Kisutu: Matapeli 12 wanaotuma Meseji za kitapeli kwenye simu, Wapandishwa Kizimbani

Huu mtwndao, lazima unashirikiana na watu wanaofanya kazi kwenye mitandao ya simu,kwenye data centres/cloud,

Pale data centre, una uwezo, wa, kusikiliza mazungumzo ya mtu, kusoma SMS zake, kuangalia mihamara yake,
Haiwezekqni, kila ni kiweka pesa, kwenye simu, dk hiyo hiyo, sms za tuma kwrnye namba hii, au mimi mwenye nyumba wako tuma hapa,

Juzi nikawa naongea na mwenye nyumba kwa simu, kuhusu pesa ya umeme nitoe kwa namba IPI,

Tunamaliza maongezi, dk 30,inaingia SMS, mimi mwenye nyumba, mbona kimya sana!

Hawa kenge inawezekana hata kudukua maongezi, wanafsnya
 
wanatumia hiyo, bulk sms machine, ina sehem za kuweka line mpaka 32
una unga na pc, kuna software ina generate namba za simu, na kutuma SMS uliyo compose (ni mwendo wa jiwe gizani)
namba iwe valid isiwe, chuma kinaenda
Ngoja waendelee kutusumbua mm nikimdaka nafanya kama alichofanyiwa yule jamaa aliefumaniwa
 
achani ufala hawa jamaa ni trained person na kuna vyuo vyao ambavyo wanafundshana ile we wa nje huwez kujua mpaka ujiunge , hawa jamaa mtaji wao mkubwa ni namba na ukitumiwa txt ujue huyo mtu anakufaham ila hiyo namba yako kuna mtu amempa ambaye anajua taarifa zako vizuri make m mweny nmetestiwa kama x2 nilishangaa mtu cmjui ila yeye ananijua kama vile tulishawah kukutana kabla cha kushangaza mkoa wak na mi nilipo vitu viwil tofaut kwhy ucjichange kusema mipango yako binafsi kwa watu
 
Lazima wajue kuwa kuna wapangaji wengine wanashindwa kulipa kodi on time.

Wanajua kuwa vyovyote vile lazima kutakuwa na wagonjwa tu.

Akili zako ni Sawa na za waganga wa kienyeji na walokole
Huko nyuma haukua hivi!! Sijui nani amekuroga Mmawia
 
Wakazi 12 wa Ifakara mkoani Morogoro, akiwemo Noel Mboyo (37) maarufu kama Mkono wa Chuma, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na mashtaka 32 yakiwemo ya kusambaza ujumbe mfupi kwa njia ya mtandao wakitaka fedha, kuongoza genge la uhalifu, kujipatia Sh 10 milioni kwa njia ya udanganyifu na kutakatisha fedha hizo.

Washtakiwa hao ni Barnaba Gidajuri (45), Rahimu Sangila (20), Ramadhan Mcheni (28), Leonard Mwilenga (23), Mohamed Masalanga (24), Festo Ndizi (27), Richard Masunga (23), Zabron Mkoi (22).

Wengine ni Shafii Mtambo (18), Mussa Lwena (23) na Agrey Razaki (23) ambao wote kwa pamoja wamefikishwa mahakamani hapo leo Mei 28, 2024 na kusomewa kesi ya uhujumu uchumi namba 14185/2024.

Washtakiwa hao wamesomewa mashtaka yao na wakili wa Serikali, Tumaini Mafuru, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Ushindi Swallo.

Katika mashtaka 32 yanayowakabili washtakiwa; mashtaka 20 ni ya kutuma ujumbe mfupi wa sms kwa watu mbalimbali wakitaka fedha; saba ni ya kusambaza ujumbe mfupi wa sms kwa njia ya mtandano; mashtaka mawili ya kujipatia fedha; shtaka moja ni kuongoza genge la uhalifu na jingine ni kutakatisha fedha.

Kabla ya kusomewa mashtaka yao, Hakimu Swallo amesema washtakiwa hawatakiwi kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo.
 
Kuna wale wanaopiga simu wakidai ni wa makao makuu ya mtandao wa simu wakisema wametuma hela imeingia kwako,
 
Pamoja na kesi nyingine lakini wana kesi ya kutakatisha.
Hiyo ndiyo kesi ya kweli kuliko hata huo utapeli.
Wataoza jela bila dhamana.
Wataijua jela
 
"MIMI MWENYE NYUMBA WAKO APA MBONA SIKU ZINAZIDI?" 12 WAFIKISHWA MAHAKAMANI, WAKABILIWA MASHTAKA 32.

Na. Jeshi la Polisi, Dar es Salaam, Mei 28, 2024

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imewapandisha kizimbani wakazi 12 wa Ifakara, Morogoro akiwemo Barnaba Gidajuri (45) wakikabiliwa na mashtaka ya kuongoza genge la uhalifu na kujipatia pesa shilingi millioni 10 kwa njia ya udanganyifu.

Jana Mei 27, 2024 wakiwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo Ushindi Swalo, Wakili wa Serikali Tumaini Mafuru alidai watuhumiwa hao wanakabiliwa na mashtaka thelathini na mbili.
Wakili Mafuru alidai mashtaka hayo ni kuongoza genge la uhalifu waliofanya Januari mosi hadi Mei 5, 2024, ambapo walituma jumbe fupi kwa watu kisha kujipatia kiasi cha Sh millioni 10.

Aidha Wakili Mafuru alidai mashtaka ya pili na ya tatu yanayomkabili mtuhumiwa Barnaba Gidajuri ilitotenda Januari 4, mwaka huu akisambaza jumbe fupi kwa njia ya mtandao wenye maneno "Mzee huyu Mganga wa tiba asili anatoka mali bila kafara, cheo, mapenzi......".."jiunge na chama huru cha freemason (666) Tanzania bila kutoa kafara ya binadamu....."

Kwa mujibu wa Wakili mashtaka mengine manne yanayomkabili Barnaba ambapo akiwa Mkoa wa Morogoro mshtakiwa alitumia laini za simu zilizosajiliwa kwa majina tofauti bila ruhusa na idhini ya wamiliki.

Aliendelea kudai kuwa mashtaka ya nane yanayomkabili mtuhumiwa huyo alitenda Mei 11, 2024 kwa kujipatia shilingi 105,000 kutoka kwa Maria Nangwa baada ya kujitambulisha kuwa ni Mganga atakayemtibia ugonjwa wake wa kifafa.
Mahakamani hapo Wakili alidai mashtaka tisa na kumi yanayomkabili mtuhumiwa Rahim Bangila (26), kwa kusambaza jumbe fupi kwa njia ya mtandao wenye maneno."Mimi mwenye nyumba wako apa mbona siku zinazidi?"
Wakili Mafuru alidai mtuhumiwa Rahim anakabiliwa ni mashtaka matatu kwa kutumia laini za simu zilizosajiliwa kwa majina ya Valence Mandaki, Nundu Gulenya na Stephen Lihami bila ruhusa ya watu hao.

Aidha, Wakili alidai mtuhumiwa mwingine Ramadhan Mcheni (28) anakabiliwa na mashtaka mengine mawili ya kutumia laini za simu zilizosajiliwa kwa majina ya watu wengine bila ruhusa yao.
Ilidaiwa Mahakamani hapo mashataka mengine mawili yanayomkabili mtuhumiwa Leonard Mwilenga (23), ambapo Mei 6, mwaka huu alitumia laini za simu zilizosajiliwa kwa majina ya watu wengine bila ruhusa yao.

Hata hivyo, Wakili aliendelea kudai Mashtaka mawili mengine yanamkabili mtuhumiwa Mohamed Masalanga (24), ambaye alitumia laini ya Irene Said bila idhini yake.

Aidha mashtaka mengine ni kusambaza jumbe fupi tofauti kwa njia ya mtandao na kujipatia kiasi cha shilingi 389,000 benki ya CRDB kwenda kwa Odilia Mathew kinyume na sheria"habari ya leo mimi mwenye nyumba wako mbona kimya na siku zinaenda?".....umepokea kiasi cha shilingi.....", pia kutumia laini yenye usajili wa mtu mwingine bila idhini yao.

Pia mashtaka mengine yanamkabili mtuhumiwa Noel Noel Mboya (37) Mkono wa chuma, ni kosa la kuharibu na kupoteza ushahidi kwa kuharibu simu aina ya Tecno na kupoteza uhalisia wa simu hiyo na kufanya ushahidi usionekane.

Wakili alidai mashtaka mengine yanayowakabili washtakiwa ni kujipatia pesa shilingi milioni 10 kwa njia ya udanyanyifu kutoka kwa watu tofauti kuwa pesa hizo zimetumwa kimakosa katika simu zao hivyo zirudishwe.

Katika mashtaka ya mwisho washtakiwa wote kwa pamoja anashtakiwa kwa kosa la utakatishaji fedha, ilidaiwa kuwa washtakiwa walijipatia Sh millioni10 wakijua pesa hizo ni madharia ya mashtaka ya kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu.

Baada ya kusomewa mashtaka yao washtakiwa hakutakiwa kujibu kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kusikiliza shauri hilo. Washtakiwa walirudishwa rumande kutokana kesi yao kutokuwa na dhamana.

Kesi hiyo ilihairishwa hadi June11, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa na upelelezi wa kesi bado unaendelea.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Rahim Bangila ( 20), Ramadhan Mcheni (28, Leonard Mwilenga (23), Mohamed Masalanga (24), Festo Ndizi(27), Richard Masunga (23), Zabron Mkoi (22), Noel Mboya@mkono wa chuma(37), Shafii Mtambo (18), Musa Lwena(23) na Agrey Razaki (23) wote wakiwa ni wakazi wa Ifakara Morogoro.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Mei 15, mwaka huu na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, ilisema watuhumiwa hao walikuwa wakipiga simu na kusambaza jumbe fupi za maneno (sms) wakidai pesa inatumwa kimakosa hivyo irudishwe, wengine wanadai kusafisha nyota, ilikupata utajiri......, wengine kujifanya Maofisa wa Serikali kwa kudai kwamba watatatua shida za watumishi wenye matatizo na mwisho huishia kuwaibia watu pesa kwa njia ya mtandao.

Katika msako huo Jeshi la Polisi lilifanikiwa kuwakamata washtakiwa wakiwa na simu 41 na laini za simu 88 za mitandao tofauti zikiwa na usajili tofauti tofauti.

Pia soma
Tuwe makini na matapeli wa "ile pesa tuma kwenye hii namba". Ni kama vile wanapata taarifa tunapofanya miamala

Kuna shida ya kupambana na matapeli mitandaoni
Jina litakuja Bamptipita Malalula
 
haooo cha mtoto kuna mapapa waoooo wanakuja mahakaman na kuwatoa haya mambo hayaishi
Hamna cha mapapa. Hujui kitu mwana kubeti mwenzangu. Ifakara hawa wapo sehemu kuna bonde la mto. Unawakuta vijana wadogo zaidi ya mia. Wanavaa smart, hao wamechoka kukaa mahabusu. Ukiwakuta kule wako smart, kaazi ni moja kupiga simu na kuandika msg. Line zipo nyingi kama karata za kamali zinavyotupwa.
Hamna papa wala nini, hiyo ni individual hustle. Na hela wanapata kweli. Nilifurahi sana kuona ile doria January kuwakamata hawa vijana. Hawa hawaibi wala kukaba. Ila simu tu wanaweza itumia.
 
Binafsi naonatofauti kwa ifakara nimjiwenye matapeliwengisana kunakipindi walikamatwakamamia semanini shidayahuu mji haunavuwanda naidadiyawatu niwengi binafsi ningeiomba serekari ijengeata viwandaviwili vikubwa pale iiliwatuwapate ajila lakinikwakutumia bguvuynaweza ukakutanusu yawakaziwa ifakara.nimatapeli
 
"MIMI MWENYE NYUMBA WAKO APA MBONA SIKU ZINAZIDI?" 12 WAFIKISHWA MAHAKAMANI, WAKABILIWA MASHTAKA 32.

Na. Jeshi la Polisi, Dar es Salaam, Mei 28, 2024

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imewapandisha kizimbani wakazi 12 wa Ifakara, Morogoro akiwemo Barnaba Gidajuri (45) wakikabiliwa na mashtaka ya kuongoza genge la uhalifu na kujipatia pesa shilingi millioni 10 kwa njia ya udanganyifu.

Jana Mei 27, 2024 wakiwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo Ushindi Swalo, Wakili wa Serikali Tumaini Mafuru alidai watuhumiwa hao wanakabiliwa na mashtaka thelathini na mbili.
Wakili Mafuru alidai mashtaka hayo ni kuongoza genge la uhalifu waliofanya Januari mosi hadi Mei 5, 2024, ambapo walituma jumbe fupi kwa watu kisha kujipatia kiasi cha Sh millioni 10.

Aidha Wakili Mafuru alidai mashtaka ya pili na ya tatu yanayomkabili mtuhumiwa Barnaba Gidajuri ilitotenda Januari 4, mwaka huu akisambaza jumbe fupi kwa njia ya mtandao wenye maneno "Mzee huyu Mganga wa tiba asili anatoka mali bila kafara, cheo, mapenzi......".."jiunge na chama huru cha freemason (666) Tanzania bila kutoa kafara ya binadamu....."

Kwa mujibu wa Wakili mashtaka mengine manne yanayomkabili Barnaba ambapo akiwa Mkoa wa Morogoro mshtakiwa alitumia laini za simu zilizosajiliwa kwa majina tofauti bila ruhusa na idhini ya wamiliki.

Aliendelea kudai kuwa mashtaka ya nane yanayomkabili mtuhumiwa huyo alitenda Mei 11, 2024 kwa kujipatia shilingi 105,000 kutoka kwa Maria Nangwa baada ya kujitambulisha kuwa ni Mganga atakayemtibia ugonjwa wake wa kifafa.
Mahakamani hapo Wakili alidai mashtaka tisa na kumi yanayomkabili mtuhumiwa Rahim Bangila (26), kwa kusambaza jumbe fupi kwa njia ya mtandao wenye maneno."Mimi mwenye nyumba wako apa mbona siku zinazidi?"
Wakili Mafuru alidai mtuhumiwa Rahim anakabiliwa ni mashtaka matatu kwa kutumia laini za simu zilizosajiliwa kwa majina ya Valence Mandaki, Nundu Gulenya na Stephen Lihami bila ruhusa ya watu hao.

Aidha, Wakili alidai mtuhumiwa mwingine Ramadhan Mcheni (28) anakabiliwa na mashtaka mengine mawili ya kutumia laini za simu zilizosajiliwa kwa majina ya watu wengine bila ruhusa yao.
Ilidaiwa Mahakamani hapo mashataka mengine mawili yanayomkabili mtuhumiwa Leonard Mwilenga (23), ambapo Mei 6, mwaka huu alitumia laini za simu zilizosajiliwa kwa majina ya watu wengine bila ruhusa yao.

Hata hivyo, Wakili aliendelea kudai Mashtaka mawili mengine yanamkabili mtuhumiwa Mohamed Masalanga (24), ambaye alitumia laini ya Irene Said bila idhini yake.

Aidha mashtaka mengine ni kusambaza jumbe fupi tofauti kwa njia ya mtandao na kujipatia kiasi cha shilingi 389,000 benki ya CRDB kwenda kwa Odilia Mathew kinyume na sheria"habari ya leo mimi mwenye nyumba wako mbona kimya na siku zinaenda?".....umepokea kiasi cha shilingi.....", pia kutumia laini yenye usajili wa mtu mwingine bila idhini yao.

Pia mashtaka mengine yanamkabili mtuhumiwa Noel Noel Mboya (37) Mkono wa chuma, ni kosa la kuharibu na kupoteza ushahidi kwa kuharibu simu aina ya Tecno na kupoteza uhalisia wa simu hiyo na kufanya ushahidi usionekane.

Wakili alidai mashtaka mengine yanayowakabili washtakiwa ni kujipatia pesa shilingi milioni 10 kwa njia ya udanyanyifu kutoka kwa watu tofauti kuwa pesa hizo zimetumwa kimakosa katika simu zao hivyo zirudishwe.

Katika mashtaka ya mwisho washtakiwa wote kwa pamoja anashtakiwa kwa kosa la utakatishaji fedha, ilidaiwa kuwa washtakiwa walijipatia Sh millioni10 wakijua pesa hizo ni madharia ya mashtaka ya kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu.

Baada ya kusomewa mashtaka yao washtakiwa hakutakiwa kujibu kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kusikiliza shauri hilo. Washtakiwa walirudishwa rumande kutokana kesi yao kutokuwa na dhamana.

Kesi hiyo ilihairishwa hadi June11, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa na upelelezi wa kesi bado unaendelea.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Rahim Bangila ( 20), Ramadhan Mcheni (28, Leonard Mwilenga (23), Mohamed Masalanga (24), Festo Ndizi(27), Richard Masunga (23), Zabron Mkoi (22), Noel Mboya@mkono wa chuma(37), Shafii Mtambo (18), Musa Lwena(23) na Agrey Razaki (23) wote wakiwa ni wakazi wa Ifakara Morogoro.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Mei 15, mwaka huu na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, ilisema watuhumiwa hao walikuwa wakipiga simu na kusambaza jumbe fupi za maneno (sms) wakidai pesa inatumwa kimakosa hivyo irudishwe, wengine wanadai kusafisha nyota, ilikupata utajiri......, wengine kujifanya Maofisa wa Serikali kwa kudai kwamba watatatua shida za watumishi wenye matatizo na mwisho huishia kuwaibia watu pesa kwa njia ya mtandao.

Katika msako huo Jeshi la Polisi lilifanikiwa kuwakamata washtakiwa wakiwa na simu 41 na laini za simu 88 za mitandao tofauti zikiwa na usajili tofauti tofauti.

Pia soma
Tuwe makini na matapeli wa "ile pesa tuma kwenye hii namba". Ni kama vile wanapata taarifa tunapofanya miamala

Kuna shida ya kupambana na matapeli mitandaoni
Kuna rai moja wacha niwapatie ukipigia number ngeni yoyote na mtu usiemjua kama umeipokea zungumza nae kiengereza tu ,lazima ataanza kubabaika jifanye hujui kabisa kiswahili.
 
iyo hela nitumie kwenye hii AirtelMoney 0780879536 jina litoke. RAMADHANI OMARY NGOLO.
 
Back
Top Bottom