Well said,tatizo wananongonzwa na emotions na sio facts,Kabendera yeye ni nani hadi apate ruhusa ya kwenda kuzika mama yake?Wafungwa/Mahabusu kibao tu wanafiwa na watu wao wa karibu na hawapewi ruhusa ya kwenda kuzika.
HOJA SITA ZA UPANDE WA UTETEZI KWANINI KABENDERA APEWE RUHUSA KUSHIRIKI MAZIKO YA MAMA YAKE
Jopo la mawakili wa Mwandishi wa habari wa kujitegemea Erick Kabendera, wakiongozwa na Wakili Jebra Kambole wamewasilisha hoja sita mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu Janet Mtega kwa mshitakiwa kupatiwa ruhusa chini ya ulinzi ili aweze kushiriki Katika maziko au kutoa heshima za mwisho kwa mama yake aliyefariki hivi karibuni.
1. Kutoa heshima za mwisho ni haki ya msingi ya binadamu. Wakili ameeleza kuwa Kabendera ana haki ya kuwa na kuheshimu familia pamoja na haki ya faragha hivyo kuna umuhimu kwa Kabendera kushiriki Katika kutoa heshima za mwisho kwa mama yake.
2. Erick Kabendera anatakiwa adhaniwe kuwa hajatenda kosa mpaka pale mahakama itakapothibitisha kuwa ametenda kosa na kumzuia kushiriki mazishi itakuwa ni adhabu ya Kinyama kwa Kabendera.
3. Tangu Mshitakiwa amekamatwa hajaonesha nia ya kutoroka au kutaka kufanya vurugu hivyo hakuna uwezekano wa mtuhumiwa kutoroka Kama atapatiwa ruhusa
4. Mashitaka anayokabiliwa nayo mshitakiwa hayahusiani na uvunjifu wa amani hivyo Mahakama itilie maanani ombi Hilo
5. Kama Mahakama ilitoa amri aende mahabusu hivyo Mahakama Ina uwezo wa kuamua ombi hilo kwani kama mshitakiwa pia aliweza kupelekwa mahakamani haitashindikana kumpeleka kanisani kumuaga mama yake.
6. Ruhusa ya Kabendera kuhudhuria mazishi Jamhuri haiwezi kuathirika
MAJIBU YA UPANDE WA SERIKALI
Jamhuri yampa pole nyingi kwa msiba wa mama yake mzazi, Bibi Verdiana Mjwahuzi. Pia Jamhuri imepinga hoja za utetezi wakidai Mahakama haina Mamlaka wala DPP hajaipa mamlaka ya kutoa maamuzi hayo.
Wakili wa Serikali, Simon Wankyo amesema...
"Hata sisi tuna masikitiko makubwa na tunampa pole nyingi Kabendera kwa kufiwa na mama yake mzazi, lakini mahakama isifungwe mikono kwa maombi yaliyowasilishwa ya kutaka mshtakiwa kushiriki Msiba.”
Mheshimiwa Hakimu katika macho ya kisheria mahakama yako haina mamlaka ya kusikiliza maombi hayo kwa sababu kesi hii ni ya uhujumu uchumi, licha ya kuwa hata sisi tuna masikitiko makubwa lakini tunaiomba Mahakama yako isifungwe mikono.”
Mama mzazi wa mwandishi Erick Kabendera, Verdiana Mjwahuzi amefariki dunia leo Jumanne Desemba 31, 2019. Amefariki akiwa Hospitali ya Amana alikokuwa akip Soma pia: - Mama Mzazi wa Erick Kabendera amuomba Rais Magufuli kumsamehe mwanae - Mwanahabari Erick Kabendera...
Well said,tatizo wananongonzwa na emotions na sio facts,Kabendera yeye ni nani hadi apate ruhusa ya kwenda kuzika mama yake?Wafungwa/Mahabusu kibao tu wanafiwa na watu wao wa karibu na hawapewi ruhusa ya kwenda kuzika.
huyu mtu ni mshitakiwa mama yake akizikwa hatapata tena nafasi ya kumuona zaidi ya kutembelea kaburi lake ni vema aruhusiwe apate nafasi ya mwisho kutoa heshima kwa mama yake hakuna mtu ajuaye kesho yake
Well said,tatizo wananongonzwa na emotions na sio facts,Kabendera yeye ni nani hadi apate ruhusa ya kwenda kuzika mama yake?Wafungwa/Mahabusu kibao tu wanafiwa na watu wao wa karibu na hawapewi ruhusa ya kwenda kuzika.
Katika utawala huu wa Magufuli, Tanzania imekuwa ni Taifa la kidikteta lisilojali Utu,Haki,Usawa na Sheria kwa raia wake.
Anayotendewa Erick ni zaidi ya Unyama na Ukaburu ulokuwa unafanywa na Makaburu wa enzi za Utawala wa weupe wachache nchini Afrika Kusini.
Mtu kafiwa na mamake mzazi tena kuna uwezekano mkubwa kifo cha mama huyu kitakuwa kimechangiwa na Utawala huuhuu! Huu ni ukatili wa hali ya juu sana.
RIP Mama Mujahwuzi na pole sana Erick! Mungu ndiye atakayekulipia kwa watesi wako.
Well said,tatizo wananongonzwa na emotions na sio facts,Kabendera yeye ni nani hadi apate ruhusa ya kwenda kuzika mama yake?Wafungwa/Mahabusu kibao tu wanafiwa na watu wao wa karibu na hawapewi ruhusa ya kwenda kuzika.
We ajuza kaa kwa kutulia, huyo Kabendera hana kosa bali kosa lake ni kukosoa, hivyo anakomolewa. Pamoja na kukomolewa kwa kesi za kubambikiwa, bado aliomba alipe plea bargaining ili alipe kama wengine, lakini kwakuwa lengo ni kumkomoa bado walimgomea. Isitoshe unaenda mwezi wa sita huu, mbona hahukimiwi? Ww leta sura yako mbaya iliyokunjamana kaa ngozi ya goti, huku ukijifanya unajua sheria kumbe ni muuza mbunye tu.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.