Unafanya kazi nzuri Mtumishi..Ukisoma kitabu cha Enoko, anasimulia kuanzia mwanzo mpaka mwisho, jinsi alivyotokewa na malaika wawili, na kama ilivyo kwa malaika wote wanapowatokea wanadamu huanza na neno “Usiogope”.
Kwa nini?
Ni kwa sababu malaika ana muonekano wa kutisha, kwa binadamu, huwezi kuwa kawaida tu unapomuona malaika ametokea mbele yako, ndiyo maana husema usiogope.
Aliambiwa Mariamu Magdalena pia.
Enoko alianza kuwaelezea malaika ambao walikwenda chumbani kwake wakati amelala.
Kwanza walikuwa wakubwa, wenye mbawa lakini sura zao zilikuwa na mng’ao mkubwa kama jua lakini macho yao yalikuwa yanawaka kama taa.
Katika maisha yake, anasema hakuwahi kuwaona viumbe wakubwa namna hiyo.
Lipsi zao zilikuwa na moto, mbawa zao zilikuwa na mchanganyiko wa rangi mbili, zambarau na dhahabu inayong’aa kupita kawaida, mikono yao ilikuwa ni meupe kama theluji.
Hebu fikiria unakutana na kiumbe kama hicho, hutoogopa? Ndiyo maana walimwambia kwanza, usiogope.
Anasema malaika hao walisimama pembeni ya kitanda chake na kumuita kwa jina lake, Enoko akainuka na kuwaangalia.
Enoko aliogopa, anasema uso wake ulitetemeka mno lakini malaika mmoja akamwambia: “Usiogope”.
Walimwambia walitumwa na Mungu kumchukua na kumpeleka mbinguni, kwa yote ambayo angekutana nayo huko basi angewaambia watoto wake, wajukuu na vizazi vyote mbeleni.
Anasema hakutaka kuwapinga, akatoka na kwenda kuonana na watoto wake, Mathusal, Regim na Gaidad, akawaambia kuhusu malaika hao na kile walichomwambia, baada ya hapo, wakamchukua na kuanza kupaa naye kwa kumbeba kwenye mbawa zao.
View attachment 3134566
Naomba sana Ndugu zangu wanaobeza Maandiko ya Manabii wengine kuita ni story za kufikirika na wengine kusema ni za mashetani wajitathimini sana..
SIRI AMBAYO WENGI HAWAJAWAHI KUIFAHAMU NI KUHUSU UNABII, MAANDIKO MATAKATIFU NA WAPI YAMEANZIA (ORIGIN)
Wengi wanaamini Biblia ya kwanza ni Hebrew Bible ila sio kweli, na hizi Bible za King James na Nyingine nazo sio za kwanza.. BIBLIA YA ETHIOPIA ndo BIBLIA KONGWE na imeandikwa kwa Lugha yao GE'EZ ina vitabu 81-88 na kitabu cha Nabii Enock kipo hakikutolewa..
SIRI AMBAYO WENGI WAMEFUNGWA HASA UFAHAMU ni kushindwa kukaa kutafakari hata kwa kupitia yaliyojili kwa Wana wa ISRAEL pale MISRI, WANA WA ISRAEL HAWAKUWA HAWA MNAOWATAJA (WAZUNGU)..
Kuna siri kubwa iliyofichwa ambayo inagusa KANISA LA ORTHODOX ambalo ni kongwe kabla ya Makanisa ya Roman Catholics, Lutheran na mengine yaliyoanzishwa na Falme zenye Nguvu na Wanaharakati wa kale kama Martin Luther nk.. Kanisa ya Orthodox pale Ethiopia bado linafundisha kwa Injili kwa kufuata miongozo na tamaduni za kale.
Kufanya story iwe fupi ni hivi.. Hao WAZUNGU (Waisrael wa sasa) HAWAJAWAHI KUWA WATUMWA CHINI YA PHARAO PALE MISRI.. Hata wakati Musa akionesha Ukuu wa Mungu mbele ya Pharao hadi anaweka mkono wake kwapani unatoka mkono ukiwa na weupe halafu anarudi hali ya kawaida hiyo isingotokea kwa Musa mzungu kama wa kwenye FILAMU zilizotengenezwa na Wazungu hadi za Nuhu, Yesu nk.. Haya yote yamefanikiwa baada ya Uvamizi wa Julius Ceaser hapa ndo walijua namna ya kuanzisha propaganda wakafanikiwa kututawala kupitia Explorer, Missionaries na MIFUMO waliyoiweka ambayo wamekuja kwa njia nyingine ya kisasa zaidi kututawala bila nguvu bali kwa akili kwa kuamini MAIGIZO YAO. ACHENI KUAMINISHWA KILA JAMBO!
KUMTAWALA MWAFRIKA IMETUMIKA AKILI KUBWA SANA HASA KUTUGOMBANISHA KWENYE DINI na lugha ndo imetumika kuleta tafsiri tofauti ili kutugawa na kuacha kufuata MUNGU WA KWELI WA MABABU ZETU tukaishia kufuata MIFUMO ya wanaotaka kututawala kupitia UDINI..
SIKU WAAFRIKA MKIACHA UDINI na KUFUATA IMANI kwa kumwamini MWENYEZI MUNGU PEKEE badala ya hizi vuta nikuvute za kutafuta Utajiri na Miujiza na kuamini Mataifa fulani ndo yamebarikiwa zaidi yako, ndo tutatoka kwenye kifungo au utumwa wa kifikra.. Fatilieni sana story ya Musa aliwapigania ndugu zake waliokuwa wanafanana nae na hata kwenye Pyramids zimechorwa picha watumwa walikuwa Waafrika pale misri ndo maana hata baada ya kuondoka pale Misri walienda umbali mrefu sana miaka 40 hawakuwa wamefika (inafikirisha sana).. Sasa Israel ya sasa kabla ya 1948 kupitishwa na Wamarekani na Waingereza tayari kulikuwa na nchi kama 7 kuchagua wapi waishi hata maeneo ya East Afrika yalikuwa kwenye list, Argentina pia ila Wazungu wakaona ili kutawala siasa za Middle East bora waingie eneo ambalo Wafilisti walivamia zamani wapewe hifadhi baadae wamewageuka Wafilisti wanasema ni eneo lao wakati wote wale eneo sio lao bali la Waafrika ambao walipewa na Mungu (fatilieni sitaki kuwaingiza kwenye siasa ila nawaonesha historia namna imepikwapikwa).
Kuonekana Primitive leo ni suala la mifumo iliyowekwa kwa WAAFRIKA MUISHIE KUUANA kwasababu ya UDINI, UBINAFSI na ELIMU YA KUKARIRISHANA wao wanazidi kutengeneza vizazi vyenye IQ kubwa.. Kuna watu wanaamini kuna Mwanadamu kapendelewa zaidi kapewa IQ zaidi ya wengine kama Mbarikiwa.. Hii toka napata kuelewa mifumo ya kidunia.. IQ inajengwa na mazingira na mambo unayofuata, ukifuata story za mafundisho ya kupandikizana chuki kamwe huwezi wafikia wazungu wala wachina.. Acheni kuwalisha sumu watoto wenu na vizazi vingine ndo mtaona BARAKA MMEPEWA NA MUNGU..
Story imeanzia kwenye Kitabu cha Enock, ninaamini Manabii walikuwa Waafrika na nitaendelea kuamini mwanadamu wa kwanza kuumbwa na Mwenyezi Mungu alikuwa Mwafrika ndo maana wale waliokwisha vuliwa hili Taji wanabaki kuwabagua Waafrika ngozi yao ili sasa wajisikie vibaya waende kutumia CHEMICAL ZAO wapate Kansa kama wao.. Mwafrika ameumbwa kwa udongo akapewa ngozi yenye kuhimili hali yoyote ila kufuata Tamaduni za nje ndo imepelekea WAAFRIKA HAWANA LENGO MOJA WALA SIO WAMOJA TENA BALI WANAWAZA KUDHURUMIANA na KUUANA.. ACHENI MAFUNDISHO YA CHUKI. FUATA IMANI YA KWELI INAYOANZA NA WEWE, SHIRIKI NA KILA MMOJA KATIKA KUSAIDIANA NA KULETA MAENDELEO KWENYE JAMII ZETU.
ROHO ZA KIBINAFSI NDO UBEPARI WENYEWE UMEWAFANYA WATU KUWA NA ROHO MBAYA.. NITAFUATA UJAMAA SIKU ZOTE MAANA HUKO NDO KUNA UPENDO WA KWELI, SIO HII CAPITALISM KWA KIVULI CHA ELIMU NA UDINI. HATUTAFIKA POPOTE!