KISWAHILI: Naomba maana ya maneno haya...

KISWAHILI: Naomba maana ya maneno haya...

Ikungeta, Ikupilika, Ulingeta, Ulimboka, ???

Ikungeta= The one who looks after me

Ikupilika=The one who listens ( kupilika maana yake kusikia)

Ulingeta-( Please look after me) Kuketa means kuona

Ulimboka Tafadhali niokoe kupoka means kuokoa
 
Last edited:
Je unaelewa nini maana ya maneno haya, Ustaarabu na Utamaduni?

Kama nilivyofundishwa na mwalimu wangu Ustaarabu ni hali ya kuwa kama Muarabu (Uarabu) na Utamaduni hi hali ya kuhusiana na Medinna, kwa sababu enzi za zamani Medinna ndio ilikuwa kitovu cha utamaduni wa hali ya juu.

Je kuna mwingine ambaye ana mawazo tofauti?
 
Kusema 'shikamoo' ni moja kati vitu vya awali kabisa ambayo tunawafundisha watoto wetu (kwa wazungumzaji wa kiswahili). Pamoja na ukweli kwamba nimekulia kwenye utamaduni huo (na naundeleza kwa watoto wangu), lakini kuna mambo kadhaa yamekuwa yakinipa shida (na labda pengine wewe pia yanakupa shida) kuhusiana na amkizi (salamu) 'shikamoo'.

(1) Maana: Neno 'Shikamoo' maana yake nini? Kwa mfano mtu akikusalimia 'Umeamkaje?' na wewe ukajibu 'salama' naona inaeleweka. Sasa ninapomwambia mtu shikamoo nakua nimemwambia/nimemuuliza nini hasa? Na yeye akijibu 'Marahaba' anakuwa anamaana gani?

(2) Nani anastahili shikamoo?: Naelewa shikamoo inaashiria heshima kwa anaepewa. Lakini je heshima hii inapaswa kuzingatia nini? - umri/rika au madaraka (nafasi ya mtu kijamii) au kitu kingine? Kama inazingatia umri/rika je katika mazingira ambayo umekutana na mtu ambaye kwa kumtizama sura tu huwezi kubashiri umri (rika) wake unawezaje kufanya maamuzi ya kutoa/kutokutoa shikamoo? Je mtu inatakiwa akuzidi miaka mingapi ili umpe shikamoo? - Kwa mfano mimi huwa napata taabu kumuakia mtu aliyenizidi mwaka mmoja!. Nimewahi kuona pia watu wanawapa shikamoo watu ambao ni wadogo kiumri kuliko wao - kwa mfano watu wenye madaraka serikalini nk. Nafahamu pia watu wengi tu huwaamkia shikamoo wake wadogo wa baba zao (tuseme, baba yako kaoa mke wa pili au watatu ambaye ni mdogo kiumri kuliko wewe).

(3) Inatolewa wakati gani/mara ngapi? Binafsi huwa naitoa mara moja kwa siku (kama mtu nimemwakia asubuhi, nikikutana nae mchana sirudii tena kumuakia, nitampa salamu nyingine za kawaida), lakini nafahamu wapo watu wengine wanaitoa mara kadhaa kwa siku kwa mtu huyohuyo (kila akikutana nae!). Kipi ni sahihi? Binafsi mtu akiniamkia zaidi ya mara moja kwa siku huwa inanichosha!

(4) Makundi: Kama umekutana na watu wengi (labda zaidi ya wanne) na wengine wanastahili shikamoo na wengine hawastahili unatakiwa ufanye/useme nini? Kwa upande mwengine umekutana na watu wengi na wote wanastahili wakuamkie inakuwaje? Mara nyingi ukikutana na kundi la watoto, kila mmoja anataka akuamkie kivyake. hili wakati mwingine lina nipa shida (unaweza kutakiwa kusema marahaba mara 20! kama wato wapo ishirini).

(5) Sistahili shikamoo: Kuna nyakati mtu anakuamkia shikamoo, lakini unahisi hustahili (pengine anaekuamkia unahisi amekuzidi umri au mnalingana!), je unafanyaje? unaitikia? Kama nilivyosema hapo juu mara nyingine si rahisi kutambua mara moja umri/rika la mtu hasa kama unakutana nae kwa mara ya kwanza. Huwa najisikia vibaya ikitokea nimemwamkia mtu ambaye baadae nagundua kumbe ni mdogo sana kwangu.

Karibu jamvini tubadilishane mawazo, tuelimishane!
 
Kwa nilivyowahi kusikia(kama kumbukumbu yangu iko sawa) ni kuwa shikamoo ina maana "nipo chini ya miguu yako".
 
Kwa nilivyowahi kusikia(kama kumbukumbu yangu iko sawa) ni kuwa shikamoo ina maana "nipo chini ya miguu yako".

Inaweza kuwa na mwelekeo unaofanana na upigaji goti/magoti kwa baadhi ya makibila hapa Tz wakati wa kusalimiana?
 
Naam, niko chini ya miguu yako ndilo nami nimewahi kusikia kuwa linazaa neno shikamoo
Maelezo mengine yanayofanana na hilo ni;
anayesema shikamoo anakuwa akimwambia mhusika 'kwa heshima nakushika miguu'
mwambiwa hujibu marahaba akimaanisha maneno mawili;
MARA , HABA, yaaani nishike miguu ndio lakini fanya hivyo sio sana ila mara haba(chache) wengine husema 'mara saba'

Nidhamu hii ilitumika sana enzi za mabwana na watwana katika jamii, mtwana alipaswa kunyenyekea kila amwonapo bwana mkubwa.
 
Kwahiyo huyo muheshimiwa Kihiyo ilipothibitika kuwa amedanganya elimu yake alipigwa chini ubunge tu na hakupelekwa segerea kunyea ndoo?
Sasa kuna bwana Chitatilo naona taratibu ana take over and soon watanzania wenye ma doc ya kufoji wataitwa chitatilo!!
 
Kusema 'shikamoo' ni moja kati vitu vya awali kabisa ....

(1) Maana: Neno 'Shikamoo' maana yake nini? Kwa mfano mtu akikusalimia 'Umeamkaje?' .... yeye akijibu 'Marahaba' anakuwa anamaana gani?

(2) Nani anastahili shikamoo?: ...Lakini je heshima hii inapaswa kuzingatia nini? - umri/rika au madaraka ... Nafahamu pia watu wengi tu huwaamkia shikamoo wake wadogo wa baba zao...

(3) Inatolewa wakati gani/mara ngapi?...

(4) Makundi: Kama umekutana na watu wengi (labda zaidi ya wanne) na wengine wanastahili shikamoo na wengine hawastahili unatakiwa ufanye/useme nini? ...ukikutana na kundi la watoto...

(5) Sistahili shikamoo: Kuna nyakati mtu anakuamkia shikamoo, lakini unahisi hustahili (pengine anaekuamkia unahisi amekuzidi umri au mnalingana!), je unafanyaje? unaitikia? Kama nilivyosema hapo juu mara nyingine si rahisi kutambua mara moja umri/rika la mtu hasa kama unakutana nae kwa mara ya kwanza. Huwa najisikia vibaya ikitokea nimemwamkia mtu ambaye baadae nagundua kumbe ni mdogo sana kwangu.

Karibu jamvini tubadilishane mawazo, tuelimishane!

Ahsante sana ndugu yangu kwa maswali yako...

Kabla ya kujibu swaala lako, kwanza kabisa yakupasa ujuwe kuwa lugha ya Kiswahili ni mchanganyiko wa lugha mbali mbali za kimataifa, ikiongozwa na lugha ya Kiarabu, Kibantu, Kiajemi (Farsi) lugha ya Wairan, Kihindi, Ki'Portuguese na nyinginezo.

Neno "Shikamoo" Linatokana na asili ya neno la kiajemi... Likimaanisha mtu mwenye cheo (Bwanyenye). Kumbuka kwamba mabwanyenye wengi wa kipindi kile walikuwa wana maumbo Manene...! Na ilikuwa kumwambia mtu "Shikamoo kwa kipindi kile ilionekana ni heshima kwa kuukubali ubwanyenye wake... Yaani ubwana mkubwa.

Lugha ya kiswahili kama zilivyo lugha zingine nayo ikajikuta ikitohoa neno hili na kujikuta likitumika kama salamu, salamu ambayo humtoka mdogo kwenda kwa kubwa.

Wapo wanaotafsiri neno hili "Shikamoo kwa maana ya "Nipo Chini ya Miguu yako... wengine wanasema maana yake ni "Shika mkono...Hii si sahihi... Labda tu kwa kuwa enzi hiyo neno hilo lilikuwa likitumika sana toka kwa wasionacho kwenda kwa walionacho...! Na walionekana waliotoa heshima hii aidha wakiinama kwa kutaka kushika miguu au kwa kuinama kidogo... na kwa wanawake kupiga magoti.

Marahaba ni neno la lugha ya "Kiarabu" na linatokana na neno "Marhaba ( مرحبا ) maana yake ni Karibu au unakaribishwa ... Welcome... Ni sawa kumwambia mtu kuwa umekubali ile heshima aliyokupa... au uliyompa.

Na wakati mwingine unaweza kumsikia Mwenye kuzungumza Kiarabu akisema "Marhaba bikum" hapa anamaana ya "Karibuni nyote".

Nadhani swali namba moja nimelijibu kulingana na maelezo niliyo yatoa hapo juu...

Swali na "2" Mwenye kustahili heshima hii ni kwa wale wote unaowaheshimu sana. Aidha Baba, Babu, Mama, Bibi, Kaka, Dada... na kwa kila aliyekuzidi umri... Hapa Umri wengi wanachukulia kuanzia miaka mitano kwenda mbele (Sina uhakika sana) Ila yule ambaye angeweza kukubeba ulipokuwa mdogo.

Suala la Mama mdogo aliye olewa na Baba mzazi, hata kama umempita miaka kumi, unampa Heshima hii tu kwa kuwa ni mke wa baba... basi. Pia kwa baba aliye muoa mama hata kama umempita miaka.... Kwa ufupi ni kuonyesha heshima tu. Hii ni sawa na kumwamkia mtu (Haswa kule visiwani) Kwa kutumia neno chei chei.

Japokuwa ukitembelea maeneo ya bara kama kule musoma mimi binafsi nimeshuhudia Babu mtu mzima akimwamkia kijana au mjukuu wake... kwa kuwa tu si mzawa wa pale na hii salamu ilikuwa inaonekana ni ya waswahili...na jamaa zangu kule hawakuwa wakijuwa ni nani haswa anastahili kupewa hii Shikamoo...

Swali nambari "3" Inatolewa wakati gani/mara ngapi?...

Jibu lake kila ukiamka asubuhi... Na kila kikipita kipindi kimoja ambacho hamjaonana... Hapa nina maana... sisi tunao zungumza Kiswahili tumepanga mida yenu kwa mpangilio huu:

Asubuhi... Kuanzia Alfajiri mpaka mida ya saa tano karibia na saa sita

Adhuhuri yaani Mchana... Kuanzia saa sita mpaka saa tisa.

Alasiri kuanzia tiisa mpaka kumi na moja...

Magharibi Mida ya kuzama kwa juwa.

Na muda Usiku pale juwa linapokuwa lishazama.

Kwa mpangilio huu... kama inatokea kuto onana kutoka kwa kipindi kimoja au viwili basi wengine wanapendelea kuamkiwa kwa salamu hii ya Shikamoo.

Swali nambari "4" Kuamkia watu wazima (wakubwa kiumri) wengi waliochanganyika na vijana... Niliwahi kumsikia jamaa mmoja akisema hivi: "...Shikamooni wakubwa...! Wadogo Marhaba..." au "wadogo amjamboo" Sina uhakika sana na hii salamu. Labda wachanguaje wengine wanaweza kuchangia zaidi.

Ukikutana na kundi la watoto ni kuitikia tu... Marhaba... basi wala usichoke ndo watoto...

Matumani kidogo nitakuwa nimesaidia kwa kiwango fulani.
 
Hivi neno linakuwa rasmi mara baada tu ya jamii kulikubali na kulitumia kama neno rasmi kwenye vyombo vya habari, bunge?Au linakuwa rasmi mara baada ya Bakita kulipitisha na/au kuliingiza kwenye kamusi? Nauliza kwa kuwa Bakita wako legelege sana katika suala la kuingiza maneno mapya kwenye kamusi!
 
Ahsante sana X-Paster kwa uchambuzi wako. Kwa hakika umenifundisha mengi. Elimu kama hizi si rahisi kuzipata shuleni.
 
Haya ni maneno ya kupita tu, ikitokea sababu ya kupatikana neno jingine basi utaona hili la kihiyo ninapotea na kushika ukanda neno jingine.
 
Nakubali maelezo ya X-PASTER kuhusu "marahaba" ni sawa kabisa.

Lakini kuhusu "shikamoo" naomba aongeze maelezo. Ni neno la Kiajemi?? Neno lipi? Najua Kiajemi kidogo sijawahi kukuta neno hili. Labda ataje jinsi anavyojua nilitafuta kwenye kamusi. Menginevyo bado naona "shikamoo" kwa maana ya Kibantu "shika mguu" ni uwezekano mkubwa zaidi.
 
MATUMIZI YA NENO UFISADI YANANICHANGANYA.
SIELEWI TOFAUTI YA WIZI NA UFISADI.
WATU WENGI WANAJITAHIDI KUTUMIA NENO UFISADI KWA CHOCHOTE WASICHOKIPENDA.
NINI MAANA YA UFISADI HASA?
Exaud J. Makyao
 
Hapo nyuma nilianzisha thread under the heading '' wasaliti wa taifa'', nilichokieleza kinafanana kwa kiasi fulani na unachozungumzia hapa.

Baada ya kuona neno fisadi linatumiwa vibaya na kusababisha kushuka kwa uzito wake nikaona ni bora liwe linatumika jina ''wasaliti wa taifa'' badala ya mafisadi, jina ambalo kwa sasa nchini linatumika kuwaadress watanzania wote wenye privelage au achievement fulani legally or not!


Thread yenyewe inapatikana hapa: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/14683-wasaliti-wa-taifa.html
 
Maana halisi ya ufisadi ni kutapanya mali kwa fujo wakati wenzako hawana hata uhakika wa watakula nini kesho.
Ufisadi katika mapenzi ni kwa mwanamume kutotosheka na mwanamke mmoja, hata apate huduma mara tatu kwa siku kama dozi, bado atatembea na kuanzia house girl mpaka mashosti wa mkewe, na kila mtaa ana mwanamke. Huitwa fisadi kiwembe.
Matumizi ya neno fisadi yameelekezwa kwa watafunaji mali ya umma katika orodha ya mafisadi iliyoandaliwa na mwanasheria
Antipasy Tundu Lissu, aliyempa Katibu Mkuu wa Chadema, Dr. Wilbrod Slaa na kuitangaza katika mkutano maarufu wa Mwembeyanga.
Kufuatia orodha hiyo, sasa kila mwizi hata wa embe lililoanguka mtini ni fisadi. Kila mwenye gari zuri ni fisadi. Kila tajiri ambae haeleweki amepata wapi utajiri ni fisadi.
Fisadi ni jina la mtu. Ufisadi ni kitendo na kifisidi ni present tense ya ufisadi
 
Wazee nimekuwa nikiachwa kizani wakati wote neno hili linapotumika hivyo naombe mnifumbue macho tujadili hivi hiki ni kiswahili,kifaransa,kigogo am kimasai.
 
hilo neno linatokana na kifupi cha neno/maneno ya kifaransa-president directeur generale(pdg) yaan kwa tafsiri ya kiswahili sanifu ni mkurugenzi/meneja mkuu wa kampuni au shirika fulani
 
Kwa lugha ya mtaani,nisijue we ulishawai ishi wapi Daslaaam,pede ni mtu mwenye pesa hasiye na shule(hakwenda darasani),walenda mbali na kutolea mfano Papa Musofe,Jack Pemba...............na wengine wengi wa mwananyamala na kijitonyama.
 
Back
Top Bottom