Kisutu: Mahakama yamhukumu Mfanyabiashara Herbinder Seth Kulipa fidia ya Tsh. 26.9 bilioni

Kisutu: Mahakama yamhukumu Mfanyabiashara Herbinder Seth Kulipa fidia ya Tsh. 26.9 bilioni

Ila hawa jamaa kama ni pesa walitupiga sana maana walikuwa wanalipwa capacity charge milioni 400 kila siku mitambo ifanye kazi au isifanye kazi pesa inaingia, ila wao kulipa faini kidogo tu waachiwe hawataki.
 
DPP Sylvester Mwakitalu leo amemuachia huru mfanyabiashara Herbinder Seth baada ya kukiri makosa na kulipa faini.

Mzee Ruge bado amekomaa, tusubiri tuone nini kinaendelea.

Source: Darmpya Blog
Yapo wapi!
 
Watafungua kesi,

Watashinda ,

Watalipwa na Richmond nyingine ipo mbioni.
 

Leo 16/06/2021 12:45
Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania (DPP), Sylvester Mwakitalu amesema, mfanyabishara Herbinder Seth anayekabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi, amekubali na kukiri makosa na kulipa faini na leo kama atakamilisha utaratibu ataachiwa huru na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Wakati hapo Jana mahakamani alitokea Seth peke yake je kila mmoja ana msimamo wake? Tusubiri leo baadae
👇🏽👇🏽👇🏽👇🏽
15/06/2021
Serikali yaafiki maombi majadiliano na Seth

Dar es Salaam. Upande wa mashtaka katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mtendaji wa PAP, Harbinder Seth, umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa wamepitia barua iliyoandikwa na mshtakiwa huyo na kufikia makubaliano kwa kile alichokiomba. Seth aliandika barua hiyo Juni 10, kwenda kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), akiomba kukiri mashtaka yake na kupunguziwa adhabu.

Barua hiyo ilijadiliwa kwa siku mbili na upande wa mashtaka na ule wa utetezi na kisha kutolewa mrejesho.

Wakili wa Serikali Mkuu, Marterus Marandu akisaidiana na Ladslaus Komanya jana alitoa maelezo hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.

Wakili Marandu alitoa maelezo hayo wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya upande wa mashtaka kuwasilisha mrejesho wa kile walichozungumza kati yao na Seth kwa ajili ya kuimaliza kesi hiyo.

“Kesi imekuja kwa ajili ya kutoa mrejesho wa barua iliyoandikwa na mshtakiwa huyu (Seth), niseme barua tumeshazipitia kwa pamoja na tumefikia mahali pa kukubaliana kuhusu kile ambacho mshtakiwa alikuwa anakiomba na baada ya hapo, tumekubaliana kuendelea na shauri hili,” alidai wakili Marandu na kuongeza:

“Kwa muktadha huo, upande wa utetezi kama hawatakuwa na pingamizi, naomba shauri hili lije mahakamani hapa kesho ( Juni 16) kwa ajili ya usikilizwaji,” alidai Marandu.

Baada ya kueleza hayo, Wakili wa Seth, Melchisedeck Lutema alikubaliana na maelezo ya upande wa mashtaka na kueleza kuwa huo ndio ukweli na ndio msimamo wa pande zote mbili za majadiliano waliyofanya.

Hakimu Shaidi baada ya kusikiliza maelezo ya pande zote alikubaliana na ombi hilo na kuahirisha kesi hadi Juni 16 itakapoitwa kwa ajili ya usikilizwaji au majadiliano ya kuimaliza kesi.

Hata hivyo, jana Seth alikuwepo mahakamani peke yake, wakati upande wa mashtaka walipowasilisha mrejesho huo.

Itakumbukwa Juni 10, Mahakama hiyo ilikubali upande wa mashtaka kufanya mazungumzo na mshtakiwa huyo ya kuimaliza kesi hiyo. Mahakama hiyo ilirihusu majadiliano hayo baada ya upande wa mashtaka kuwasilisha ombi mahakamani hapo la kutaka kufanya majadiliano na Seth na kisha kutoa mrejesho wa kile walichozungumza kwa ajili ya kuimaliza kesi.

Mbali na Seth, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ambao hawajaandika barua ya kukiri mashtaka yao kwa DPP ni aliyekuwa Mwanasheria wa kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), Joseph Makandege na Mkurugenzi wa VIP na mmiliki mwenza wa zamani wa kampuni ya IPTL, James Rugemalira.

Katika kesi ya msingi, Seth na wenzake wanakabiliwa na mashtaka 12 likiwemo la kutakatisha fedha na kuisababisha Serikali hasara ya Dola za Marekani 22,198,544.60 na Sh 309,461,300,158.27.
Nani kuilipa Standard chartered Malaysia, ni Harbinder au awamu ya serekali zinazo kuja na interest kuongezeka.
 
Tukishamuachia ule mpunga wote alioupiga unarudi?maana kuna kesi standard charted walishinda kwenye mahakama ya kimataifa kuhusu haya ma mitambo ya IPTL au tuna muacha ende then tunawakamua wanaichi wakalipe deni?
Maana tusijekua tunafurahia jamaa kuachiwa then madeni tunakamuliwa sisi.
 
Singa singa intown....sasa ile mitambo pale pameota nyasi....yale ma HOF engines yatahitaji mpunga ww kutosha kuyaamsha na kuyawasha au kuyauza ... Kuna hatari ya kesi inakuja kati ya GOVT na SETH + RUGE na hichi ndicho yule jamaa alikikwepa akaamua kuwahifadhi akiamini kwa mateso na kukosa uhuru natural death itasema nao...
We unadhani waliemuachia Ni wajinga Kama wewe??!
 
Back
Top Bottom