Kiswahili fasaha kinatoweka

Kiswahili fasaha kinatoweka

a e i o u,,hizi ni herufi kuu tamka kwa sauti kuu
 
Katika mchakato wa kusanifisha Lugha ya Kiswahili,Wakenya walipinga sana lahaja ya kiunguja kuwa ndo lahaja ya usanifu wa Kiswahili,nadhani kasumba hii ndo sababu wao kutumia lahaja zao hasa kilamu.
kiswahili fasaha kimebaki huko visiwani
 
Nadra ni uchache au mara chache.

Kinyume cha nadra ni aghalabu.

Aghalabu ni mara nyingi.
Hakuna nyingi qala kidogo.
Aghalabu ni aghalabu, asiyejuwa hatojuwa hata kulitumia kwake kwenye sentensi.

Kiarabu chake ni "ghalban" (غالباً).

Mimi naijuwa lugha kama lugha tu, siyo mkalimani.
 
Hakuna nyingi qala kidogo.
Aghalabu ni aghalabu, asiyejuwa hatojuwa hata kulitumia kwake kwenye sentensi.

Kiarabu chake ni "ghaliban".

Mimi naijuwa lugha kama lugha tu, siyo mkalimani.
Andika "ghaliban" KWA mwandishi ya kiarabu
 
Vyombo vya habari vinavyoongoza kutumia kiswahili fasaha ni ITV na Radio One.

Radio One walianzisha hadi kipindi cha Kiswahili asubuhi jumamosi, nadhani muasisi alikuwa Julius Nyaisangah (marehemu hivi sasa), akaja kukiendeleza kipindi Regina Mziwanda ambaye yupo BBC hivi sasa. Pia Regina aliendeleza hii hadi Clouds, ndio akarithi Mwihava ndio huwa unamsikia Mwihava akimuuliza muuliza maswali Oni Sigala.

Kuonyesha = kuonesha.

Kuonesha = kuona

Kuonyesha = kuonya.

Masaa = saa
‘Kuonyesha’ siyo sahihi?
 
Kwa mujibu wa nini?

Una kamusi ya Kiswahili hapo ulipo?
Hii inaitwa MNYUMBULIKO WA VITENZI.

Ukipitia masomo ya sarufi ya Kiswahili utaona namna ambavyo VITENZI VINANYUMBULISHWA.

...ili kujua usahihi wa Kitenzi, lazima uangalie MZIZI WAKE katika mnyumbuliko wake.

Yaani:-

On-A

On-EKANA

On-WA

Ali-ON-ekana

Ali-ON-a

ON-esha

ON-eshana .... nk

Mzizi wa KITENZI ni "ON" na sio "ONY".
 
The same goes with every other languages in the world, sio kiswahili tuu, ukienda uingereza watakwambia hivohivo vijana wanaharibu lugha, ukienda ufaransa utaambiwa hivohivo, hata ujerumani. Kiswahili kimeundwa na lugha mbalimbali kama lugha zote hapa duniani, lugha hubadilika kadri binadamu anayetumia hio lugha anavobadilika, sio jambo la ajabu.

Hata mwenyew nachukizwa ila naumia kimyakimya.
 
Halimaanishi kwa wingi wala kwa uchache.

Aghalabu ni aghalabu.
Madam, tusaidie kwa kuandika sentensi ukitumia neno hilo 'aghalabu'. Tafadhali, i kwani wengi tunalitumia vibaya
 
Hii inaitwa MNYUMBULIKO WA VITENZI.

Ukipitia masomo ya sarufi ya Kiswahili utaona namna ambavyo VITENZI VINANYUMBULISHWA.

...ili kujua usahihi wa Kitenzi, lazima uangalie MZIZI WAKE katika mnyumbuliko wake.

Yaani:-

On-A

On-EKANA

On-WA

Ali-ON-ekana

Ali-ON-a

ON-esha

ON-eshana .... nk

Mzizi wa KITENZI ni "ON" na sio "ONY".
Lakini kamusi si huandikwa na wataalamu wa lugha?

Ina maana wataalamu hao walikosea?

Na siyo kamusi moja tu. Za TUKI zinalo hilo neno ‘onyesha’.

Za Oxford zinalo hilo neno’onyesha’.

Wote hawa wamekosea?
 
Back
Top Bottom