Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wikipedia hata Mtoto wa chekechea anaweza kuweka data ama kuedit hivyo reference yako haiwezi kuwa sahihiWasomaji JF, please as time goes on jari9bu kum ignore Pascal!
Ikulu
Description
The White House, also known in English as the State House, is an official residence and workplace of the President of the United Republic of Tanzania. Wikipedia
Ajabu huo mti wenye matunda umejificha,sasa sijui utapigwaje mawe wakati hauonekani!Kaka Pascal Mayalla kuongoza hawa viumbe wa leo ni kazi sana maana kila utakachakifanya watainuka kukupinga. Na pia kumbuka mti wenye matunda ndio huo unaopigwa mawe
Kama una akili safi huwezi kusema habari ya kukomboa uchumi wakati waGONJWA wamejaa Magufuli hostel , Uwanja wa sabasaba ndio quarantine centre.
Umekurupuka brother. Think twice before you comment brother. Kwa sasa kuna lundo kubwa la wafanyakazi ktk sekta binafsi wanaachishwa kazi kwa sababu ya huu ugojwa wa korona. Waajiri wengi wanasingizia kuyumba kiuchumi. Haya hili jambo limeshughulikiwaje? au serikali ipo tayari kuona watu wanakufa kwa janga la njaa na korona? Angalia Rais wa SA ameitaka serikali yake ipunguze kodi kwa makampuni mbalimbali hili lina maana kubwa sana kwa makampuni kwa sababu ile hela ambayo ingetumika kulipa kodi wataitumia kuwalipa wafanyakazi wao na hao wafanyakazi watalipa indirect tax kwa namna moja au nyingine na maisha yatasonga mbele.
Makonda mwenywe KWA KINYWA CHAKE amesema kuwa WATU WASIJE DAR MAANA DAR WATU WANAPUKUTIKA!
Mbali na kupukutika kwa huu ugonjwa wa korona, watu watakufa kwa sababu ya hali mbaya ya kiuchumi.
Alitakiwa kuwa mstari wa mbele kuongoza maombi!!Magufuli bwana. Anasema Corona ni ka ugonjwa kadogo tu, tumuombe Mungu, sasa yeye mbona amekimbilia Chato???
Ana imani haba. Aje Dar tuombe pamoja na tupige kazi pamoja.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kwani ameenda South Africa???Hoja ni Kukimbia kipindi cha kupambana tulitarajia awe mstari wa mbele vitani....ANgeenda CHATTLE Nov 2019 tusingemtafuta ila kakimbia baada ya kuona covid19 anasepa na kijiji cha DSM.
Pale Mikocheni kwa Mwalimu ni Mali UA Serikali??? Au Mwitogo Kule Butiama nako pia??? Mbona alipatumia kuongoza nchi na mambo yakaenda Sawa? Acheni upotoshaji Mkuu wa Nchi Huko na Kazi zinaenda. Mnaomtaka mna yenu na hamtafanikiwaPaskali umetoa mifano ya ikulu nyingine hapa TZ jee hizo ni mali binafsi au za uma? rais ajaye ataweza kwenda kufanyia majukumu yake Chato? Kwa maana fupi unataka kila rais ajenge international airport kijijini kwake na ikulu yake. Lakini kumbuka watangulizi wa awamu nyingine hakuna aliyefanya hivyo
Wikipedia hata Mtoto wa chekechea anaweza kuweka data ama kuedit hivyo reference yako haiwezi kuwa sahihi
Nimesoma nakubaliana na wewe kuwa Rais anaweza timiza majukumu yake akiwa popote lakini jambo muhimu na la msingi ni kuwa waliosema hapa ndio ikulu ya Rais hawakua wajinga kwa kuamua hivyo walitazama vitu vingi sana,Moja security,ufanisi na mpangilio mzuri wa rekodi kwa kua nyaraka muhimu na za nchi haziwezi kaa nyumbani kwa rais hivyo ndio maana kuna ofisi ya rais,accessibility yake kwa yeye ndiye kiongozi mkuu ni lazima kwa muda mwingi wa kazi awe ofisi kuu kwa majukumu ,maana haiwezekani leo uwe Dar,kesho Dodoma,kesho kutwa Njombe inawezekana but for specific reasons kama likizo hivyo nilitegemea useme Rais yuko likizo au ziara but kukaa bila sababu ni kuongeza gharama kuendesha serikali very possible kuona gari inajazwa confidential document moja kupeleka nyumbani kwa rais kusainiwa na kurudishwa ofisini.Wanabodi,
Kiukweli baadhi ya Watanzania ni walalamishi mpaka basi, baada ya rais Magufuli kushinda urais wa Tanzania katika uchaguzi huru, wa haki na wa kidemokrasia, na serikali ikaamua kujenga uwanja wa ndege Chato, kuna watu humu walipinga sana ujenzi wa uwanja huo, mimi ni miongoni mwa wachache tuliounga mkono ujenzi wa uwanja huo
Naunga Mkono Uwanja wa Ndege wa Chato, Una Justification, Utakuwa kama Ggabolite, au Yamoussoukro, Watalii Watamiminika! - JamiiForums
Sasa rais Magufuli yuko Chato, watu humu wanaanza tena kupiga kelele, kwanini rais yuko Chato muda mrefu?.
Japo Kiswahili ndio lugha yetu ya taifa, lakini kiukweli Kiswahili ni kigumu hata kwa baadhi ya Waswahili wenyewe, hivyo kwa vile ni mmoja wa Watanzania tuliobahatika kuzaliwa mjini, kukulia mjini, kusomea mjini na sasa tunaishi mjini, Kiswahili ndio lugha yetu kuu, tunakimanya vilivyo.
Wengi wasiojua Kiswahili barabara, wanadhani Ikulu ni eneo rasmi specific la makazi ya rais kuishi na kufanyia shughuli zake kama ilivyo Ikulu ya Magogoni au Ikulu ya Chamwino, kumaanisha rais asipokuwa Ikulu ya Magogoni au Chamwino, akiwa pengine popote, anakuwa hayuko kazini, hivyo huku kwenye mitandao ya kijamii sasa kuna kelele za watu kutaka kulazimisha lazima wamuone rais Magufuli na kumsikia akitokea ama Ikulu ya Magogoni, au Ikulu ya Chamwino.
Ikulu sio eneo lolote specific, bali eneo lolote la makazi rasmi ya rais ambapo anaweza kutimiza majukumu yake ya urais, hivyo kwa Tanzania tuna ikulu ya Magogoni, Ikulu ya Chamwino, Ikulu ndogo ya Lushoto na karibu kila mkoa kuna Ikulu ndogo kama ya Arusha, Tanga, Morogoro, Mishi, Iringa, etc.
Enzi za Nyerere aliamua yeye hakai Ikulu bali aliishi Msasani, kama angeamua kufanyia kazi zozote za urais hapo Msasani, then pangekuwa ni ikulu ya Msasani. Mwalimu Nyerere alikuwa anakwenda likizo Butiama, wakati akiwa Butiama, akiamua kufanya majukumu yoyote ya kirais, then hapo Butiama panakuwa ni Ikulu ya Butiama.
Kwa muda sasa rais Magufuli yuko kijijini kwake Chato, kwa vile huko Chato anatimiza majukumu yake yote ya urais, then hapo Chato ni ikulu ya Chato, as long as mambo yote yanakwenda, hizi kelele za watu kutaka kumuona rais Magufuli akiwa ikulu ya Magogoni au ikulu ya Chamwino za nini?.
Hii ni press release ya leo
View attachment 1426440
Hitimisho.
Watanzania wazalendo watapenda kumuona rais wao akitimiza majukumu yake ya urais akiwa popote na tungependa rais wetu awe free kukaa mahali popote anapopenda as long as it takes.
Kuna watu wenye akili fupi wanadhani uwepo wa rais Magufuli Chato ni kuikimbia Corona, it's not!, kwa sisi ambao ka Kolona ni kaugonjwa kadogo ambacho hakatishi na tusitishane, hatuwezi kukuambia ka Kolona!.
Tupunguzeni kulalamika!
Paskali
Rejea
Hongera Rais Magufuli kuipendezesha Ikulu yetu kuliko enzi za Nyerere, Ikulu iwe kivutio cha utalii, restrictions ziondolewe watalii wafurike - JamiiForums
Tusilalamike tuu, kulaumu na kulaani kila kitu, kwenye mazuri tupongeze! Rais Magufuli is changing for the better!. - JamiiForums
Tusikalie kumlaumu tu Rais Magufuli na Serikali yake wanapofanya mabaya, kwenye mazuri, pia tupongeze!. - JamiiForums
Paschal Mayalla: Acheni kulalamika, kubalini mafanikio ya Serikali - JamiiForums
Kwahiyo afadhali kulinda uchumi huku watu wakifa kwa maelfu a day? Nipe jibu kwanza kwa swali hilo! From there tutaongea maana tunajadili wala hakuna ugomvi!. Ecuador maiti zinaokotwa barabarani, tufike hapo?
Bodies are being left in the streets in an overwhelmed Ecuadorian city
Bodies are being left in the streets in an overwhelmed Ecuadorian city
Bodies Rotting in the Street: COVID-19 Chaos Grips Ecuador
Bodies Rotting in the Street: COVID-19 Chaos Grips Ecuador
Perfect, kumbe tuko pamoja! Nakubaliana na hoja yako by 100%Kwanza, mkuu hujaelewa hoja yangu. Hoja yangu ni kwamba wakati tunaendelea kupambana na huu ugonjwa wa korona serikali inabidi ije na strategic plan ya kuhakikisha uchumi nao hauteteleki sana maana uchumi ukiteteleka hali itazidi kuwa mbaya sana kwa wananchi.
Pili, primary responsibility ya serikali ni kulinda wananchi wake. Lakini serikali ilipokubushwa kufanya jitahanda za kuhakikisha tunapambana ipasavyo na hili gonjwa walipuuzia na ndiyo maana leo hii hali inazidi kuwa mbaya.
Mbali na kuhimiza maombi wana mpango gani wa kimkakati wa kupambana na hili gonjwa? Hakuna njia yoyote madhubuti ya kuhakikisha hili gonjwa halienei nchini. Kwanza ndiyo wanazidi kumwaga petrol kwenye moto(Kuhimiza mikusanyiko).
☝️Jamani Serikali ya CCM rejesheni tenda za matangazo mlizozisitisha kwa Pascal Mayalla