Kiswahili: Matumizi ya Herufi “L” na “R”

Kote, kwenye kutamka na kuandika.
Kwenye kuandika ni tatizo la shule. Kile kiswahili tunasoma shuleni ndiyo hutatua mambo hayo. Kwenye kuongea sina hakika sana maana wanaweza kutumia herufi hizo zote. Labda wanakuwa hawako familiar na hayo maneno hivyo hawajui ni herufi gani inahitajika.
 
Wewe shida yako siyo kushindwa kutamka au kutofautisha herufi ^ARA^ na ^ELO,^ bali tu unashindwa kutambua na kutofautisha maneno maneno yanayokaribiana kimuundo.
 
Kutamka na kuandika, vyote hivi ni kutofanya mazoezi ya kutosha ili kurekebisha, utotoni ama ukubwani.
 
Haroo...hii seredi nimeierewa sana wakuu.Naifuatiria huku nakunywa uji muraini.😝😝😝😝
 
Wewe shida yako siyo kushindwa kutamka au kutofautisha herufi ^ARA^ na ^ELO,^ bali tu unashindwa kutambua na kutofautisha maneno maneno yanayokaribiana kimuundo.
Upo sahihi kabisa, nimejaribu kuvuta picha ya maneno mengine ninayochanganya,

Inafika kipindi inabidi ni google...

No wonder kiswahili ndio somo nililokua nafeli zaidi.

Asante.
 
Swali hapa si geographical upbringing, bali makuzi. Je alifundishwa kutamka na kutofautisha hizo herufi!??? HIli ni suala litokanalo na kukosa mafunzo sahihi utotoni ama kutoweka juhudi za kurekebisha ukubwani.
Inawezekana kurekebisha lakini kujitahidi kurekebisha ukubwani unaweza geuka kituko. Kuna redio Mbeya inaitwa Dream Fm. Nafikiri wameambiwa watamke R inapotakiwa, ni kituko jinsi wanavyojitahidi waitamke. Mwisho wa siku hawavutii kuwasikiliza. Au msikilize Bahati Bukuku akijitahidi kutamka R
Kutamka na kuandika, vyote hivi ni kutofanya mazoezi ya kutosha ili kurekebisha, utotoni ama ukubwani.

Mbaya zaidi huwezi fanya mazoezi kama jamii inayokuzunguka/unaoongea nao kila siku hawana hiyo R au L. Labda upate kocha.
 
Huenda wanaonekana kituko kwa sababu wengi wanaowasikiliza tayari wameshazoea kuchanganya hizo herufi
 
Kwa nini kuna wanyakyusa wameishi maisha yao yote Dar es Salaam wanachanganya R na L halafu kuna Wanyakyusa wameishi maisha yao yote Mbeya na wanaweza kutofautisha hizo herufi?
Bado matatizo yanakuwa ya kabila ambalo linaathiri pia makuzi ndani ya familia. Twajifunza lugha kupitia wazazi, jamii zinazotuzunguka na elimu darasani. Wapo ambao ni wepesi wa kujifunza mambo mapya na kufuta ya zamani.

Lakini si ajabu ukienda Nyanda za juu ukawakuta watu wanaoweza kutofautisha R na L. Hawatakuwa wengi sana kama wale wasioweza kutofautisha. Mimi kabila nalichukulia kama pombe. Pombe ina madhara, lakini sio wote wanyao pombe watapata madhara. Lakini wengi wanaokunywa pombe wanaweza pata matatizo fulani ambayo yanaweza yakatokea hata usipokunywa pombe.
 
Hili suala la kabila nina mashaka nalo.
Kariba kila mkoa ukienda utakutana na watu wa asili wa eneo hilo wanaochanganya hizo herufi.
 

Four Language Skills:
1. Speaking
2. Writing
3. Listening
4. Reading
 
Juzi kuna mtu kajirecord anaimba "I lani lani lani to you, i lani to youuuuu", aliniharibia siku yangu walai, nilihisi kichefu chefu, pumzi ilibana nadhani nilipatwa na Panic attack, [emoji1][emoji1]

Kuna msanii mmoja mkubwa tu, ameshirikishwa wimbo naupenda sana lakini ikifika verse yake hua natamani nipeleke mbele, anasema "...wala Hakuniulumia..."

Tena mie naona bora anayeandika kuliko anayeongea, inachefua sana.

UDUNI WA ELIMU na KUIGA VISIVYOFAA.
 
Hapana. Sioni kama kuna lugha ambayo ni sahihi kuliko nyingine. Ukiona hivyo kiswahili si lugha yao ya asili. Wanaotumia R au L wako sahihi tu....hiyo ni free style
Wewe ndiyo umeongea ukweli,unajua kuna watu wanaojifanya walienda shule kusoma wanadhani wanajua kila kitu, mtu aweke R au L bado kama anaongea na mswahili mwenzie atamuelewa tu,sasa shida inakua wapi
 
Wewe utakua ni kijana mdogo sana mwenye kudhani kwenda chuo kikuu ni kumaliza yote,swala ni unamuelewa aliyeweka R au L katika sentensi au huelewi,jibu ni unaelewa sana,sasa tatizo ni nini
 
Ukija kwetu tunasema abali za saa izi si utakufa kabisa😀😀
 
Mtu anasema rotion badala ya lotion!
 
Saramareko
 
Wewe utakua ni kijana mdogo sana mwenye kudhani kwenda chuo kikuu ni kumaliza yote,swala ni unamuelewa aliyeweka R au L katika sentensi au huelewi,jibu ni unaelewa sana,sasa tatizo ni nini
Kama umeenda shule walau ya upili halafu uwe umeandaa insha kwa lugha ya malkia hizo R na L uwe unazibadilisha ndo utajua madhara ya unachokitetea. Mkienda shule na kupata zero ndo mnakuja kulalama mtaani. Ushawahi hata kuandika barua ya maombi ya kazi ukazibadikisha R na L ukaona matokeo yake? Usitetee ujinga hakuna mwalimu anaweza kukufundisha hivyo! Matamshi na kuandika ni vitu viwili tofauti. By the way umri wangu unahusianaje na hizo R na L? Assuption kwamba unapoandika huo upuuzi kwamba utaeleweka ni ujinga mwingine ambao unahitaji kwenda elimu ya watu wazima.
 
Sababu kubwa no kutokana na matamshi kwenye makabila yetu. Mfano kwa wenzetu Wakurya hutumia "r" badala ya "l" kama vile (chakura) badala ya chakula, wari badala ya wali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…