Kiswahili sanifu kinapotea, ni janga kubwa

Kiswahili sanifu kinapotea, ni janga kubwa

Kwa sasa hakuna kiswahili cha kuandika wala kuzungumza, kama hiyo mifano uliyoitowa, pasopokuwa na H huwekwa na panapohitajika haiwekwi. Jana namsikiliza Daktari anasema tusile WANGA kwa wingi , ninavyofahamu mimi WANGA ni witches na uwanga ndio starch, sasa huu mkorogo upo katika jamii yote hata wasomi. Inasikitisha
 
Mtu anakwambia mama yangu. Yangu ni kiswahili gani?
 
Hilo sio kosa la kushindwa kujua lugha, ni athari za lafudhi, kuna makabila hawana 'r' na mengine hawana 'l' kwa hiyo wanachanganya.

Vv
Hapa kuna huyu msanii anaitwa Darasa, kila nikimsikiliza mahojiano yake yeye kwenye kila L anatumia R, nadhani ni moja ya watu wasiokua na matamshi ya L kwa sana.

Ila sio siri inakera sana kusoma ujumbe wa mtu mzima aliyesoma shule msingi na sekondari kushindwa kuandika maneno ipasavyo..
 
Lugha yoyote ni mapokeo toka kwa waliotangulia kuizungumza ile lugha kama chombo cha mawasiliano baina yao. Wanaopokelewa wakiwa wanaongea lugha sanifu na yenye ushwawishi kwa msikilizaji, basi humshawishi naye kujifunza kwa mbinu zaidi ili naye awe mwanagenzi katika lugha husika.

Kama kutakuwa na changamoto kwa waliopokelewa lugha ni dhahiri shayiri kwamba hata watakaopokea basi pia wataiendekeza hiyo changamoto kwa kiasi kikubwa sana. Kwa mintarafu hiyo inatupasa sie ambao nio wajuvi wa lugha tuijitahidi katika mazungumzo yetu kuizungumza kwa kina na ufasaha, kuiandika kwa madoido ili ivutie na wengine na hata tunapojivunia kwamba kiswahili ni lugha yetu basi isiwe tunasifia kitu ambacho wenyewe hakituburudishi,

Unapojifunza lugha unatakiwa uwe na shawishi ya kujua zaid lugha, na bahati mbaya lugha ya kiswahili ni pana sana kuokana na chimbuko lake na jinsi ambavyo wanajamii wameipokea katika sehemu husika. kuna lahaja ya kiunguja, kimtan'gata, kilamu ambao wanazungumza kiswahili kimoja ila kuna baadhi ya maneno huwa hawasikilizani. kwa lahaja ya kiunguja mtu atakwambia tungule ila kwa bara tunasemaa nyanya, au viazi mbatata kwa unguja ila tanga wanaita viazi ulaya au mviringo.

Nadhani tuwe na bidii ya kujivunia urithi wetu kwa vizazi vya baadaye ili nawe waweze kuwaridhisha vizazi vyao kwani kama wazee wetu wasingelikuwa na ufahamu mzuri na kuipokea hii lugha adhimu basi hata sie leo tusingekuwa twaweza dadavua ambo kama hivi.

Lugha ni fahari ya muongeaji
 
Mkuu
Nimetembelea tovuti nyingi za wazungu, wakenya, wa uganda, na wanaijeria, huwezi kukuta ugonjwa kama huu wa watanzania.

Sisi hatujui lolote. Kiswahili hatujui wala Kiingereza hatujui! Hii inaakisi mfumo mbovu wa elimu ambao kusema kweli watu wanaenda shule kusomea ujinga! cc FaizaFoxy

"Illiteracy level" ya Tanzania ni kubwa sana maana tuna watu waliohitimu mpaka vyuo vikuu lakini bado ni ILLITERATES. Tuna mambumbumbu mengi sana yasojua lugha, si kuandika wala kuongea!!

Mungu tusaidie!
Mkuu,ndiyo haya niliyosema na tunayosema,wadau wanasingizia ooh,athari za lugha mama 'Vernaculars'
Mimi nakakataa katakata,kwenye lugha mambo ya msingi ni Sarufi na misamiati sahihi,mbona tunaangalia runinga tunawasikia waMalaysia,wa Sauzi n.k wanaongea lugha fasaha,athari haziondoki..mie chuo tulikuwa na profesa Muholanzi kasoma Uingereza,kafundisha na kuishi "Anglophone countries' lukuki mbona akizungumza unamwelewa vizuri na achapii kama sie

Alitwambia Netherlands wanatumia kiingereza kama sie na zaidi ya 50% ya watu wao wanakisoma mashuleni na kukizungumza..
Mfano mdogo kwa wapenda mpira wa miguu wasikilize 'Dutch footballers' mbona wanakizungumza na unaelewa..
Haya mambo ya lugha mama yapo dunia nzima.

Hata Kiingereza,kuna Eire,Gaelic,Scotch n.k pia Kichina hakifanani kuna Mandarin,Cantonese n.k hizo ni lahaja tu,shida yetu ni ' good command in grammar and fluency' kwenye kila upande..
Yaani Kiswahili tatizo,Kiingereza janga na hizo lugha mama mnazojifichia kwamo kwishnei safari ya kaburi ishafika..
Vijana wangapi tuliozaliwa mid 70s,80s na millennials wanaeza zungumza Kisikuma,Kisambaa,Kiyao au Kihaya kwa ufasaha zaidi ya salamu na 'surnames' kwenye vyeti vya kuzaliwa na shule..

Mimi sio 'linguist' ila kwa mwendo tushapoteza identity yetu kwenye suala la lugha na utaifa,najua kuna 'pro-maendeleos' humu mtatema povu,ila ukweli usemwe..mfano tu,mie nimesoma na 'magabachori' Aga Khan schools,baadhi walikuwa marafiki ila ukifika makwao,salamu moaka maongezi basic ni kiGujarati,Urdu,Hindi...na wengine tunawapa hadi madaraka mfano Manji,Mo,yule jamaa wa Babati n.k hawajui vizuri Kiswahili..hii ni dharau na makusudi,kwa sababu hawaoni mfano kwetu..Nendeni kwa wenzetu Baltic na Nordic countries,Germany,Holland na Scandinavia..sheria ya kwanza ya kuishi kwao na 'integration' ni 'proper language skills and command' hutaki ondoka..
 
Kweli integration kwa wenzetu ni muhimu sana kwa kila sehemu na lazima ujue hutaki utabaki kuwa mbumbumbu tu
Lakini tukubali sisi ni wabaguzi kuliko wao
 
Na hii athari yake inakuja mpaka kwenye kutamka majina ya Watu, Mtu inakuwia vigumu kufahamu fulani anaitwa Lama au ni Rama anayetamka anakosea.

Mimi mpaka leo sifahamu jina halisi ni Dokta Lwaitama au Rwaitama kwa sababu kila Mtangazaji/Mwandishi anatamka/andika kivyake.
Ni kweli,watu wa 'Lake Zone' wana hiyo shida sana,nakiri mimi mmoja wa wazazi wangu ametokea huko..niliwahi muuliza mjomba angu mmoja ni 'lingust' mahiri na profesa wa Kiswahili,,aliniambia makosa ya mwanzo yalifanyika enzi uokoloni na Wamsionari wakiwa wanadahali watoto mashuleni pia na wao wana lahaja nyingi mfano Wahaya,kuna Kiziba (Bukoba district,Misenyi na Bukoba Vijijini),Kihanja( Muleba),Ihangiro(Muleba),Kyamutwara(In beween Muleba na Bukoba vijijini,along highway Muleba to Bukoba town) Kinyambo( Kyerwa na Karagwe).
Hizo sehemu zina 'intonations na vocal sounds' za alfabeti kama a,h,r na l..na waalimu wa awali haza wakoloni na Wamisionari kwa ugeni wali'standardize' matokeo yakawa hayo,unakuta jina hilo let's say Muleba ni KaRugendo, Kiziba ni KaLugendo, Lwaitama huku,Rwaitama kule,Rwakibalila huku Lwakibalila kule..n.k
Mengine nishasahau mpaka nkimtembelea au 'nkibumiana' nae nimuulize,acha uvivu unaeza 'mgoogle' ukipata muda Professor Mugyabuso M.Mulokozi na mwenzake Kulikoyela Kahigi..walikuwa TUKI na TATAKI 'for a very long time'wameandika sana mabo ya sarufi,bahati mbaya mimi sio linguist ..wadau wengine wataelezea zaidi ikiwapendeza...
 
Mkuu,mimi siongelei ubaguzi hapa,naongelea 'identity' na 'language crisis' tulio nayo..
Hivi mtu akikuuliza Ujerumani,UK au Finland au Urusi unawaza nini kichwani mwako..
Kwanza ni lugha,hata sie ebu ona,Kiingera( England),Kiarabu( Arabs) huoni "mental picture' unayotengeneza kichwani mwako??
Najua suala la lugha ni mjadala mpana,kuna mataifa yana 'ethnicity' nyingi mfano Indonesia,zaidi ya 300 lakini waweza ku 'adopt walau lugha moja popular Bahasa ndiyo identity yao,Malaysia wameforce Malay,India wameforce Hindi..Algeria,Kiarabu ingwara kuna Kabylie na Berber..

Sie pia tuna bahati mtangamano wa pre-colonial era na ukoloni wenyewe ulitengeneza Kiswahili ingawa tu jamii nyingi zaidi ya 120..
Nyerere akatumia hizo advantage na 'king' Kiswahili ikawa 'unifying language'
Kwaiyo ni muhimu kukipa survival and growth mechanism,nielewe hapa..SIKITAI DUAL LANGUAGE SYSTEMS HATA ADOPTION YA ENGLISH AS LINGUA FRANCA..SO LONG AS TUKUBALIANE..LAKINI HUACHI LUGHA YAKO ATI KISA UPUUZI..

Mfano Israel uses English in almost everything,kuna waisraeli wageni na kizazoi kipya hakina hata good command an fluency ya hiyo wanazidiwa hata na 'maadui zao pendwa' waarabu..lakini hawaichi...
Panama,official language ni Spanish,lakini ni watumiaji waakubwa wa kiingereza kwa sabau ya biashara na mfereji..
Habari ya kuwa dual,trilingual ama multiple kwangu mimi sio mjadala wala tatizo,hayo ni maamuzi wa shirikishi kama taifa na watu...linazungumzika na kuamulika..
HASIRA YANGU NI UMBU MBUMBU WETU KWENYE KILA LUGHA..hata ambayo tunaiongea na kuitumia kila siku hadi kuiimbia 'ubongo wa fleva' kama NYEGEZI....
 
Kirare..
Sie ugomv
Lugha yoyote ni mapokeo toka kwa waliotangulia kuizungumza ile lugha kama chombo cha mawasiliano baina yao. Wanaopokelewa wakiwa wanaongea lugha sanifu na yenye ushwawishi kwa msikilizaji, basi humshawishi naye kujifunza kwa mbinu zaidi ili naye awe mwanagenzi katika lugha husika.

Kama kutakuwa na changamoto kwa waliopokelewa lugha ni dhahiri shayiri kwamba hata watakaopokea basi pia wataiendekeza hiyo changamoto kwa kiasi kikubwa sana. Kwa mintarafu hiyo inatupasa sie ambao nio wajuvi wa lugha tuijitahidi katika mazungumzo yetu kuizungumza kwa kina na ufasaha, kuiandika kwa madoido ili ivutie na wengine na hata tunapojivunia kwamba kiswahili ni lugha yetu basi isiwe tunasifia kitu ambacho wenyewe hakituburudishi,

Unapojifunza lugha unatakiwa uwe na shawishi ya kujua zaid lugha, na bahati mbaya lugha ya kiswahili ni pana sana kuokana na chimbuko lake na jinsi ambavyo wanajamii wameipokea katika sehemu husika. kuna lahaja ya kiunguja, kimtan'gata, kilamu ambao wanazungumza kiswahili kimoja ila kuna baadhi ya maneno huwa hawasikilizani. kwa lahaja ya kiunguja mtu atakwambia tungule ila kwa bara tunasemaa nyanya, au viazi mbatata kwa unguja ila tanga wanaita viazi ulaya au mviringo.

Nadhani tuwe na bidii ya kujivunia urithi wetu kwa vizazi vya baadaye ili nawe waweze kuwaridhisha vizazi vyao kwani kama wazee wetu wasingelikuwa na ufahamu mzuri na kuipokea hii lugha adhimu basi hata sie leo tusingekuwa twaweza dadavua ambo kama hivi.

Lugha ni fahari ya muongeaji

Kirare,

Mie binafsi shida yangu sio lahaja,misamiati au diversity ya lugha,hata hizo lugha kongwe zinaazima misamiati kibao..
Kaangalie Queen's English imeazima misamiati mingapi toka Kihindi,Kiswahili n.k, American English imeazima maneno mengi ya Native Americans..over 10%..
Shida ni sisi wa leo na hao wa jana 'fluency and excellent command of grammar na mengineyo' kwenye lugha yetu Kiswahili..
Kwenye Kiiengezereza huko ndio jahazi lilishazamia bahari Nungwi siku nyingi..'ea hostage,rite track only work n.k' atusaidie Mola tuu!!
Mnamkumbuka Philip Mulugo alichotufanya kwenye mkutano mwaka 2014...ukitoka hapo nipe majibu mujaribu braza...
Bahati mbaya mtandao unazingua nitaupload usiku...
 
Kwenye suala la mazungumzo hasahasa ya vijana sio shida, vijana always huwa wana lugha zao.

Hata kwenye maandishi pia lazima ujiulize je ni aina gani ya mazungumzo.Kama sio ya kiofisi sio kesi.Lugha huwa ipo tofauti kulingana na class
Mkuu haya mambo yanachukuliwa Poa kwenye Message na text za simu tu; Ukijaribu kufanya hivyo kwenye Document Official ambayo itasomwa, basi amini kwamba utaonekana kilaza na Document yako haitakuwa considered;

Mimi pia nimeliona hilo, ila most of times kwenye text, chats za simu; kwenye official document sijaona bado;
 
Mm nikiona mtu anachanganya R na L namuona ni mjinga wa hali ya juu....mfano Kaburi anasema kabuli.....Msaraba/msalaba...Gari/Gali.... Askari/askali....Jaribu/Jalibu....ukichanganya hapo nakuona kiazi...
Nilimwacha mpenzi wangu kwa sababu hii!
R na L maana ni kipimo tosha cha 'IQ'
 
.
IMG_5057.JPG
 
Back
Top Bottom