KISUTU: Mahakama upande wa Watoto yatupilia mbali shtaka la Hamisa Mobetto dhidi ya Diamond kuhusu malezi ya mtoto wao

Anasikiliza sana kelele za watu sasa atajifunza kama mambo ya familia yanahitaji busara zaidi
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu upande wa Watoto imetupilia mbali kesi aliyofunguliwa na Modo Hamisa Mobeto dhidi ya mwanamuziki Diamond Platnumz juu ya matunzo ya mtoto Prince Abdul.
Uamuzi huo umetolewa leo Ijumaa Novemba 10 ,2017 na Hakimu Devotha Kisoka wa Mahakama hiyo baada ya kusikiliza hoja za pande hizo mbili husika.
Diamond aliwasilisha pingamizi dhidi ya kesi hiyo iliyofunguliwa na Mobeto akidai kuwa kesi hiyo imefunguliwa kwa kutumia kifungu ambacho si sahihi. Hoja ambayo ilipingwa na Mobeto.
Mobeto alifungua kesi hiyo mahakamani hapo, pamoja na mambo mengine anaiomba matunzo ya mtoto waliozaa na msanii Diamond.
Mobeto anaiomba mahakama imwamuru Diamond kutoa matunzo ya mtoto ya kila mwezi na alifungua kesi hiyo kupitia mawakili wake Abdullah Lyana na Walter Godluck kutoka kampuni ya uwakili ya Century Attorneys.
Kupitia hati hiyo ya madai, Mobeto anaomba Diamond amuombe msamaha kwa kumsababishia madhara yaliyoishtua familia yake
Diamond aliwasilisha hati ya majibu hayo kinzani akipinga maombi hayo ya Mobeto akidai gharama anazodai kulipwa kwa mwezi ya Sh 5 milioni kwa ajili ya matunzo ya mtoto ni kubwa hawezi kuzimudu.
 
Kwahiyo mkuu mahakama imesemaje sasa kwamba alipe kidogo au asilipe kabisa hata mia
Ataendelea kupokea kile kile anacho pewa na Diamond maana mahakama imeona hakuna case ya kujibu..
 
Teh Teh....ngoja nitumie style hii ya wale majaa wa face book.....
Kumuona Da Mange akitokwa jasho baada ya kupata habari hii gonga like.....
hahahahahaha
 
Tatizo la hamisa anapenda show off na kuwarusha wabaya wake,maisha ya mashindano mitandaon jumlisha support ya uongo na kweli toka kwa mange ndo maana hawez ona hasara maana hapo anategemea zile photoshoot kumlindia heshima ya mtandaoni kuliko njaa ya maisha halisi

Kwa zari bora ana kaurithi ka ivan na anavyopenda bata sasa lazima ajichotee ka akiba kake aendelee kulinda ka cheo ka ubosslady. Mujini pagumu acha tu watu waishi kwa maigizo
 
Mange kuepuka aibu keshajitungia story zamaan. Na misukule yake imeshangilia balaa utadhan inafaidika kwenye hio child support
Teh Teh....ngoja nitumie style hii ya wale majaa wa face book.....
Kumuona Da Mange akitokwa jasho baada ya kupata habari hii gonga like.....
hahahahahaha
 
Zari mjanja yule...hata Domo akimnyima cash anajua jinsi ya kumkamua!

Atatumia hata njia za kimafia ili apate mshiko kwa Domo, na afterall yy ana mitego kibao ya kumkamatisha!

Sasa hamisa anategemea child support tu maana itakuwa Domo hata kitumbua chake hakitaki tena, anaogopa camera[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Mange kuepuka aibu keshajitungia story zamaan. Na misukule yake imeshangilia balaa utadhan inafaidika kwenye hio child support
Yule hakimu ni jembe mama makini. Huwa anachukia mtu kufanya mtoto kama kinga na njia ya kutekeleza matamanio yako. Uamuzi huu nimeupenda ingawa kosa la mabeto ambalo akinamama wengi wanalo hawaangalii future ya mtoto. Imagine zari ndiyo kwa sasa anamiliki Diamond why for heaven sake uoneshe picha upo katika kitanda cha zari na hata mtandio wake na kesho ampende mwanao? Je hujui sie k unayoifakamia ni bora kuliko Mtoto? Wengine mjifunze ukizaa na tuliooa jaribu kuwa mnafiki kwa bimkubwa na si ajabu ukampindua
 
Hizi zitakuwa story, angekuwa bahir hivyo asingekuwa anasafiri na msururu wa watu wote wale maana inamcost.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…