Kiswahili fasaha ni kipi?

Kiswahili fasaha ni kipi?

Ndio - ni conjuction
Nilikuwa naumwa ndio maana sikuja shule.
Hapa kiunganishi si ndio, bali ni ndiyo maana. Ndio au maana haiwezi kusimama yenyewe hapa kama kiunganishi.

Mfano mwingine ni kwa vile, ambapo kwa na vile kila moja binafsi hapa haiwezi kuwa kiunganishi.

NB: Ni makosa kusema ndio maana, kama ulivyotumia hapa. Ndiyo hurejelea hali, ambapo ngeli yake (I/Zi) hushurutisha upatanishi wa kisarufi wa ndiyo.

Nilikuwa naumwa. Hali hiyo ndiyo ilisababisha sikuja shule (au: Sababu hiyo ndiyo ilifanya sikuja shule.)
 
Hapa kiunganishi si ndio, bali ni ndiyo maana. Ndio au ndiyo haiwezi kusimama yenyewe kama kiunganishi.

NB: Ni makosa kusema ndio maana, kama ulivyotumia hapa. Ndiyo hurejelea hali, ambapo ngeli yake hushurutisha upatanishi wa kisarufi wa ndiyo.

Nilikuwa naumwa. Hali hiyo ndiyo ilisababisha sikuja shule (au: Sababu hiyo ndiyo ilifanya sikuja shule.)
asante mkuu kiswahili tunakiharibu sana sisi.
 
Yaani ukisema ''ndiye'' umebeba maana nzima ukimlenga mtu ...Nikiwa na maana ukijibu na neno ndiye haina haja ya kuweka tena yeye ...Ukisema ''ndio/ndiyo yeye'' sawa ni sawa na neno moja tu ''Ndiye'' kimaana .
Unaongea kinadharia zaidi. Lakini mambo uwanjani ni tofauti na uelewa wako.
 
Mko poa bila shaka

Kiswahili fasaha ni kipi au neno sahihi ni lipi

1. Ndiyo
Au
2. Ndio

Lipi neno sahihi
Ndio, kweli kabisa! Katika Kiswahili sanifu, hiyo ndiyo tofauti ya "ndiyo" na "ndio."

Ndio - Kukubali
Ndiyo - Kiunganishi (wakati mwingine huwa ndiye)

Ova
 
Ndio, kweli kabisa! Katika Kiswahili sanifu, hiyo ndiyo tofauti ya "ndiyo" na "ndio."

Ndio - Kukubali
Ndiyo - Kiunganishi (wakati mwingine huwa ndiye)

Ova
Ungekuwa unaweka na sentensi kabisa, ungeona jinsi unavyoenda kinyume nyume.

Ndiyo na ndio vyote vinakubali (vinaonesha uyakinifu), isipokuwa muktadha wa matumizi yao ni tofauti.

1. Huwezi kusema ndio nimekubali. Tunasema ndiyo, nimekubali.

2. Ndio hawa walijiunga na chama hivi karibuni. (sahihi)

3. Unaipenda JF - ndiyo au siyo? (Ni makosa kusema ndio au sio!)

NB: Kwa namna gani ndiyo hutumika kama kiunganishi?
 
Center na centre, ipi ni sahihi?

Color na colour, ipi ni sahihi?

Najua ni misamiati ya lugha tofauti. Ila, kuna sehemu nataka kuelekea na hayo maelezo ya utofauti wake….
 
Center na centre, ipi ni sahihi?

Color na colour, ipi ni sahihi?

Najua ni misamiati ya lugha tofauti. Ila, kuna sehemu nataka kuelekea na hayo maelezo ya utofauti wake….
Kuna American English (AmE) na British English (BrE). Color, honor, organization na center ni AmE
 
  • Thanks
Reactions: ywf
Kwa mbaali kama naelewa tofauti kati ya 'ndio' na 'ndiyo'.
1. Hawa ndio vijana wenye nguvu.
2. Ndiyo nakuja.
Kwa mifano hii, wataalam mtasema kama nimeelewa au bado
 
Back
Top Bottom