Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 21,470
- 40,593
Tatizo hili naona limekuwa kubwa sana kwenye matumizi ya kawaida na wakati mwingine hadi kwenye matumizi Rasmi ya Lugha yetu ya Kiswahili. Inanonesha kwamba watu wengi labda kutokana na Lugha zao za asili wanashindwa kabisa kutofautisha matumizi ya her " L " na " R " wakati wanafanya uandishi wa maandiko yao.
Mtu badala ya kuandika "Jaribu" yeye ataandika "Jalibu", au wengi wetu hatuwezi kuandika "Dharula" badala yake tunaandika "Dharura" na mengine mengi yanayohusisha matumizi ya herufi hizo mbili.
kingine ni kutokutumia "h" kwenye negation na kutumia vowel peke yake.. hii hua inanikera sana sababu ni kitu obvious sana
akwenda - hakwenda
akusema - hakusema
Kilaza anaelevusha waelevu,DHARULA=DHARURA
Zaabu= Dhahabu
Samani=Thamani
Ngombe=Ng`ombe
okonkwo jr miye siyo kilaza wa Lugha hii adhimu. Dharula ndiyo neno sahihi na wala siyo "dharura". Nikwambie tu wengine tulishiriki kwenye vita kati ya siye tuliokuwa tunadhani matumizi sahihi ya neno linalotakiwa kuashiria uelekeo ni "onyesha" na siyo "onesha" na wale waliokuwa wanaamini kinyume chake, bahati mbaya sana tulishindwa vita ile baada ya mapambano mengi sana. Kama una ushahidi kuwa neno sahihi ni DHARURA na siyo DHARULA basi uuweke hapa Jamvini.
Preta, bitimkongwe 42_007 nziriye Manyunchwi Zamaulid SaaMbovu Kaboom hii lugha ya Kiswahili tunaitumia kwa mazoea lakini wakati mwingine huwa tunaipotoa!! Nimeona brawn shao kaathiriwa labda na lugha yake ya asili badala ya kuandika "thamani" akaandika "dhamani" Tujifunze wote kwa pamoja!!