Kiswahili fasaha kinatoweka

Kiswahili fasaha kinatoweka

si afadhali hata hiyo mifano uliyoonyesha,wewe angalia matumizi mabovu ya lugha waliyonayo asilimia 80 ya Watanzania,hivi Sasa hawaongei kiswahili sanifu,hasa kwenye matumizi ya viambishi
utakuta awe kiongozi wa nchi, Mwalimu,anayejiita mwanaharakati wa lugha, waandishi na watangazaji wa habari ni kuboronga na kubagaza kwa kwenda mbele
kiambishi Cha wakati uliopita kutumika kwa wakati uliopo
mambo kama

aliyepo badala ya aliye
aliyekuwepo badala ya aliyepo
iliyokuwepo badala ya iliyopo

yaani matumizi ya viambishi vya wakati uliopita kwa wakati uliopo yameshamiri kwa asilimia 80 ya Watanzania na inaonekana ni jambo la kawaida
kwa kweli kiswahili kipo Gizani
Yaani wewe ndio umenikoroga kabisa 🤯 Nlikuwaga simpendi mwalimu wangu wa kiswahili alikua anaitwa Sekule kwasababu ya kufinya. Yule mwalimu hapana jamani 🙌🏾 Hadi nimesikia maumivu ya vifinyo vyake upya. Basi na somo nkalichukia completely hata sikumbuki tena kiambishi ndio ki nini 😏
 
Sio vizuri kuwa na kaida katika lugha ya mazungumzo . Lugha sanifu inaweza kutumika katika maandishi na katika maandiko rasmi. Ukiongea Kama Kiswahili kinavyotakiwa kuandikwa utaongea Kama kingereza Cha watanzania they talk like a book Yani wazungu wanashangaa Sana😆 afu utakuta lijitu linajinasibu linajua kingereza kumbe linaongea lugha ya kiuandishi😆
Unataka kuhalalisha makosa.
Wimbo wangu kuita nyimbo yangu ni kosa kubwa iwe katika kuongea au kuandika.
 
Siwezi kubisha sana kwenye hili, lakini ukweli kabisa, mzizi sahihi wa Kitenzi ONA ni "ON".

Kutoka kwenye "ON" ndipo unapoweza kukinyumbua kitenzi kwenda kwenye muelekeo uutakao.

Kama ni lahaja sijui, na sijaelewa hii lahaja ya "ONYESHA" ni ya nchi gani au eneo lipi la kijografia!

Lakini pia, kabla na baada ya uhuru tulipitia mchakato wa USANIFISHAJI WA KISWAHILI ambapo lahaja zote za Kiswahili zilisawazishwa (standardized) tukapata lahaja ya sasa ya KISWAHILI SANIFU ambayo ilitolewa kwa kiasi kikubwa kutoka kwenye Kiunguja.

Hivyo, lahaja zingine zilififishwa na kutotambulika rasmi.

Na kwa ufahamu wangu usio na mashaka wala ubabaishaji, neno SANIFU ni ONESHA.

Hapa sasa nazungumza kama mtaalamu wa Lugha na sio Kanjanja. Tunaweza kubishana katika usahihi wa lugha na ndio utamu wa utaalamu. Kubishana na kukinzana.

Lakini pia ONYESHA linaweza kuwa sawa kwa hoja ulizozitoa. Lugha inapanuka na kukubalika kulingana na mazingira au mazoea.

Sipingi. Mimi nitaenda na ONESHA.
Wapemba nyanya huita tungule,kitambo nikatumwa na mama wa kipemba nikamnunulie tungule gengeni,nilizurura,nikarudi na jibu la hakuna tungule,bomba wanaita mfereji
 
Kwa utafiti wangu mdogo hakujawahi kutokea matumizi mabovu ya lugha ya kiswahili kama muda huu tulionao.

Kibaya zaidi hata baadhi ya vyombo vya habari vikubwa vinashiriki dhambi hii.

Maneno mazuri ya kiswahili yamepindishwa kiasi inaleta kichefuchefu hata kusikiliza. Hapa nitaweka baadhi ya maneno.

Alikuwa = alikua
Kwa hiyo = ko
Baadhi = baazi
kufanikiwa = kujipata
sasa = saivi
Ndio hivyo = ndoivo
Ndio nini = ndonini
serikali = serekali/selekale
yaani = yani
mtaa = kitaa/kitaani
kwa sababu = co

Pasipo kuchukuliwa hatua za makusudi lugha hii inaelekea kupotea.

Chanzo kikuu cha haya ni uholela wa vyombo vya habari hasa habari za mtandaoni.

Nashauri mambo makubwa mawili yafanyike kwa haraka.

Kuwe na takwa la lazima kwa waleta habari kwa jamii wote kuwa na ufaulu mzuri wa lugha hii

vyombo vya habari vyote yaani vya kawaida na mitandaoni lazima visajiliwe kwanza na mamlaka za kiserikali kabla ya kuanza kupeleka habari yoyote kwa jamii.

Tuungane pamoja kuinusuru tunu yetu kuu ya lugha ya kiswahili

Kitakusaidia nini hicho kiswahili fasaha ?

Lengo la lugha ni watu kuweza kuwasiliana na kuelewana hapo inatosha kabisa .
 
Sipo nyumbani sasa hivi. Nikirudi nitakuwekea picha ya ukurasa yenye neno ‘onyesha’ na fasıli yake toka kamusi tatu tofauti zilizochapiswa na taasisi tofauti.

Ni vigumu sana mimi kukubali kwamba, wataalamu tofauti wa lugha ya Kiswahili, kutoka taasisi tofauti tofauti, wote wakosee katika kuliweka hilo neno kwenye kamusi walizozichapisha na kuzihariri.

Uzuri wa hizi kamusi, huwa zinachapisha majina ya wataalamu waliohusika katika kuzitengeneza.

Nitakuwekea picha ya kurasa zenye majina yao.

Ni watu wenye shahada za juu za lugha ya Kiswahili. Ni watu waliofanya tafiti na kuandika juu ya lugha ya Kiswahili.

Kwa ufupi, ni wataalamu wa lugha ya Kiswahili. Hivyo, ni watu ambao wanatambulika kama mamlaka katika fani zao.

Wataalamu wa Kiswahili kutoka chuo kikuu cha Oxford, kutoka chuo kikuu cha Nairobi, kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam, wote hawa wakosee katika kuliweka kwenye kamusi hilo neno?

Au siku hizi kamusi siyo kitabu cha mamlaka na marejeo katika kutafuta fasili na maana za maneno?

Anyway, nitarudi na screenshots. Ngoja nimalizie kubeba boksi kwanza.
haya kumekucha wakuu
 
Back
Top Bottom