Kisutu: Kesi ya Freeman Mbowe yaahirishwa hadi Kesho 06/08/2021, Mtandao umesumbua

Kisutu: Kesi ya Freeman Mbowe yaahirishwa hadi Kesho 06/08/2021, Mtandao umesumbua

Ni Asubuhi tulivu ya siku ya Alhamisi.

Kiongozi mkuu wa Upinzani Freeman Mbowe anatarajiwa kuletwa mahakamani Kisutu Leo katika Kesi ya Ugaidi.

Kesi hii inavuta kila mpenda haki na mwanademokrasia kutokana na ukweli Mbowe amebambikizwa kesi hii ili kumnyamazisha kutokana na Kampeni aliyoasisi ya Kudai Katiba Mpya

Mahakama hii inatarajiwa kufurika umati mkubwa wa watu kulaani unyama na uonevu wa vyombo vya dola.Ikumbukwe ni juzi tu bila Aibu alijitokeza IGP Simon Sirro na kuingilia mhimili wa Mahakama kwa kumhukumu Mbowe huku akijua kesi iko mahakamani.

Watu wengine wanaotarajiwa kufurika Kisutu ni Wawakilishi kutoka Jumuiya ya Ulaya, Marekani na balozi kadhaa nchini huku vyombo vikubwa vya Habari Duniani BBC, VOA, DW na Aljazeera vikitarajiwa kuwa live mahakamani.

Molemo media tayari iko kwenye viwanja vya Mahakama hii kuwaletea kila kinachojiri.

Updates
Imethibitishwa kwamba Freeman Mbowe hataletwa mahakamani na badala yake kesi inaendeshwa kwa njia ya Mtandao (Video Conference)

Taarifa za Uhakika ni kwamba dola Wana hofu kubwa kumleta Mbowe Mahakamani kutokana na Hasira ya wananchi.

Pamoja na vitisho vya IGP Simon Sirro alivyotoa juzi dhidi ya watakaohudhuria mahakamani Kisutu na kuongea uongo mwingi dhidi ya Mbowe lakini Leo idadi kubwa ya watu imehudhuria mahakamani na wengine wakiendelea kumiminika kabla ya kuanza kuondoka baada ya Taarifa kwamba kesi itaendeshwa kimtandao.

Kamanda wa Polisi DSM Muliro Jumanne alifika mapema Kisutu kuona Hali ya mambo huku kukiwa na Askari zaidi ya 100 wenye silaha na wengine waliovalia kiraia.

Pamoja na Serikali kuogopa kumleta Mbowe Mahakamani lakini ni wazi Kelele za umma unaotaka haki zimewatisha na kuwaogofya

Kesi Yaahirishwa
Ilipotimu saa 4 na dakika 20 kesi Imeahirishwa hadi kesho Ijumaa tarehe 6 August saa 3 Asubuhi kutokana na kile kilichoelezwa ni matatizo ya kimtandao

=====

KISUTU, DAR: Kesi ya Freeman Mbowe (CHADEMA) imeahirishwa hadi Kesho kutokana na muonekano hafifu wa Video Conference

Watuhumiwa wataletwa kesho saa 3 asubuhi mahakamani (Physically)

Kesho mtandao utakuwepo? Kila mara ninapoenda TRA kulipa lugha iliyozoeleka huko ni mtandao unasumbua! Wahusika wameamua kutumia njia ya kuwavuruga watu kiasaikolojia tu ili wahudhuriaji wapungue mmoja baada ya mwingine.
 
Kama na wewe upo hapo kisutu naomba nisahihishe idadi. Watakua 18 🤣🤣🤣
Mimi nilikuwa Chadema ila naichukia kwa vile wanamwendekeza mpuuzi Tundu Lissu ambaye ni mbinafsi ajabu
 
Kuna watu wanasema hapo watu wameandamana [emoji23][emoji23][emoji23] wafuasi wa chadema Kusimama na vijibango ety ndo kuandamana [emoji23][emoji23][emoji23] Watu wenyewe hata hawajai kwenye difenda ya police.
Acha umbeya mpikie mumeo chakula
 
Hivi unamkumbuka mdude alijigamba vipi baada ya kusamehewa? Kiongozi gani anakubali maneno ya kejeli kama hayo. Midomo inawaponza
Kama maneno ya kejeli huwezi yavumilia achia ngazi kaa pembenj hulazimishwi kuwa kiongozi na uongozi ni hiari sio utumwa.
 
Mulemule naye kaufayta wakati aliapa kuishauri serikali kwa uaminifu!

Na kuishi kote ughaibuni hajui kuwa wazungu hawana dogo kwenye suala la Amani hasa wanaposokia UGHAIDI. Kuna point tunapoteza hapa halafu wanakuja kutumia nguvu kuimarisha uchumi wa kisiasa!
Fungua bichwa lako weyee!
Wangejua umuhimu wa amani, haki za binaadamu na utawala wa sheria, wasingekuwa wanawabagua, kuwaua na kuwadharirisha Wamarekani weusi kule kwao!
 
Hivi unamkumbuka mdude alijigamba vipi baada ya kusamehewa? Kiongozi gani anakubali maneno ya kejeli kama hayo. Midomo inawaponza
Unajivua sidiria yako ya mtumba. ! Mdude kaachiwa na SSH au na mahakama?
Unataka awe loyal baada ya kuteswa na asiseme tena?
Kajambe mbele huko...!
Nyie ndio watu ambao baba zenu waliungana na wakoloni tusipate uhuru mapema.
 
Nngefurahi sana nyie wafuasi uchwara mlioandamana mngekula kipigo heavy weight
 
Nngefurahi sana nyie wafuasi uchwara mlioandamana mngekula kipigo heavy weight
Ndio ungeongeza kipato?Hizi chuki zitatufikisha pabaya!Tutarudi kulekule kwenye kusherehekea misiba ya jirani!
 
Mambo ya usalama wa ndani ya nchi yatabaki kuwa ya nchi.

Tanzania is a sovereign coutry.

ila Chadema hakikufaa kabisaa kuwa chama cha upinzani nchini Tanzania kwa tabia ya mara kwa mara wanayo ionyesha inapo tokea jambo lolote basi wanaenda kuichongea Tanzania kwa mataifa makubwa wakitegemea Viongozi wetu wataogopa!! thubutu!!!! kamwe tusivumilie tabia hii ya kizandiki!!! labda wakafanye siasa zao Burundi lkn sio Tz.

Tunaomba viongozi wetu wasiyumbe kabisa, wawe imara kusimamia sheria za nchi.

Demokrasia sio kuvunja amani.
Kmmmk
 
Ndio ungeongeza kipato?Hizi chuki zitatufikisha pabaya!Tutarudi kulekule kwenye kusherehekea misiba ya jirani!
Mbona nyie mlisheherekea msiba wa Magufuli.? Mnavoandamana mnapata faida gani zaidi ya kufaidisha matumbo ya wanasiasa.? Kwenye hayo maandamano umemuona kiongozi yupi ambaye hua anawahamasisha kuandamana.?
Tumia akili za kiutu uzima mzee
 
Narudia,chuki haziwezi kukusogeza hatua moja mbele kwenye maisha yako!Sanasana itakutesa tu!
Nimemuona Sugu na Mnyika wakiingia Kisutu!Hao wengine hawajaruhusiwa labda kutokana na ufinyu wa eneo!So naona viongozi wa CDM hawako nyuma!
Maandamano na kukusanyika ni haki ya kikatiba,kama hayana maana basi badilisheni katiba muyaondoe!
 
Wenzetu Kenya na Uganda wanajiweka kwenye ramani ya dunia kwenye Olympics na kujiletea sifa kedekede sisi tunaendelea kujiharibia huko CNN BBC na ALJAZEERA kwa kesi za kitoto.
Why do we devote most of our time on petty issues???
Shule hazina madarasa, wengine wanashea darasa kwa wakati mmoja sisi tunahangaika na Mbowe.
Watu wanatumia v8 lkn hofu yao kubwa Ni Mbowe.
Believe me CCM wanamuogopa Mbowe kuliko uviko
 
Hivi unamkumbuka mdude alijigamba vipi baada ya kusamehewa? Kiongozi gani anakubali maneno ya kejeli kama hayo. Midomo inawaponza
Ukiona kiongozi anaongoza kwa kutumia mihemko, basi huyo hafai kuwa kiongozi.

Uongozi ni kupakwa matoke
 
Narudia,chuki haziwezi kukusogeza hatua moja mbele kwenye maisha yako!Sanasana itakutesa tu!
Nimemuona Sugu na Mnyika wakiingia Kisutu!Hao wengine hawajaruhusiwa labda kutokana na ufinyu wa eneo!So naona viongozi wa CDM hawako nyuma!
Maandamano na kukusanyika ni haki ya kikatiba,kama hayana maana basi badilisheni katiba muyaondoe!
Mm sina ushabiki wa chama chochote hapa Tz, lakini chadema msipobadili aina ya mapambano yenu kwenye kudai hiyo demokrasia mnayoitaka bc mtaendelea kulia-lia milele na hamtofanikiwa. Endelea kupambana kwa ajili ya tumbo la mwanasiasa ashibe na mkipata shida hakuna atakayewajua
 
Back
Top Bottom