwanasheria yeyote uliza "remedies za judicial review" ie. habeas corpus, quo warranto, prohibito, mandamus, procedendo, and certiorari.
 
Nitasema na mbiguni nitasema mda wangu ukifika ,hakuna UGAIDI KWA MBOWE,

KAMA MBOWE NI GAIDI BASI NA FAMILIA MWL NYERERE NI FAMILY YA UGAIDI ,naishia hapo, wengine mpo hapo hata hamjui taifa kimetokea wapi, tz history back ground hamjui nawambia, umejikuta tu upo police,Tiss, magereza,uamiaji, JWTZ, Mgambo, n.k someni history ya taifa Hili mtajua tumetoka wapi na mtaondoka gizani, na kuongeza kitu flani vichwani kwenu
kwa kusema hivyo unafikiri umemwokoa kwa chochote? bado yupo segerea usiku huu.
 
Mi nadhani kuna tatizo kwenye ofisi na mfumo mzima wa mashtaka kwa serikali yetu.kwanza Mara nyingi watuhumiwa wanakaa polisi zaidi ya muda wa kisheria kufikishwa mahakamani ie unategemea na mood ya polisi, pili wanakamata watuhumiwa kabla ya upelelezi haujakamilika matokeo yake wakifika mahakamani unakuta mtuhumiwa hana cha kujibu ie case ya uamsho.tatu taratibu na sheria hazifuatwi wakati wa ukamataji wa watuhumiwa Mara nyingi utavamiwa, kupigwa au hata kusachiwa bila kuwepo mashahidi,mwanasheria nk
Kiujumla Tanzania ndio nchi ambayo polisi anaweza kujichukulia sheria mkononi,hawafuati weledi na taaluma ya kipolisi katika kutekeleza majukumu yao.

Kwa kesi ya Mbowe hata kama anayo kesi ya kujibu ila kwa jicho la kawaida kabisa tunaona kuna ukiukwaji kubwa wa sheria kuanzia kukamatwa kwake,kushikiliwa na kufikishwa mahakamani. Sasa haya mambo anafanyiwa Mbowe ambaye ni mtu yuko kwenye spotlight, je sisi wananchi wa kawaida inakuwaje tukiacha itikadi za kisiasa.
Ukamatwaji wa Magaidi ndiyo upo hivyo, na ashukuru nchi yetu imestaarabika, nchi nyingine order ingekuwa ni "Shoot to kill", no mambo ya mahakama.
 
Muda mchache uliopita Mwenyekiti wa Chadema Mbowe alikuwa mahakamani Kisutu.

UPDATE:


TAARIFA KWA UMMA JUU YA AFYA YA MWENYEKITI WA TAIFA MHE.FREEMAN MBOWE .

Tumepokea taarifa za hivi punde kuwa Mwenyekiti wa Chama Taifa Mhe.Freeman Mbowe amefikishwa katika Mahakama ya Kisutu na amesomewa Mashitaka ya Ugaidi.

Hii ni pamoja na ukweli kuwa Familia na Mawakili wake walijulishwa kuwa wanampeleka hospitali na hivyo alifikishwa Mahakamani kimyakimya bila kuwa na uwakilishi wa wanasheria wala familia yake.

Taarifa zaidi zitakuja hapo baadaye ili kujua aina halisi ya mashitaka ambayo amefunguliwa (charge sheet) baada ya kuiona hati ya mashitaka .

Imetolewa Leo tarehe 26 Julai,2021

John Mrema
Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje
Nadhani wanasubili ndevu ziote na mvi zionekane tena kama wakati ule. Si unajua ukikosa saloon kwa wiki mbili?
 
Soon wataaibika Katiba mpyaa HAIEPUKIKI
Upo sawa mkuu KATIBA INAKUJA NA HAKUNA WA KUZUIA ningesema Mara nyingi wi confidence, maana najua who iam in connection with my Lord, kakuna wakuzuia ,wanajidanganya tu , tz ni nchi ya Mungu, na kawaumba watz KWA mfano wake, twende tu
 
Back
Top Bottom