Kisutu: Kesi ya Erick Kabendera yaendelea. Jamhuri yaweka kisiki Erick kushiriki msiba wa mama yake mzazi

Kisutu: Kesi ya Erick Kabendera yaendelea. Jamhuri yaweka kisiki Erick kushiriki msiba wa mama yake mzazi

Wanasubiri nini kuninyonga? Mmeshanyonga wangapi mpaka sasa hivi ili nijue kwangu itakuwa muendelezo tu?
Wewe kula kulala nani ahangaike na wewe serikali ina hangaika na kina Kabendera ili waache kukupa vijisenti ili usitukana serikali. Naona hali yako ni mbaya sana nimeambiwa uchumi wako umeyumba.
 
Wewe ni zaidi. Ndiyo mliokuwa mnapata pesa toka kwa mabeberu kupitia kwa Kabendera. Pole kunywa maji upunguze stress Kabendera karudishwa mahabusu hakuna cha kuaga wala kuzika. Mwakilishe mkuu!
Sisi siku hizi haturopoki sana...Matokeo yatatoka wala usiwe na wasiwasi! Kuna siku utakuwa unalia sana humu Jf kwa ajili ya fulani! Short time ahead my friend! Hatunaga maneno maneno sana baada ya kugundua tunapokwama ni wapi! Discipline itatembea tu mkuu mark me!
 
View attachment 1310339

Awali:


Erick Kabendera mwandishi wa Kujitegemea wa Habari za uchunguzi inaendelea leo Mahakama ya Kisutu.

Kabendera anashtakiwa kwa Makosa matatu ikiwemo kukwepa Kodi, Utakatishaji Fedha na kujihusisha na genge la uhalifu.


UPDATES

MAHAKAMA YAOMBWA KABENDERA KUMUAGA MAMAKE


HOJA SITA ZA UPANDE WA UTETEZI KWANINI KABENDERA APEWE RUHUSA KUSHIRIKI MAZIKO YA MAMA YAKE

Jopo la mawakili wa Mwandishi wa habari wa kujitegemea Erick Kabendera, wakiongozwa na Wakili Jebra Kambole wamewasilisha hoja sita mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu Janet Mtega kwa mshitakiwa kupatiwa ruhusa chini ya ulinzi ili aweze kushiriki Katika maziko au kutoa heshima za mwisho kwa mama yake aliyefariki hivi karibuni.

1. Kutoa heshima za mwisho ni haki ya msingi ya binadamu. Wakili ameeleza kuwa Kabendera ana haki ya kuwa na kuheshimu familia pamoja na haki ya faragha hivyo kuna umuhimu kwa Kabendera kushiriki Katika kutoa heshima za mwisho kwa mama yake.

2. Erick Kabendera anatakiwa adhaniwe kuwa hajatenda kosa mpaka pale mahakama itakapothibitisha kuwa ametenda kosa na kumzuia kushiriki mazishi itakuwa ni adhabu ya Kinyama kwa Kabendera.

3. Tangu Mshitakiwa amekamatwa hajaonesha nia ya kutoroka au kutaka kufanya vurugu hivyo hakuna uwezekano wa mtuhumiwa kutoroka Kama atapatiwa ruhusa

4. Mashitaka anayokabiliwa nayo mshitakiwa hayahusiani na uvunjifu wa amani hivyo Mahakama itilie maanani ombi Hilo

5. Kama Mahakama ilitoa amri aende mahabusu hivyo Mahakama Ina uwezo wa kuamua ombi hilo kwani kama mshitakiwa pia aliweza kupelekwa mahakamani haitashindikana kumpeleka kanisani kumuaga mama yake.

6. Ruhusa ya Kabendera kuhudhuria mazishi Jamhuri haiwezi kuathirika



MAJIBU YA UPANDE WA SERIKALI

Jamhuri yampa pole nyingi kwa msiba wa mama yake mzazi, Bibi Verdiana Mjwahuzi. Pia Jamhuri imepinga hoja za utetezi wakidai Mahakama haina Mamlaka wala DPP hajaipa mamlaka ya kutoa maamuzi hayo.

Wakili wa Serikali, Simon Wankyo amesema...

"Hata sisi tuna masikitiko makubwa na tunampa pole nyingi Kabendera kwa kufiwa na mama yake mzazi, lakini mahakama isifungwe mikono kwa maombi yaliyowasilishwa ya kutaka mshtakiwa kushiriki Msiba.”

Mheshimiwa Hakimu katika macho ya kisheria mahakama yako haina mamlaka ya kusikiliza maombi hayo kwa sababu kesi hii ni ya uhujumu uchumi, licha ya kuwa hata sisi tuna masikitiko makubwa lakini tunaiomba Mahakama yako isifungwe mikono.”


Soma:
Huyu Simon wankyo atakuwa mchawi si bure

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sisi siku hizi haturopoki sana...Matokeo yatatoka wala usiwe na wasiwasi! Kuna siku utakuwa unalia sana humu Jf kwa ajili ya fulani! Short time ahead my friend! Hatunaga maneno maneno sana baada ya kugundua tunapokwama ni wapi! Discipline itatembea tu mkuu mark me!
Siku hiyo tunaanza na wewe!
 
Wewe kula kulala nani ahangaike na wewe serikali ina hangaika na kina Kabendera ili waache kukupa vijisenti ili usitukana serikali. Naona hali yako ni mbaya sana nimeambiwa uchumi wako umeyumba.

Ni kweli aisee, kwa hiyo mimi sintanyogwa kama wale wengine mliowanyonga? Uchumi wangu umeyumba muda sana mkuu, nipeni na mimi ajira huko kwenye kundi lenu la watu wasiojulikana niwe na maisha kama ww.
 
Ni kweli aisee, kwa hiyo mimi sintanyogwa kama wale wengine mliowanyonga? Uchumi wangu umeyumba muda sana mkuu, nipeni na mimi ajira huko kwenye kundi lenu la watu wasiojulikana niwe na maisha kama ww.
Wewe uko lazy mno wanahitajika watu wanaojitegemea siyo kula kulala mkuu!
 
Ila huu.ni ukatili wa hali ya juu sana,naimani ipo siku kabendela atakuja kuingia ikulu na kuna familia zitakuja kunyongwa na kuishia mahakani.
Haiwezekani mtu afanyiwe ukatili kiasi hiki hata kama kesho mtu anachukuwa nchi hii huwezi sahau hujuma hizi lazima ujifunze kuumiza hata kama wewe ni swala tano, inauma na inaumiza huyu jamaa yuko na wakati mgumu sana mungu amsaidie na amtie nguvu ili aweze kuyashinda na kuyapita haya yote maana ni mateso ni sawa na mtu akushushe kwenye bwawa la mamba.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Natoa rai kwa kila mwanakagera 2020 bwana yule tusimpe na wawakilishi wote wa CCM wa ngazi za udiwani na ubunge waende na maji. Namchukia sana..I can't express my hatred into words.
 
Akina Mzee Mwanakijiji huwa hawaoni huu upande. Wao wanaona mazuri tu...!!
Usiandike kutoka kwenye hisia tu. Hivi, mnajua kuna Watanzania wangapi wako rumande au jela na wamepoteza wapendwa wao? Suala hapa lilitakiwa kuulizwa (badala ya kuomba) ni utaratibu gani uliopo kisheria wa mfungwa au mshtakiwa aliye rumande anapopata msiba? Na je utaratibu huo kwanini usitumike (kama upo) kwa Eric Kabendera? Hili ndilo swali langu badala ya kutoa lawama tu. Maana binadamu wote ni sawa. Ila kama huwa hawaruhusiwi kwenda kwenye misiba hata kama ni wa baba au mama, au mtoto, kwanini iwe tofauti kwa Kabendera? Tuwe na ubinadamu, mwenzetu kafiwa na Mungu ampe faraja sana lakini tusije tukajiona miungu wa kudhania tunajua majibu ya maswali ya umilele.
 
Back
Top Bottom