No PERMISSION
Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu imekubali pingamizi la upande wa mashtaka la kumzuia mwanahabari Erick Kabendera kuhudhuria mazishi ya mama yake mzazi, Bi.Verdiana Mwahuzi, yatakayofanyika hapo kesho.
Awali upande wa utetezi uliomba Mahakama kutoa ruhusa kwa Kabendera kumuaga mama yake aliyefariki Disemba 31, lakini Wakili wa serikali Wankyo Simon amesemahoja zilizowasilishwa hazina mashiko na kuiomba Mahakama kutupilia mbali maombi hayo.
Pia Wankyo ameeleza kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kumpa ruhusa Kabendera, bali mamlaka hiyo ni ya DPP, na DPP hajatoa ruhusa. Hivyo mama yake Kabendera atazikwa bila uwepo wa mwanae.!