Kiswahili sanifu kinapotea, ni janga kubwa

Mpucha

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2012
Posts
1,273
Reaction score
1,662
Naandika kwa masikitiko, ninaposoma magazeti, maandiko mbalimbali nk kwenye mitandao, au hata kusikiliza mazungumzo ya vijana wetu wa leo nagundua kuna shida kubwa sana kwenye lugha yetu, herufi "h" imepotea kabisa, mfano ni maneno yanayohitaji" H" yanapewa "a, e, i,o,u" mfano akuna, ata kidogo, atari, iyo, apo nk nk ni mfano mdogo tu, hii inaashiria nini, kwamba walimu pia ni tatizo ?
 
Shehe, shida ya lugha ni janga kubwa,ukweli ni kwamba hii hali ni taswira na 'vivid reflection' ya El'mu yetu..
Kuanzia aliye juu mpaka sie kina pangu pakavu,hii lugha kwetu ni dhofuli hali...
HATUJUIII..!! na usiombe usikilize hizi FM radio stations za siku hizi..
Kiiengereza hilo ndio janga kuanzia kwa 'wanene' mpaka watoto wetu,Kiswahili lishakuwa janga nalo..kusoma hatupendi,kujifunza hatutaki..tooba yaraabi....nakwambia ukikutana na kijana wa leo umri aghalabu wa miaka 15 - 35 ukamwambia mzungumze nusu saa Kiswahili bila kutia neo la 'kidhungu' na makosa ya matamshi ya a,h,l na r.
Kakanipime siku hiyo ntakutumia 'hela' na hicho kiiengereza ndio kabisa ataongea sentensi za Telenovela,American series na 'slang' ya hapa na pale...
UKWELI NI HIVI,,HATUJUI LOLOTE..NA HATUTAKI KUKUBALI HILO..
 
Naandika kwa masikitiko, ninaposoma magazeti, maandiko mbalimbali nk kwenye mitandao, au hata kusikiliza mazungumzo ya vijana wetu wa leo nagundua kuna shida kubwa sana kwenye lugha yetu, herufi "h" imepotea kabisa, mfano ni maneno yanayohitaji" H" yanapewa "a, e, i,o,u" mfano akuna, ata kidogo, atari, iyo, apo nk nk ni mfano mdogo tu, hii inaashiria nini, kwamba walimu pia ni tatizo ?
Namkumbuka mwalimu wangu wa Kiswahili shule ya msingi na form 1 na 2 walinipa msingi mzuri sana wa hii lugha adhimu kabisa.

Huwa nakereka sana nikikuta mtu hajaweka H panapotakiwa au amechanganya R na L
 
Tena unamsikia kiongozi kbs anatamka maneno hadharani (L)aisi, Tabo(L)a, (L)amani, Ba(L)aba(L)a na mengine.
Wewe ni yale yale tu, 'kbs' ndio vitu gani.... nachukia uandishi wa aina hii hasa akiandika ME.
 
Naandika kwa masikitiko, ninaposoma magazeti, maandiko mbalimbali nk kwenye mitandao, au hata kusikiliza mazungumzo ya vijana wetu wa leo nagundua kuna shida kubwa sana kwenye lugha yetu, herufi "h" imepotea kabisa, mfano ni maneno yanayohitaji" H" yanapewa "a, e, i,o,u" mfano akuna, ata kidogo, atari, iyo, apo nk nk ni mfano mdogo tu, hii inaashiria nini, kwamba walimu pia ni tatizo ?
Yaani ni aibu kubwa, kiingereza hatujui na kiswahili sasa hatujui! Hata ukiangalia mabandiko ya huku utasikitika, mtu badala ya kuandika 'hata' anaandika 'ata', badala ya kuandika 'huko' anaandika 'uko'! Kwenye magazeti makini kama Mwananchi, mambo ni hayo hayo kama hiyo 'ayo ayo.

Vv
 
Kwenye suala la mazungumzo hasahasa ya vijana sio shida, vijana always huwa wana lugha zao.

Hata kwenye maandishi pia lazima ujiulize je ni aina gani ya mazungumzo.Kama sio ya kiofisi sio kesi.Lugha huwa ipo tofauti kulingana na class
Sijakuelewa, kwa mtazamo wewe hilo sio tatizo
 
Habali, balua, safali, Shelia...nakereka sana mtu anaposhindwa kutofautisha matumizi ya L na R
Hilo sio kosa la kushindwa kujua lugha, ni athari za lafudhi, kuna makabila hawana 'r' na mengine hawana 'l' kwa hiyo wanachanganya.

Vv
 
Uwezo wako wa kufikiri umeishia hapo?

Nakushauri wakati mwingine usininukuu
Sawa mkuu, rejea kwenye mada ni uchafuzi wa kiswahili.... endelea kukosoa watu huku wewe ukiandika 'kbs'.
 
Acha kunichekesha bwana [emoji38]
Yani unamsikiliza unabaki unashangaa hivi anafanya makusudi au ni kwa bahati mbaya? Lakini kama ni kwa bahati mbaya mbona kila wakati anarudia kutamka vile vile ambavyo si sahihi!
 
Naandika kwa masikitiko, ninaposoma magazeti, maandiko mbalimbali nk kwenye mitandao, au hata kusikiliza mazungumzo ya vijana wetu wa leo nagundua kuna shida kubwa sana kwenye lugha yetu, herufi "h" imepotea kabisa, mfano ni maneno yanayohitaji" H" yanapewa "a, e, i,o,u" mfano akuna, ata kidogo, atari, iyo, apo nk nk ni mfano mdogo tu, hii inaashiria nini, kwamba walimu pia ni tatizo ?
Kweli kabisa kiswahili sanifu ndiyo kwaheli kabisa mtu anaandika eti "kabisa" inakuwa "kabixa" sijui kunachuo au shule inayofundisha hivo sikuizi
 
Back
Top Bottom