Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 63,730
- 111,542
Wanatenda sana, ila haya ni ya kubambikizia fullstop.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wewe kula kulala nani ahangaike na wewe serikali ina hangaika na kina Kabendera ili waache kukupa vijisenti ili usitukana serikali. Naona hali yako ni mbaya sana nimeambiwa uchumi wako umeyumba.Wanasubiri nini kuninyonga? Mmeshanyonga wangapi mpaka sasa hivi ili nijue kwangu itakuwa muendelezo tu?
Sisi siku hizi haturopoki sana...Matokeo yatatoka wala usiwe na wasiwasi! Kuna siku utakuwa unalia sana humu Jf kwa ajili ya fulani! Short time ahead my friend! Hatunaga maneno maneno sana baada ya kugundua tunapokwama ni wapi! Discipline itatembea tu mkuu mark me!Wewe ni zaidi. Ndiyo mliokuwa mnapata pesa toka kwa mabeberu kupitia kwa Kabendera. Pole kunywa maji upunguze stress Kabendera karudishwa mahabusu hakuna cha kuaga wala kuzika. Mwakilishe mkuu!
Tatizo kina watu wanadhani serikali inaendeshwa kwa huruma na kuombewa na kusaidiana. Ikiwa ni hivyo nani angekuwa gerezani?
Huyu Simon wankyo atakuwa mchawi si bureView attachment 1310339
Awali:
Erick Kabendera mwandishi wa Kujitegemea wa Habari za uchunguzi inaendelea leo Mahakama ya Kisutu.
Kabendera anashtakiwa kwa Makosa matatu ikiwemo kukwepa Kodi, Utakatishaji Fedha na kujihusisha na genge la uhalifu.
UPDATES
MAHAKAMA YAOMBWA KABENDERA KUMUAGA MAMAKE
HOJA SITA ZA UPANDE WA UTETEZI KWANINI KABENDERA APEWE RUHUSA KUSHIRIKI MAZIKO YA MAMA YAKE
Jopo la mawakili wa Mwandishi wa habari wa kujitegemea Erick Kabendera, wakiongozwa na Wakili Jebra Kambole wamewasilisha hoja sita mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu Janet Mtega kwa mshitakiwa kupatiwa ruhusa chini ya ulinzi ili aweze kushiriki Katika maziko au kutoa heshima za mwisho kwa mama yake aliyefariki hivi karibuni.
1. Kutoa heshima za mwisho ni haki ya msingi ya binadamu. Wakili ameeleza kuwa Kabendera ana haki ya kuwa na kuheshimu familia pamoja na haki ya faragha hivyo kuna umuhimu kwa Kabendera kushiriki Katika kutoa heshima za mwisho kwa mama yake.
2. Erick Kabendera anatakiwa adhaniwe kuwa hajatenda kosa mpaka pale mahakama itakapothibitisha kuwa ametenda kosa na kumzuia kushiriki mazishi itakuwa ni adhabu ya Kinyama kwa Kabendera.
3. Tangu Mshitakiwa amekamatwa hajaonesha nia ya kutoroka au kutaka kufanya vurugu hivyo hakuna uwezekano wa mtuhumiwa kutoroka Kama atapatiwa ruhusa
4. Mashitaka anayokabiliwa nayo mshitakiwa hayahusiani na uvunjifu wa amani hivyo Mahakama itilie maanani ombi Hilo
5. Kama Mahakama ilitoa amri aende mahabusu hivyo Mahakama Ina uwezo wa kuamua ombi hilo kwani kama mshitakiwa pia aliweza kupelekwa mahakamani haitashindikana kumpeleka kanisani kumuaga mama yake.
6. Ruhusa ya Kabendera kuhudhuria mazishi Jamhuri haiwezi kuathirika
MAJIBU YA UPANDE WA SERIKALI
Jamhuri yampa pole nyingi kwa msiba wa mama yake mzazi, Bibi Verdiana Mjwahuzi. Pia Jamhuri imepinga hoja za utetezi wakidai Mahakama haina Mamlaka wala DPP hajaipa mamlaka ya kutoa maamuzi hayo.
Wakili wa Serikali, Simon Wankyo amesema...
"Hata sisi tuna masikitiko makubwa na tunampa pole nyingi Kabendera kwa kufiwa na mama yake mzazi, lakini mahakama isifungwe mikono kwa maombi yaliyowasilishwa ya kutaka mshtakiwa kushiriki Msiba.”
Mheshimiwa Hakimu katika macho ya kisheria mahakama yako haina mamlaka ya kusikiliza maombi hayo kwa sababu kesi hii ni ya uhujumu uchumi, licha ya kuwa hata sisi tuna masikitiko makubwa lakini tunaiomba Mahakama yako isifungwe mikono.”
Soma:TANZIA - Mama mzazi wa Mwandishi Erick Kabendera, Verdiana Mjwahuzi amefariki dunia leo Jumanne Desemba 31, 2019
Mama mzazi wa mwandishi Erick Kabendera, Verdiana Mjwahuzi amefariki dunia leo Jumanne Desemba 31, 2019. Amefariki akiwa Hospitali ya Amana alikokuwa akip Soma pia: Mama Mzazi wa Erick Kabendera amuomba Rais Magufuli kumsamehe mwanaewww.jamiiforums.com
Sheria ni Sheria na huruma ni huruma!
Siku hiyo tunaanza na wewe!Sisi siku hizi haturopoki sana...Matokeo yatatoka wala usiwe na wasiwasi! Kuna siku utakuwa unalia sana humu Jf kwa ajili ya fulani! Short time ahead my friend! Hatunaga maneno maneno sana baada ya kugundua tunapokwama ni wapi! Discipline itatembea tu mkuu mark me!
PoaSiku hiyo tunaanza na wewe!
Wewe kula kulala nani ahangaike na wewe serikali ina hangaika na kina Kabendera ili waache kukupa vijisenti ili usitukana serikali. Naona hali yako ni mbaya sana nimeambiwa uchumi wako umeyumba.
Au tuanze na wewe sasa hivi? Then waje wanasaccos waanze kulalamika kama wanavyolalamika sasa hivi kwa Kabendera??
Wewe uko lazy mno wanahitajika watu wanaojitegemea siyo kula kulala mkuu!Ni kweli aisee, kwa hiyo mimi sintanyogwa kama wale wengine mliowanyonga? Uchumi wangu umeyumba muda sana mkuu, nipeni na mimi ajira huko kwenye kundi lenu la watu wasiojulikana niwe na maisha kama ww.
Sijibizani na wajinga!Au tuanze na wewe sasa hivi? Then waje wanasaccos waanze kulalamika kama wanavyolalamika sasa hivi kwa Kabendera??
Unyama wa hali ya juu kabisa. Watalipwa hapa hapa!Mjibu vizuri alichosema, je kuna utaratibu wa kisheria kwa mfungwa au mahabusu wa kutolewa gerezani na kwenda kushiriki msiba au tukio lolote?
Sent using Jamii Forums mobile app
Usiandike kutoka kwenye hisia tu. Hivi, mnajua kuna Watanzania wangapi wako rumande au jela na wamepoteza wapendwa wao? Suala hapa lilitakiwa kuulizwa (badala ya kuomba) ni utaratibu gani uliopo kisheria wa mfungwa au mshtakiwa aliye rumande anapopata msiba? Na je utaratibu huo kwanini usitumike (kama upo) kwa Eric Kabendera? Hili ndilo swali langu badala ya kutoa lawama tu. Maana binadamu wote ni sawa. Ila kama huwa hawaruhusiwi kwenda kwenye misiba hata kama ni wa baba au mama, au mtoto, kwanini iwe tofauti kwa Kabendera? Tuwe na ubinadamu, mwenzetu kafiwa na Mungu ampe faraja sana lakini tusije tukajiona miungu wa kudhania tunajua majibu ya maswali ya umilele.Akina Mzee Mwanakijiji huwa hawaoni huu upande. Wao wanaona mazuri tu...!!