Kiswahili sanifu kinapotea, ni janga kubwa

Kiswahili sanifu kinapotea, ni janga kubwa

Unakuta mtu anasema "Tukio limetokea majira ya saa tatu usiku"
 
Na hii athari yake inakuja mpaka kwenye kutamka majina ya Watu, Mtu inakuwia vigumu kufahamu fulani anaitwa Lama au ni Rama anayetamka anakosea.

Mimi mpaka leo sifahamu jina halisi ni Dokta Lwaitama au Rwaitama kwa sababu kila Mtangazaji/Mwandishi anatamka/andika kivyake.
 
Unakuta mtu anasema "Tukio limetokea majira ya saa tatu usiku"
Au utasikia "Mtu mmoja ameweza kufa".

Media zimejaa Watu wasio sahihi kabisa na Mamlaka zipo zinaangalia tu.
 
Habali, balua, safali, Shelia...nakereka sana mtu anaposhindwa kutofautisha matumizi ya L na R
Xaxa vipi mxee.

Naishi sanawali ya juu. Kesho nitakuja kukuona iri tifanye kazi mahari furani.

Tujivinjali ote. Mimi mtu wa hivi kwanza najua hana akili kabisa na sitaki kumsikiliza.

Hili limenifanya hata viongozi wakubwa nisiwasikilize wanaongea lugha yao waijuayo wenyewe.
 
Kwenye suala la mazungumzo hasahasa ya vijana sio shida, vijana always huwa wana lugha zao.

Hata kwenye maandishi pia lazima ujiulize je ni aina gani ya mazungumzo.Kama sio ya kiofisi sio kesi.Lugha huwa ipo tofauti kulingana na class

Ukiambiwa lugha za vijana au lugha za ofisini,hapa huwa tunazungumzia msamiati,mbali na ufasaha.

Ufasaha wa lugha haujalishi msamiati unaotumiwa. Ndio maana pakawa na lugha ya vijana,lugha ya kifani,lugha ya kiofisi.

Kwahiyo sio kwamba kisa ni lugha ya vijana ndio isiwe fasaha.

Ufasaha una angalia pia matamshi ya maneno.

Sasa mathalani kimtaa mtaa au sisi vijana huwa tunatumia tamko "Kilaza" kwa umoja una kuta mtu anasema "Kiraza".

Nakuja kuendelea haoa nilipoishia....
 
Tatizo hii ya kufupisha maneno imejitokeza kwa sababu ya ujumbe ya SMS kwenye simu. Watu walianza kukatisha herufu ili kuokoa muda wa kuandika. Ni tatizo si ya kiswahili tu, hata kiingereza utakuta maneno kama coz (because), rite (right), nk
 
Yaani uko kama mimi yaani eti jitu zima linaandika ww,nn,mm,vzr, hv, khaa ila siku hizi naanza kuzoea maana asilimia 90 ya watu wanaandika hivyo siku hizo

Ushawahi kuwakanya watu hao ?
 
Hao waandishi wa habari wanaochanganya L na R wanaboa sana wanapoandika, "There is a big ERECTION coming" wakiimanisha ELECTION!
 
Ushawahi kuwakanya watu hao ?
Siku hizi huwa nakausha tu maana wengi wao ukiwaambia wanaona una gubu kwa kuwa kwao ni kitu cha kawaida kabisa. Kuna mtu mmoja enzi hizo graduate kabisa alikuwa ananiandikia x badala ya s nikamwambia aisee alinitolea povu balaa eti nimuondolee ushamba wangu wa CASS ( college niliyosoma kipindi hicho ilikuwa inaitwa hivi) na eti ningekuwa nimesoma UDBS kama yeye ningekuwa mjanja kama yeye. Nikasema hewalaa ila najua ukikua utaacha
 
Hutakiwi kuchoka kuwakerebisha.

Je unafikiri njia uliyo tumia kumrekebisja ilikuwa sahihi ?
 
Siku hizi huwa nakausha tu maana wengi wao ukiwaambia wanaona una gubu kwa kuwa kwao ni kitu cha kawaida kabisa. Kuna mtu mmoja enzi hizo graduate kabisa alikuwa ananiandikia x badala ya s nikamwambia aisee alinitolea povu balaa eti nimuondolee ushamba wangu wa CASS ( college niliyosoma kipindi hicho ilikuwa inaitwa hivi) na eti ningekuwa nimesoma UDBS kama yeye ningekuwa mjanja kama yeye. Nikasema hewalaa ila najua ukikua utaacha
Hutakiwi kuchoka kuwarekebisha.
 
Mm nikiona mtu anachanganya R na L namuona ni mjinga wa hali ya juu....mfano Kaburi anasema kabuli.....Msaraba/msalaba...Gari/Gali.... Askari/askali....Jaribu/Jalibu....ukichanganya hapo nakuona kiazi...
Hivi sahihi ni
Msaraba kweli na sio msala
 
Namkumbuka mwalimu wangu wa Kiswahili shule ya msingi na form 1 na 2 walinipa msingi mzuri sana wa hii lugha adhimu kabisa.

Huwa nakereka sana nikikuta mtu hajaweka H panapotakiwa au amechanganya R na L
Kuna Mwl mmoja ana Shahada ya uzamili katika lugha lakini kwa kuchanganya r na l ni bingwa.
Hapo ndio utajiuliza maswali yasio kuwa na idadi.
 
Wengine wanaona wako sawa kabisa kutumia hayo maneno kwa mfano mtu anawasalimia HABALI ZENU
 
Nachukia sana nikisikia mtu anaseme "apana" "akuna" na maneno yanayofanana na hayo.
 
Dhofuli manake hoi au taabani,isyojiweza..fasiri hii ni kwa uelewa wangu mie ukitaka ufafanuzi zaidi tembelea tafuta kamusi mtandao ya TUKI au TATAKI...
 
Back
Top Bottom