Kisutu: Kesi ya Freeman Mbowe yaahirishwa hadi Kesho 06/08/2021, Mtandao umesumbua

Kisutu: Kesi ya Freeman Mbowe yaahirishwa hadi Kesho 06/08/2021, Mtandao umesumbua

Tunajua Nulad yupo! Wakati wa Euromaidan alikuwepo.
=====
Hivi hawa wamekuja kusikiliza kesi ama wamekuja kuingilia uhuru wa mahakama katika kesi hii?. Hii wapi karama ya watu hawa juu ya kuhimiza serikali ifuate sheria kwa mujibu wa katiba yao na Ilani zao zauchaguzi?
Ukishajua kuandika vizuri vitu vikasomeka,urudi tena
 
Kikundi cha watu 50 wanataka kuleta vurugu, peleka ndani wakalale na kunguni wakitoka j3 waende kuwasimulia wenzao vizuri Clubhouse na Maria Space.
Nashangaa police wananipita Kama hawanioni au sionekani? Nawapiga picha hawanioni, au niwasogelee niwaguse SHATI,
 
Hapo wakubwa wameamua kupima upepo ili kuona nini Wanachadema wangefanya leo. Mwisho wameamua wawalete tu watuhumiwa physically mahakamani.
 
Polisi leo kila kona wanazurura na magari ya washa washa kwelii chdm pamoja na kubanwa kote lakini bado ni tishio kwa ccm maana ccm ni jeshi LA polisi.
Ni Asubuhi tulivu ya siku ya Alhamisi.

Kiongozi mkuu wa Upinzani Freeman Mbowe anatarajiwa kuletwa mahakamani Kisutu Leo katika Kesi ya Ugaidi.

Kesi hii inavuta kila mpenda haki na mwanademokrasia kutokana na ukweli Mbowe amebambikizwa kesi hii ili kumnyamazisha kutokana na Kampeni aliyoasisi ya Kudai Katiba Mpya

Mahakama hii inatarajiwa kufurika umati mkubwa wa watu kulaani unyama na uonevu wa vyombo vya dola.Ikumbukwe ni juzi tu bila Aibu alijitokeza IGP Simon Sirro na kuingilia mhimili wa Mahakama kwa kumhukumu Mbowe huku akijua kesi iko mahakamani.

Watu wengine wanaotarajiwa kufurika Kisutu ni Wawakilishi kutoka Jumuiya ya Ulaya, Marekani na balozi kadhaa nchini huku vyombo vikubwa vya Habari Duniani BBC, VOA, DW na Aljazeera vikitarajiwa kuwa live mahakamani.

Molemo media tayari iko kwenye viwanja vya Mahakama hii kuwaletea kila kinachojiri.

Updates
Imethibitishwa kwamba Freeman Mbowe hataletwa mahakamani na badala yake kesi inaendeshwa kwa njia ya Mtandao (Video Conference)

Taarifa za Uhakika ni kwamba dola Wana hofu kubwa kumleta Mbowe Mahakamani kutokana na Hasira ya wananchi.

Pamoja na vitisho vya IGP Simon Sirro alivyotoa juzi dhidi ya watakaohudhuria mahakamani Kisutu na kuongea uongo mwingi dhidi ya Mbowe lakini Leo idadi kubwa ya watu imehudhuria mahakamani na wengine wakiendelea kumiminika kabla ya kuanza kuondoka baada ya Taarifa kwamba kesi itaendeshwa kimtandao.

Kamanda wa Polisi DSM Muliro Jumanne alifika mapema Kisutu kuona Hali ya mambo huku kukiwa na Askari zaidi ya 100 wenye silaha na wengine waliovalia kiraia.

Pamoja na Serikali kuogopa kumleta Mbowe Mahakamani lakini ni wazi Kelele za umma unaotaka haki zimewatisha na kuwaogofya

Kesi Yaahirishwa
Ilipotimu saa 4 na dakika 20 kesi Imeahirishwa hadi kesho Ijumaa tarehe 6 August saa 3 Asubuhi kutokana na kile kilichoelezwa ni matatizo ya kimtandao

=====

KISUTU, DAR: Kesi ya Freeman Mbowe (CHADEMA) imeahirishwa hadi Kesho kutokana na muonekano hafifu wa Video Conference

Watuhumiwa wataletwa kesho saa 3 asubuhi mahakamani (Physically)

View attachment 1880638

Si leo
 
Uzee dawa.

Mzee Mgaya jana aliwashauri wafuasi wa Chadema wasiende mahakama ya kisutu jijini Dar es salaam kwa sababu kesi za Ugaidi huendeshwa kwa njia ya mtandao.

Johnthebaptist nilileta uzi hapa nikimnukuu mzee Mgaya lakini ukafutwa.

Muda huu Mgaya kanipigia simu anasema uzee dawa na siasa siyo uadui.

Mungu ni mwema wakati wote!
 
Unadhani hiki unachoandika hapa kitafuta udhalimu wa yule ibilisi aliyeko motoni? Hata huyu mama wa kambo aaue wapinzani wote hapo uwanja wa taifa, bado lile takataka lilikuwa ni janga kwa nchi hii. Tunamshukuru Mungu kwa kutuondolea yule mtu muovu bila damu kumwagika.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Aliwaondolea lile jitu ovu bila damu kumwagika na sasa mambo ni safi! Mama yuko vizuri hadi magaidi sasa yanakamatwa!

Kumbe lile takataka lilikuwa linalea magaidi!

Makofi kwa mama
 
Ok. Wewe Mama D Kama Mama D mtazamo wako kuhusu katiba Ni upi?

Je ni (a)unaunga mkono kuwa tunaihitaji katiba mpya au ni (b) Hauungi mkono uhitaji wa katiba mpya.

Jibu fupi fupi tu.(a) au (b).

Mabadiliko ya katiba ni muhimu sana kadri ya uhitaji na maboresho ya nchi

Tunahitaji katiba mpya kadri ya mahitaji ya taifa letu kwa vizazi vya sasa na vijavyo na sio katiba kwa maslahi ya kikundi cha watu wala chama flani
 


Kesi ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe, imeahirishwa hadi kesho Agosti 6, 2021, kutokana na muonekano hafifu wa video conference, kesi hiyo ilikuwa inaendeshwa kwa mfumo huo, ambapo kesho atafikishwa mahakamani majira ya saa 3:00 asubuhi.

Kesi hiyo ya ugaidi ilikuwa itajwe leo Agosti 5, 2021, ambapo Mbowe na wenzake walikuwa katika Gereza la Ukonga Dar es Salaam lakini kutokana na matatizo ya mtandao ilishindwa kuendeshwa vizuri.

Akizungumza hii leo mara baada ya kesi hiyo kuahirishwa Wakili wa upande wa utetezi Peter Kibatala, amesema kuwa, "Teknolojia imefeli hivyo tumeshindwa kufanikisha mchakato huo kwa sababu kumekuwa na mawasiliano hafifu kati ya video conference facility za hapa katika Mahakama ya Kisutu na Gereza la Ukonga na tumekubaliana kwamba kesho washtakiwa waletwe mahakamani," ameeleza Wakili Kibatala

SOURCE; MPEKUZI
 
Mabadiliko ya katiba ni muhimu sana kadri ya uhitaji na maboresho ya nchi

Tunahitaji katiba mpya kadri ya mahitaji ya taifa letu kwa vizazi vya sasa na vijavyo na sio katiba kwa maslahi ya kikundi cha watu wala chama flani
Nimeomba jibu liwe fupi fupi . Je jibu ni (a) au (b) ??
Maelezo mengi hayatakiwa.
 
kwa hiyo kesi inaendelea huko kwa njia ya mtandao sasa hivi?
 
Nimeomba jibu liwe fupi fupi . Je jibu ni (a) au (b) ??
Maelezo mengi hayatakiwa.

Mimi sio kilaza nikupe jibu kwa kujaribisha

Nimekupa jibu na sababu pia

Sawa eeeeh
 
Km kweli amewahi kuuza madawa club akatuharibia mamia ya vijana basi yote kheri wakuadhibu waadhibu
 
Back
Top Bottom