Kisutu: Kesi ya Erick Kabendera yaendelea. Jamhuri yaweka kisiki Erick kushiriki msiba wa mama yake mzazi

Hili kosa la kukwepa kodi ilikuwaje Makonda yeye hakushitakiwa pamoja na ushaidi wa wazi ulokuwapo kwenye ishu ya makontena
 
Nakuombea siku uko ndani gerezani, mama yako au baba yako wanafariki, na usiruhusiwe kwenda kuwaaga.

Sent using Unataka kujua ili iweje
 
Kwa nafasi yake raisi ana uwezo wa kila aina kuangalia afya ya mama yake mzazi.

Lakini wakati anaomboleza kifo cha dada yake (Monica) kitu kilichokuwa kinamsumbua nani ataziba pengo la Monica sio kwamba hana ndugu wengine. Isipokuwa Monica ndio mtoto ambae mama yao kamzoea na aliekuwa akimtegemea kwa mambo mengi ya kila siku including emotional support ata kama Magu ndio anagharamia.

Kwa ivyo huo uchungu raisi nae anaujua, usimfanyie mtu kitu ambacho wewe usingependa kufanyiwa.

Uwezi kumfunga mtoto wa mwenzako kwa kosa ambalo madhara yake ni makelele tu ambayo hayana impact zozote kwa serikari, kama adhabu sijui ipi itazidi hili kumsababishia kifo cha mama yake na kumzika pia wamnyime kuna watu wana roho mmbaya,
 
Umejibu vizuri,watanzania siku zote huwa wanalenga kupata huruma ni sawa na tabia za bati huwa linawahi kupata joto na kuwahi kupoa
 
Hili linafanya watu wawe na chuki na viongoz wao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ina maana hata wafungwa waanze kuhudhuria misiba?
Je kabendera ana uraia maalum tofauti na mahabusu wengine?

Tusimamie sheria na tuepuke mambo ya kujitakia.
[emoji1241][emoji818]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kila aliye,still kuwa mfungwa hakumzuii mtu kunyimwa haki za msingi

haki za msingi ndio zipi zinazolindwa ukiwa jela?

hata kuzaa ni haki ya msingi

Kabendera aachiwe akazae kisha arudi?

Huyu mwandishi kafanyiwa dhulma, na hayuko peke yake, lakini kuachiwa kwenda kuzika huwa hakuna anaepewa fursa hiyo

mimi natetea usawa hata kwenye kuonewa, tuonewe kwa usawa

unamuachia Kabendera kwani Rugemarila hajafiwa? Namtumia Rugemarila kama mfano wa prominent detainee, na sijui kama kafiwa lakini tunajuaje hajafiwa na mama, mke, mtoto, kaka, kipindi chote hiki ????

yani mahabusu woooote waliotiwa kizuizini awamu hii kwa kesi za dhulma hakuna aliyefiwa na mamaake?

hivi nyinyi hamna ndugu walioko humu majela ya Tanzania, hamuwaulizi? hamuwatembelei wakawaambia?
 
Kuna kitu sijaelewa ati mahakama yako haina mamlaka..... Sasa kwanini kesi iko hapo mahakamani??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana Erick, Mungu ni mwema siku zote. Atakulipia kwa haya unayotendewa. Siku hizi kesi kuu ni uhujumu uchumi. Inatisha sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…