Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Watu wanaosema ulasimu badala ya urasimu, Dal es saram badala ya Dar es Salaam, ulojo badala ya urojo, talatibu badala ya taratibu na michanganyiko mingine kama hiyo huwa wana tatizo gani hasa?
Siku hizi karibuni sio tu kutamka maneno yenye L na R imekuwa changamoto kubwa bali hata kuandika nalo limekuwa tatizo kubwa. Unaweza kuta tangazo limeandikwa tunauza tofari badala ya tofali, kujigalagalaza bada ya kujigaragaza, mchere badala ya mchele n.k Hivi kama kutamka ni shida hata kuandika ambapo mtu unatumia muda mwingi kufikiri bado nako hakusaidii?!
Michanganyo hii kwa sasa imeshika kasi hadi kwa watangazaji kwenye vyombo vya habari. Unakuaje mtangazi kama huwezi kutamka maneno ya lugha yako kwa ufasaha?
Hili tatizo la kuchanganya L na R linatokana na nini na linatatuliwa vipi kwa watu walioweza kulitatua?