Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
- Thread starter
- #41
Mazindu...Baba yangu as i said, mimi binafsi nakuheshimu sana kwanza kwa UMRI wako na hata kwa maandishi yako; sijapingana kabisa na historia yako unayo iandika na wala sijasema kwamba kile nilicho kisoma shuleni kuhusu historia ya Tanganyika/Tanzania ndio cha kweli, laa hasha! Nilicho kisema ambacho naendelea kukisisitiza ni kwamba, somo la historia huwezi ku prove ukweli wake, nimejerea mambo kadhaa kwamba hata historia ya Mapinduzi ya Zanzibar kile tulicho fundishwa shuleni ni tofauti na tunacho ambiwa na wazee wa Kizanzibar ambao wapo hai to date, nimemtolea mfano mzee Visram Kassam, huyu ni mwandishi mkongwe, nimeanza kuzoma makara zake tokea mwaka 1984 alipokua akiandika gazeti la Mzalendo those years, ameendelea kuwepo akilini mwangu hadi sasa nikiwa na umri wa utu uzima; now coming back to your articles, mimi sijui na sina hakika kama unayo yasema ni ya kweli au na wewe umeongeza CHUMVI, sina proves kwasababu ile ile tu, HISTORIA huwezi kuithibitisha, ni mambo ya mtu kuweka kumbukumbu zake na mwingine anaweza kuzipotosha atakavyo na hasa kama mlengwa unamchukia au unampenda sana, kwa unayemchukia, the law of nature says, "hutayasema mazuri yake hata kidogo, utataka yasijulikane" mfano wako ni kwamba kwenye maandishi yako, huwezi kuzungumzia kabisa kitendo cha Nyerere kunyang'anya shule na taasisi za dini yake ili hata wasio wa dini yake (nimekwepa kusema Waislam ili twende sawa ) ili Watanzania wasome; hilo hakuna sheikh ambaye atalizungumza, lakini ungependa kuwaweka watu unao wapenda (may be wengine nao waliwaficha ili tusiwajue ) ili wajulikane na hapa ndio shida ya somo la historia inapokuja kwangu, NO PROVES. Ingekua ni sayansi, it doesnt matter whether we are friends or not, ukweli wake UPO Maabara. Can site one of the example; mhe rais wa awamu ya tano alipingana sana na actions za kudhibiti CORONA nchini mwake, hadi sasa hivi watu wanamzodoa kwa maneno, lakini tuwaulize kivitendo, alicho kikataa Magufuli, leo wanafanya nini tofauti na alicho kisema Magufuli? Well, dunia anafanyaje sasa tofauti na alichokua anasimamia Magufuli? Hiyo ndio sayansi, unampenda au unamchukia haijalishi, ukweli upo!
Mimi nazugumza historia ninayoifahamu ya uhuru kwa ''facts.''
Mathalan nakuaambia kuwa katika mswada wa kitabu cha Kleist Sykes ameandika vipi waliasisi African Association mwaka wa wa 1929 na kawataja ndani ya mswada hawa wafuatao kuwa ndiyo waasisi: Cecil Matola (President), Klesit Sykes (Secretary), Mzee bin Sudi, Zibe Kidasi, Ibrahim Hamisi, Seleiman Majisu, Ali Said Mpima, Rawson Watts na Raikes Kusi.
Hii ni ''fact'' haina ubishi na haiwezi kuingia kwenye hayo unayosema kuwa huwezi kuwa na ithibati.
Kleist kaandika na nimekupa ushahidi wa rejea ya seminar paper Idara ya Historia Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam ba kitabu cha John Iliffe.
Sasa hiyo chumvi itatoka wapi?
Kwa Iliffe au kwangu?
Taarifa hii hakuna katika kitabu walichohariri Temu na Kimambo, ''A History of Tanznaia,'' (1969) wala katika kitabu cha Chuo Cha CCM Kivukoni (1981)wala katika wasifu wa Julius Nyerere (2020) kitabu kilichoandikwa na Prof. Shivji at. al.
Kuhusu elimu zipo ''facts.''
Serikali iliivunja EAMWS wakati wanajiandaa kujenga Chuo Kikuu mwaka wa 1968 na jiwe la msingi Nyerere ndiye aliyeliweka.
Katika miaka ya 1970 Organisation of Islamic Conference (OIC) walitaka kujenga Chuo Kikuu Tanzania, serikali ikakataa kutoka kibali OIC wakaenda kujenga chuo hicho Mbale, Uganda.
Halikadhalika shule za Kanisa zilitaifishwa lakini Waislam hawakupewa nafasi ya kusoma.
Kulikuwa na mfumo ndani ya Wizara ya Elimu ambao watendaji wa Kanisa walijipanga katika nafasi zote kuzuia Waislam wasisome.
Uko ushahidi.
Ndipo nakuambia usijadili kitu ambacho huna ujuzi nacho.
Usidhani mimi niko hapa kufanya maskhara.
Hizi nilizokuwekea hapa ni "facts," ukisoma kitabu cha Sykes utajifunza mengi.
Ndiyo maana kitabu hiki kimechapwa mara nne toka 1998 na sasa kinakwenda toleo la tano.
Usiwe na haraka ya kuja hapa kujadiliana na mimi kwani wewe haya hayakuhusu wa kuwajibu Waislam ni serikali iseme kuwa Mohamed Said ni muongo hakuna ukweli katika haya anayoandika.