Kusema 'shikamoo' ni moja kati vitu vya awali kabisa ....
(1) Maana: Neno 'Shikamoo' maana yake nini? Kwa mfano mtu akikusalimia 'Umeamkaje?' .... yeye akijibu 'Marahaba' anakuwa anamaana gani?
(2) Nani anastahili shikamoo?: ...Lakini je heshima hii inapaswa kuzingatia nini? - umri/rika au madaraka ... Nafahamu pia watu wengi tu huwaamkia shikamoo wake wadogo wa baba zao...
(3) Inatolewa wakati gani/mara ngapi?...
(4) Makundi: Kama umekutana na watu wengi (labda zaidi ya wanne) na wengine wanastahili shikamoo na wengine hawastahili unatakiwa ufanye/useme nini? ...ukikutana na kundi la watoto...
(5) Sistahili shikamoo: Kuna nyakati mtu anakuamkia shikamoo, lakini unahisi hustahili (pengine anaekuamkia unahisi amekuzidi umri au mnalingana!), je unafanyaje? unaitikia? Kama nilivyosema hapo juu mara nyingine si rahisi kutambua mara moja umri/rika la mtu hasa kama unakutana nae kwa mara ya kwanza. Huwa najisikia vibaya ikitokea nimemwamkia mtu ambaye baadae nagundua kumbe ni mdogo sana kwangu.
Karibu jamvini tubadilishane mawazo, tuelimishane!