Rusumo one
JF-Expert Member
- Oct 4, 2018
- 3,458
- 4,283
Ngonjera hizi si nyakati zake
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu usiandike ili uonekana ya kuwa na ww umeandika rudi nyuma tangia awamu ya kwanza hadi ya nne na unitajie mahabusu m1 tu aliyerusiwa kutoka magereza kwenda kuhudhuria msiba wa mama, baba, mke au mtoto wake.
Au tangia tupate uhuru hakuna mahabusu aliyefiwa na wazazi wake? Hata kwa nchi tunazozisifia kuwa zina demokrasi hakuna mahabusu ambae kesi yake ni unbaillable ambae amewahi kutolewa magereza na kwenda kuhudhuria mazishi.
Sent using Jamii Forums mobile app
Niwatofautishe na nini? Ili uweze kutofautisha ni lazima uwe na vitu zaidi ya ki1Unawezatofautisha vipi wahalifu,maana wahalifu ni zao la jamii
Unawezavipi jitofautisha kati ya civilized and educated society and uncivilized and uneducated society kama unamiliki sheria zilizopitwa na wakati.Hizo sheria zinazobadlika unazisema za nyumban kwenu au?
Kama jambo hulielewi bora ukae kimya
Sent using Jamii Forums mobile app
Erick Kabendera mwandishi wa Kujitegemea wa Habari za uchunguzi inaendelea leo Mahakama ya Kisutu.
Kabendera anashtakiwa kwa Makosa matatu ikiwemo kukwepa Kodi, Utakatishaji Fedha na kujihusisha na genge la uhalifu.
UPDATES
MAHAKAMA YAOMBWA KABENDERA KUMUAGA MAMAKE
HOJA SITA ZA UPANDE WA UTETEZI KWANINI KABENDERA APEWE RUHUSA KUSHIRIKI MAZIKO YA MAMA YAKE
Jopo la mawakili wa Mwandishi wa habari wa kujitegemea Erick Kabendera, wakiongozwa na Wakili Jebra Kambole wamewasilisha hoja sita mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu Janet Mtega kwa mshitakiwa kupatiwa ruhusa chini ya ulinzi ili aweze kushiriki Katika maziko au kutoa heshima za mwisho kwa mama yake aliyefariki hivi karibuni.
1. Kutoa heshima za mwisho ni haki ya msingi ya binadamu. Wakili ameeleza kuwa Kabendera ana haki ya kuwa na kuheshimu familia pamoja na haki ya faragha hivyo kuna umuhimu kwa Kabendera kushiriki Katika kutoa heshima za mwisho kwa mama yake.
2. Erick Kabendera anatakiwa adhaniwe kuwa hajatenda kosa mpaka pale mahakama itakapothibitisha kuwa ametenda kosa na kumzuia kushiriki mazishi itakuwa ni adhabu ya Kinyama kwa Kabendera.
3. Tangu Mshitakiwa amekamatwa hajaonesha nia ya kutoroka au kutaka kufanya vurugu hivyo hakuna uwezekano wa mtuhumiwa kutoroka Kama atapatiwa ruhusa
4. Mashitaka anayokabiliwa nayo mshitakiwa hayahusiani na uvunjifu wa amani hivyo Mahakama itilie maanani ombi Hilo
5. Kama Mahakama ilitoa amri aende mahabusu hivyo Mahakama Ina uwezo wa kuamua ombi hilo kwani kama mshitakiwa pia aliweza kupelekwa mahakamani haitashindikana kumpeleka kanisani kumuaga mama yake.
6. Ruhusa ya Kabendera kuhudhuria mazishi Jamhuri haiwezi kuathirika
MAJIBU YA UPANDE WA SERIKALI
Jamhuri yampa pole nyingi kwa msiba wa mama yake mzazi, Bibi Verdiana Mjwahuzi. Pia Jamhuri imepinga hoja za utetezi wakidai Mahakama haina Mamlaka wala DPP hajaipa mamlaka ya kutoa maamuzi hayo.
Wakili wa Serikali, Simon Wankyo amesema...
"Hata sisi tuna masikitiko makubwa na tunampa pole nyingi Kabendera kwa kufiwa na mama yake mzazi, lakini mahakama isifungwe mikono kwa maombi yaliyowasilishwa ya kutaka mshtakiwa kushiriki Msiba.”
Mheshimiwa Hakimu katika macho ya kisheria mahakama yako haina mamlaka ya kusikiliza maombi hayo kwa sababu kesi hii ni ya uhujumu uchumi, licha ya kuwa hata sisi tuna masikitiko makubwa lakini tunaiomba Mahakama yako isifungwe mikono.”
Pia soma
TANZIA - Mama mzazi wa Mwandishi Erick Kabendera, Verdiana Mjwahuzi amefariki dunia leo Jumanne Desemba 31, 2019
Mama mzazi wa mwandishi Erick Kabendera, Verdiana Mjwahuzi amefariki dunia leo Jumanne Desemba 31, 2019. Amefariki akiwa Hospitali ya Amana alikokuwa akip Soma pia: - Mama Mzazi wa Erick Kabendera amuomba Rais Magufuli kumsamehe mwanae - Mwanahabari Erick Kabendera...www.jamiiforums.com
Hivi kwani waliopo na kesi zisozo na dhamana huwa wanaruhusiwa kwanda kuzika ?
He's all alone! Wanamchora tuuh...wako wapi wale waliomtumia na kumvimbisha kichwa?
Bahati mbaya hao wanaoamini hivyo siyo mahakimu na wanaongonzwa na emotions...wanaoshinikiza KABENDERA apewe ruhusa kumzika mama yake wanaamini KESI yake ni ya KUBAMBIKIWA, ni kesi ya UONGO.
Kupel
Kitu gani kinasababisha upelelezi kutokukamilika?.
Kama kweli waliona makosa kwake,kwa Nini wasioneshe ushahidi usio na Shaka ili kijana ahukumiwe?.
Kuna Nini kinachowazungusha upelelezi haujakamilika?.
Au walimkamata kimakosa?.
Mkuu wa majaji,Roho wa Mungu akuongoze usimamie hili,mtu akikamatwa tia miezi miwili au mitatu, upelelezi Kama Bado tupilia mbali.
Kwaiyo atolewe mahabusu akafanye mambo ya jamii? Je ilishawahi kutokea nchini au Kabendera ni special?Umeshasema mshtakiwa kwa maana bado hajakutwa na hatia.
Vipi ikitokea akaachiwa huru kwa kukosekana ushahidi wa kumtia hatiani.
Usiwe unajitoa ufaham tu mwenzio amefiwa na bi mkubwa wake!
Sent using Jamii Forums mobile app
Bahati mbaya hao wanaoamini hivyo siyo mahakimu na wanaongonzwa na emotions.
Once a fool always a fool, may the pit of hell open up and shallow you and your jiweKwani alizaliwa peke yake? Lini mshitakiwa aliwahi ruhusiwa kwenda kwenye mazishi? Au hii iwe special kwa huyu, mwandishi habari? Wakulima je? Wafugaji je?
Tusiishie kusikitika, tuepuke kujiingiza kwenye mambo ya kujitakia. Kulikuwa na kila njia ya kuachana na hayo lakini naona alijivunia ushujaa.
Mungu akubariki na akupe maisha marefu, umeongea ukweli mtupu, shukurani kabisa mkuuMkuu tetea uovu maana uko mezani kwa mfalme na sahani yako imejaa mlo wa kutosha, na namna nzuri ya huo mlo ili uweze kushuka utakavyo ni pamoja na kujenga hoja ya kuutetea huo uovu. Hata akina Mwigulu, Nape, Januari nk walikuwa wanatetea uovu enzi za JK wakiwa mezani kwenye mlo kama ww. Ila hiyo warmup inayowakuta hivi sasa akili imewarudia.