Kisutu: Kesi ya Erick Kabendera yaendelea. Jamhuri yaweka kisiki Erick kushiriki msiba wa mama yake mzazi

Kisutu: Kesi ya Erick Kabendera yaendelea. Jamhuri yaweka kisiki Erick kushiriki msiba wa mama yake mzazi

haki za msingi ndio zipi zinazolindwa ukiwa jela?

hata kuzaa ni haki ya msingi

Kabendera aachiwe akazae kisha arudi?

Huyu mwandishi kafanyiwa dhulma, na hayuko peke yake, lakini kuachiwa kwenda kuzika huwa hakuna anaepewa fursa hiyo

mimi natetea usawa hata kwenye kuonewa, tuonewe kwa usawa

unamuachia Kabendera kwani Rugemarila hajafiwa?

mahabusu woooote waliotiwa kizuizini awamu hii kwa kesi za dhulma hakuna aliyefiwa na mamaake?

hivi nyinyi hamna ndugu walioko humu majela ya Tanzania, hamuwaulizi? hamuwatembelei wakawaambia?
Well said,tatizo wananongonzwa na emotions na sio facts,Kabendera yeye ni nani hadi apate ruhusa ya kwenda kuzika mama yake?Wafungwa/Mahabusu kibao tu wanafiwa na watu wao wa karibu na hawapewi ruhusa ya kwenda kuzika.
 
Erick Kabendera mwandishi wa Kujitegemea wa Habari za uchunguzi inaendelea leo Mahakama ya Kisutu.

Kabendera anashtakiwa kwa Makosa matatu ikiwemo kukwepa Kodi, Utakatishaji Fedha na kujihusisha na genge la uhalifu.


UPDATES

MAHAKAMA YAOMBWA KABENDERA KUMUAGA MAMAKE


HOJA SITA ZA UPANDE WA UTETEZI KWANINI KABENDERA APEWE RUHUSA KUSHIRIKI MAZIKO YA MAMA YAKE

Jopo la mawakili wa Mwandishi wa habari wa kujitegemea Erick Kabendera, wakiongozwa na Wakili Jebra Kambole wamewasilisha hoja sita mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu Janet Mtega kwa mshitakiwa kupatiwa ruhusa chini ya ulinzi ili aweze kushiriki Katika maziko au kutoa heshima za mwisho kwa mama yake aliyefariki hivi karibuni.

1. Kutoa heshima za mwisho ni haki ya msingi ya binadamu. Wakili ameeleza kuwa Kabendera ana haki ya kuwa na kuheshimu familia pamoja na haki ya faragha hivyo kuna umuhimu kwa Kabendera kushiriki Katika kutoa heshima za mwisho kwa mama yake.

2. Erick Kabendera anatakiwa adhaniwe kuwa hajatenda kosa mpaka pale mahakama itakapothibitisha kuwa ametenda kosa na kumzuia kushiriki mazishi itakuwa ni adhabu ya Kinyama kwa Kabendera.

3. Tangu Mshitakiwa amekamatwa hajaonesha nia ya kutoroka au kutaka kufanya vurugu hivyo hakuna uwezekano wa mtuhumiwa kutoroka Kama atapatiwa ruhusa

4. Mashitaka anayokabiliwa nayo mshitakiwa hayahusiani na uvunjifu wa amani hivyo Mahakama itilie maanani ombi Hilo

5. Kama Mahakama ilitoa amri aende mahabusu hivyo Mahakama Ina uwezo wa kuamua ombi hilo kwani kama mshitakiwa pia aliweza kupelekwa mahakamani haitashindikana kumpeleka kanisani kumuaga mama yake.

6. Ruhusa ya Kabendera kuhudhuria mazishi Jamhuri haiwezi kuathirika



MAJIBU YA UPANDE WA SERIKALI

Jamhuri yampa pole nyingi kwa msiba wa mama yake mzazi, Bibi Verdiana Mjwahuzi. Pia Jamhuri imepinga hoja za utetezi wakidai Mahakama haina Mamlaka wala DPP hajaipa mamlaka ya kutoa maamuzi hayo.

Wakili wa Serikali, Simon Wankyo amesema...

"Hata sisi tuna masikitiko makubwa na tunampa pole nyingi Kabendera kwa kufiwa na mama yake mzazi, lakini mahakama isifungwe mikono kwa maombi yaliyowasilishwa ya kutaka mshtakiwa kushiriki Msiba.”

Mheshimiwa Hakimu katika macho ya kisheria mahakama yako haina mamlaka ya kusikiliza maombi hayo kwa sababu kesi hii ni ya uhujumu uchumi, licha ya kuwa hata sisi tuna masikitiko makubwa lakini tunaiomba Mahakama yako isifungwe mikono.”



Pia soma
Ombi limetupiliwa mbali
 
Hii ni vunga tu komando yoso anakuja hivi punde na kauli ya kusamehewa kwake ili sifa na utukufu umrudie yeye.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizi kesi za uhujumu u humi kwa waandishi wa habari zinatumika kisiasa.

Na kwa mwendo huu, serikali inapata "laana" za wazazi wanaofariki kwa pressure za watoto wao kufungwa.

Serikali ya Magufuli ina "laana" ya mama Kabendera.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kumbe you believe in curse

Where does it come from [emoji23][emoji23][emoji16][emoji16]

Heri ya mwaka mpya mkuu wangu kiranga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
huyu mtu ni mshitakiwa mama yake akizikwa hatapata tena nafasi ya kumuona zaidi ya kutembelea kaburi lake ni vema aruhusiwe apate nafasi ya mwisho kutoa heshima kwa mama yake hakuna mtu ajuaye kesho yake
Mawazo yangu Kama ya kwako,kwa mfungwa Sawa ila mahabusu!!!!!
 
Kwani Ni mfungwa huyo?
Ndo maana wanatafuta makosa kwake hivo tambua huwenda asikutwe na kosa,maana Bado Ni mtuhumiwa
 
Well said,tatizo wananongonzwa na emotions na sio facts,Kabendera yeye ni nani hadi apate ruhusa ya kwenda kuzika mama yake?Wafungwa/Mahabusu kibao tu wanafiwa na watu wao wa karibu na hawapewi ruhusa ya kwenda kuzika.
Jaribu kuwa na huruma

Mengine mezea moyoni itasaidia mkuu

Dunia ni Pana sana hii mkuu

Kuna siku utakumbuka haya maneno victorie
 
Jaribu kuwa na huruma

Mengine mezea moyoni itasaidia mkuu

Dunia ni Pana sana hii mkuu

Kuna siku utakumbuka haya maneno victorie
Nina huruma sana tu,lakini siwezi ruhusu huruma zangu zibypass facts.
 
Kabendera ni tofauti maana yeye amebambikiwa kesi ili akomolowe ili kumfurahisha rais. Kwahiyo jitahidi kuelewa hilo.
Haya ya kubambikwa kesi bado hayajathibitishwa na mahakama.
Ni mahakama ndio itatafsiri sheria kuonesha kama kabambikwa au ana hatia
 
Katika utawala huu wa Magufuli, Tanzania imekuwa ni Taifa la kidikteta lisilojali Utu,Haki,Usawa na Sheria kwa raia wake.
Anayotendewa Erick ni zaidi ya Unyama na Ukaburu ulokuwa unafanywa na Makaburu wa enzi za Utawala wa weupe wachache nchini Afrika Kusini.

Mtu kafiwa na mamake mzazi tena kuna uwezekano mkubwa kifo cha mama huyu kitakuwa kimechangiwa na Utawala huuhuu! Huu ni ukatili wa hali ya juu sana.

RIP Mama Mujahwuzi na pole sana Erick! Mungu ndiye atakayekulipia kwa watesi wako.
Kuna mtuhumiwa aliwahi kwenda kumzika mama au babake yake akiwa mahabusu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Well said,tatizo wananongonzwa na emotions na sio facts,Kabendera yeye ni nani hadi apate ruhusa ya kwenda kuzika mama yake?Wafungwa/Mahabusu kibao tu wanafiwa na watu wao wa karibu na hawapewi ruhusa ya kwenda kuzika.

We ajuza kaa kwa kutulia, huyo Kabendera hana kosa bali kosa lake ni kukosoa, hivyo anakomolewa. Pamoja na kukomolewa kwa kesi za kubambikiwa, bado aliomba alipe plea bargaining ili alipe kama wengine, lakini kwakuwa lengo ni kumkomoa bado walimgomea. Isitoshe unaenda mwezi wa sita huu, mbona hahukimiwi? Ww leta sura yako mbaya iliyokunjamana kaa ngozi ya goti, huku ukijifanya unajua sheria kumbe ni muuza mbunye tu.
 
Back
Top Bottom